Baada ya Hayati Magufuli ni Hussen Bashe

Slowly

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
10,489
34,796
Awamu ya tatu na ya nne tulikuwa na wazir mwenye misimamo mikali kabisa alieitwa John Pombe Joseph Maghufuli, Kwa sasa tuna wazir wa namna hyo hyo anaitwa Hussen Bashe .....

Bashe ni mzalendo , Bashe ni mpambanaji , very young and highly exposed , anayevaa uhusika , mwenye misimamo isiyoyumba na asiyeogopa kukosea pale anapoona Kuna manufaa Kwa Taifa ....

Ukweli ni kuwa katika Baraza la mawaziri hayupo wazir anayepambana kama Bashe , sekta ya kilimo ni ngumu , imetelekezwa mda mrefu na kusababisha mrundikano wa matatizo sugu yanayohitaji roho ya paka kuyasawazisha .... bashe anaenda door to door ni kazi ngumu inayohtaji kujitoa ..... Hujuma ni nyingi but ni ahueni Kuwa Raisi Samia ameendelea kumpa go_ahead

Wananchi wengi wa Taifa hili wanategemea kilimo kama chanzo cha ajira , na huwez kumwelewa bashe mpak uwe kwenye ulingo wa kilimo.

Hvi nini utafanya Kama wazir wa kilimo endapo Mazao wanayolima wakulima wanaishia kupata hasara ????

Utawaletea mbolea , utawaletea mbegu watalima , watanavuna wanapata lakini hakuna kitu, soko la ndani chenga , na la nje umefunga , alaf unasema kilimo ni utajiri , kilimo ni uti wa mgongo , what the fu_ck

Msimu wa mwaka 2019-2020 niliamua kulima ili kutafta mtaji , nililima hekar 3 za mpunga , ilikuwa ni kazi ngumu Sana yenye kuchakaza mwili , mwaka ulianza vibaya Ila tulimaliza Kwa neema ,....lakini ndo nilishuhudia the horror of Tanzanian agriculture, kuna us_enge Sana kwenye kilimo cha bongo

Gharama kuanzia Kukodi eneo mpak kuvuna na kuhifadhi Mazao shambani ilinicost almost 1.8 million .... nilipata gunia kama 60 hivi

Nakumbuka msimu huo mvua zilikubali na watu waliivisha , bei ilikuwa Chini Sana Mchele uliuzwa Kati ya TSH 900-TSH 1100 Kwa kilo.

Ilinilazimu nisubiri msimu mwingine lengo upande kidog ili niuze , daah Kwa kweli ilikuwa ni totaly loss of time , huku nikiwa sina hela kabisa ya kusurvive ,magunia yako tuu ndani.

Serikali ilizuia Mchele kuuzwa nje , Hali hii kiukweli ilifanya wakulima wadogo wadogo Kama Sisi tuumie Sana , na hii ilitengeneza loophole ya uhuni mwingi ufanyike.

Kuna madalali walipata connection ya njia za panya kupeleka Mchele South Sudan na Uganda aisee wale jamaa walitajirika asikwambie mtu , imagine wanachukua Mchele Kwa 900 wanapitisha kimaghumashi wakila sahani moja na mamlaka , wanapiga faida ya kufa mtu, Sisi wanyonge tulikinywea.

Mwisho mwaka 2021 baada ya kusubiria usku usiokucha niliamua kuuza tuu kibabe nikaambulia 2.5 milion ,nikatimkia zangu DSM

Bashe ameamua kuchukua njia ngumu Ila yenye manufaa Kwa wakulima , kuruhusu watu kutoka nje wachukue moja Kwa moja Kwa wakulima nampa hongera japo kuna side effect zake , hiii inasaidia wananchi kupunguziwa makali ya madalali ambao ni moja ya changamoto kubwa kwenye biashara hapa bongo... Kiukweli watu kutoka nje wanakuja na bei isiyo na longo longo

Ingekuwa kipind hiki nilikuwa na uhakika wa kukunja Milion 7 Kwa mtaji wa 1.8 milion ...

Mawaziri mizigo kwenye hii nchi ni wazir wa nishati, mawasiliano na fedha ... Hawa jamaa chenga Sana , baada ya kilimo Bashe apewe nishati
 
May be maana ni ukanda uleule wale wa pwani waliozoea tangu wadogo ili wacheze ngoma nyumbani hawataweza kulisaidia taifa

USSR
 
Hili neno mzalendo ni la kiwaki kinyama!! Utawala wa bongo hakunaga mzalendo zaid ya teacher na moringe.
 
Huna akili hata kidogo! Hivi toka lini maharage mboga ya watu wakipato cha chini kabisa ikawa tshs 4000 kwa kg??

Hivi unamjua Bashe au unamsikia?? Moja ya watu wapigaji ni Bashe kwa taarifa yako!

Bashe ni kijana wa Rostam! Elewa hilo
 
May be maana ni ukanda uleule wale wa pwani waliozoea tangu wadogo ili wacheze ngoma nyumbani hawataweza kulisaidia taifa

USSR
Kassim ni wa hiyo kanda ya Pwani ila vipi anafanana na VICE kwenye upambanaji?
 
Hapo mwisho sijakubaliana, kwa maono aliyo nayo kwenye Kilimo aendelee kubaki hapo at least for some 10 yrs. Tutafika mahali pazuri, lkn pia Serikali isaidie zaidi mechanisation kwenye Kilimo.
 
Huna akili hata kidogo! Hivi toka lini maharage mboga ya watu wakipato cha chini kabisa ikawa tshs 4000 kwa kg??

Hivi unamjua Bashe au unamsikia?? Moja ya watu wapigaji ni Bashe kwa taarifa yako!

Bashe ni kijana wa Rostam! Elewa hilo

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
Ulitaka maharage yauzwe sh ngapi labda , ndio ni kijana wa Rostam we ulitaka awe kijana wa nan
 
Ni kweli ungewza pata 7m kipind hiki sema gharam za uzalishaji kwa sasa zipo juu kuliko kipindi kile
 
Back
Top Bottom