Baada ya jipu la wakala wa vipimo sasa kuhamia NSSF

Baada ya jipu la wakala wa vipimo sasa kuhamia NSSF

Ni kumuunga mkono tu rais ili nchi irudi kwenye mstari. Ila haimaanishi tusimkosoe, tutamuunga mkini ila atambue kuwa pamoja na kumuunga mkono sisi si cheerleaders.
 
Asante mkuu kula like na wewe ,Magufuli akitaka atawale kirahisi ni kuja tu na katiba mpya itakayo beba mfumo mpya naam ni rasimu ya Warioba
Eti Mwakiembe eti kasema kwenye suala la katiba kaambiwa na rais waendelee pale walipoishia...yaani katiba pendekezwa.
 
Yaani hamna kitu kitakua kizuri kwa Magufuli kama kupeleka Muswada bungeni wa kuwapa meno Takukuru na Usalama wa Taifa ,haya mambo ya kupigiana simu kizembe yasinge fanikiwa ,Dau usiye mtaka kaja
Mkuu Unaona Mbali Naunga Mkono Hoja
 
Bomba la gesi Jamhuri tunaomba mukafanye research za haki, je gharama halisi ikoje?.Tija kwaa Taifa maana si kila eneo linaguswa?
 
Dah! Endelea kuwatumbua tu Mheshimiwa Magufuli. You have my full support. Ninasikitika sana kwanini ulichelewa kuwa rais wa nchi hii. Kila mpenda nchi hii, yaani mzalendo wa kweli ni lazima akuunge mkono bila kujalisha utofauti wa vyama. Na ninaipenda sana kauli yako kwamba "hii ni serikali ya John Pombe Magufuli" Ninafarijika kugundua kwamba hii si ile serikali ya genge la watu wachache kuwanyonya wengi. Tumbua tu mpaka waishe wote.
 
Suala la udini halipo hapa kwani ni taasisi ngapi ambazo DG ni wakristo na watu mbona dini zote wapo ndani ya taasisi.hata NSSF mbona wakristu ni wengi kuliko waisilamu.acha wivu wa kijinga kaka
Mkuu tuwekeane milioni moja kila mtu, mimi na wewe tufanye utafiti kwa branch zao za hapa dar tuu
 
Taarifa za ki intelijensia zolizonifika ni kuwa baada ya jipu wakala wa vipimo kutumbiliwa sasa hali ya wakubwa huko NSSF matumbo yako moto na kwa taariza zaidi hivi Leo Waziri mkuu majaliwa alokuwa atembelee NSSF lakini imeahirishwa ghafla.

Taariza toka jikoni watakaotumbuliwa ni mkuu wa shirika, mkuu wa miradi na uwekezaji pamoja na wote waliohusika kufanya miradi ya kisanii hasa daraja la Kigamboni ambako gharama halisi si zaidi ya bilioni 160 ila NSSF waliweka cha juu hadi 260b utakumbuka kuwa Magufuli wakati huo akiwa waziri wa ujenzi alimgomea dau kujenga na kusimamia daraja hilo ila dau alimzunguka kwa JK na hatimae JP aliondolewa ujenzi na kupelekwa uvuvi ndipo dau alipocheza mchezo na mkataba wa ujenzi ukasainiwa.

Kuna taarifa kuwa wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi wakati huo JP alisharudi ujenzi, dau hakumtaarifu JP kuhusu ufunguzi huo kitu kilichomshangaza sana JP. Kwa taarifa za ndani ni kuwa bwana dau alokuwa na dharau sana enzi za JK na aliwaona mawaziri wote kama watunza bustani hata waziri wa kazi enzi hizo alokuwa hawezi kuhoji lolote pale NSSF maana dau akipiga simu kwa JK kibarua hatarini.[/QUOT


Majipu yapo mengi mno. mimi namwonea tu huruma JPM maana atapasua mpaka achoke.Kwenye miradi iliyo kamilika ndio usiseme. Mingi overprised,na imejengwa chini ya kiwango nk. Mfamo kaone UDOM na majengo mengine barabara na madaraja,shule hospital nyingi zilijengwa chini ya viwango pia. Majipu bado yapo Tannesco,DAWASCO,TLR, Vivuko vya kigamboni,(hivyo vinaweza kuua watu wakati wowote,kwa kinakwenda kwa nguvu za Mungu tu!). Mengine Viwanjwa vya ndege.Kwenye bandari zingine maana amegusa Dar Tu.Juzi wazili mkuu amepagua kwenye mita za mafuta kwenye mita za gesi inayonunuliwa njee na kuingizwa nchini je? nenda hizo zingine pia utaona mengi ya ajabu.Kiujumla nchi ilioza kwa ufisadi!!.Sipati picha kama kweli nchi ilikuwa na kiongozi au ni gari lililokuwa linakwenda bila dereva!!tumwombe tu Mungu amlinde hiyo kazi siyo mchezo maana anakata mirija ya wakubwa!
 
Eti Mwakiembe eti kasema kwenye suala la katiba kaambiwa na rais waendelee pale walipoishia...yaani katiba pendekezwa.
Kwa maana kwamba iwekwe rasmi kwa ajili ya kura za maoni ?? Naanza kuona dalili mbaya za utawala wake,Zanzibar na Katiba mpya vingekua sababu ya mimi kumpa kura yangu 2020 vinginevyo anajiweka pabaya
 
Kwa maana kwamba iwekwe rasmi kwa ajili ya kura za maoni ?? Naanza kuona dalili mbaya za utawala wake,Zanzibar na Katiba mpya vingekua sababu ya mimi kumpa kura yangu 2020 vinginevyo anajiweka pabaya
Yeah..wanaamanisha tuelekee kwenye kura za maoni, mimi binafsi kufikia hapo ndipo nikaona UNAFIKI kwenye kauli na harakati hizi za president.
 
Yeah..wanaamanisha tuelekee kwenye kura za maoni, mimi binafsi kufikia hapo ndipo nikaona UNAFIKI kwenye kauli na harakati hizi za president.
Kwenda kinyume na CCM wanachotaka hatothubutu kamwe na akithubutu atakwamishwa ,hizi harakati za kutumbua majipu naanza kuona ni mpango wa wana ccm wenyewe kukiimarisha chama chao kwa ajili ya mbio za uraisi 2020 na sio Serikali ,asipo itisha mchakato wa katiba upya kwa maana ya rasimu ya Warioba ,basi hiyo katiba yao ya kina Chenge na Sita ikifika kupigiwa kura za maoni ,Magufuli atakua ameiridhia na ndio kielelezo tosha cha kuelezea dhamira yake ya unafki ,hata hivyo ni swala la muda tu makucha yake yatakua yameshajitokeza
 
Aha!kumbe hivi vizee vijizi sana mambo gani ya kuongeza mapesa yote hayo 100bil 'Mungu atawaona'.
 
Hureee mambo yameiva sasa dau atapelekwa sirya na board mpya Nssf ikiteuliwa atarudishwa na kufungwa,stay tuened
 
Imeonekana kuwa la Dau sio jipu Bali ni Tumour ambayo ukitoa vibaya mgonjwa anakufa ....utumbuaji wake unaweza kusababisha mtetemeko mkubwa...., inabidi apelekwe kwanza nje asiingilie
 
Back
Top Bottom