Baada ya kama miaka mitano nchi za Afrika(Ikiwemo Tanzania) zitaanza kwenda kununua na kuomba msaada wa chakula Afghanstan.

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Jan 31, 2021
7,224
12,729
Sema tulivyo makauzu hata aibu hatutaona.
Afghanstan kwa sehemu kubwa ni jangwa. Lakini bahati nzuri upande wa Kaskazini imepitiwa na mto mkuwa wa Amu Darya ambao inashare na nchi kadhaa. Sasa ili kuzalisha chakula utawala wa Taliban umeamua kujenga mfereji mkubwa wa umwagiliaji kutoka mto huo na kubadili Hekta laki tano na nusu za jangwa kuwa eneo la kilimo(Hizo ni kama ekari milioni moja na laki tatu). Mfereji huo uitwao Qosh Tepa utakuwa na urefu wa kilomita 285. Kazi ya kuujenga ilianza mwaka 2022 na tayari mpaka sasa kilomita 100 zimeishachimbuliwa.

Mfereji huu utaiwezesha Afganstan kujitosheleza kwa chakula na kuwa na ziada ya kuuza na kutoa msaada. Kwa kasi ya ujenzi wa mradi hu na kwa jinsi Waafghanstan wanavyojielewa, ndani ya miaka mitano nchi za Afrika, ikiwemo Tanzania zitaanza kwenda Afghanstan kuomba msaada wa chakula.

1703512085895.png

1703512666106.jpeg


1703512736659.png


1703512903855.jpeg


1703512941317.jpeg

1703512973394.jpeg
 
Walaaniwe marekani na mashoga zake kwakuiharibu hii nchi
Ila safi sana Afghanistan kuna muda ukipata changamoto zinakujenga sana nazinakufanya uwaze nje ya box
Afghanistan wanapitia changamoto sana kwasasa hasa kwenye upande wa misosi umekua shida kwao
Safi sana taleban
 
Back
Top Bottom