Uchaguzi 2020 Baada ya Dkt. Chiduo (Marehemu) Gairo yapata Dkt. Joel Mmassa mhadhiri UDOM kunyukana kura ya maoni CCM na tajiri wa Gairo mhe. Shabiby

DT125

JF-Expert Member
Oct 19, 2011
266
500
Na mwandishi wetu
Jimbo la Gairo mkoani Morogoro ni kati ya majimbo nchini yatakayokuwa na upinzani mkali. Tajiri wa kampuni ya mabasi ya abiria Ahmed Shabiby awamu hii anakabiliwa na upinzani mkali jimboni kwake.

Mtoto wa mwalimu mstaafu na mzee maarufu wa Gairo Mzee Johnson Mmassa, ajulikanae kama Dr. Joel J. Mmassa msomi wa kiwango cha PhD ya uchumi na mhadhiri wa chuo kikuu kikubwa hapa nchini maarufu kama UDOM ni mmoja kati ya watia nia kuwania ubunge wa jimbo la Gairo.

Wakazi wa mji wa Gairo uliopo mpakani mwa mkoa wa Morogoro na Dodoma barabara kuu ya Dar Es Salaam na Dodoma wanatabainisha kuwa kama Dr. Joel hatachomoa jina lake kwa ushawishi wa aina yoyote toka kwa tajiri Shabiby huenda ikawa ni mwisho wa ubunge kwa Mhe. Shabiby.

Nikiwa njiani kuelekea Dodoma kijana mmoja mkazi wa hapa aliniambia kuwa Gairo baada ya Dr. Chiduo tunakwenda kupata mbunge msomi mwingine mwenye kiwango cha juu cha elimu (Daktari).

Aliendelea kueleza kuwa kwa ushawishi wa pesa ya Shabiby tunaamini ataongoza kwa wingi wa kura ya maoni lakini hata hivyo tunauhakika vikao vya juu vya chama chini ya Mhe. Magufuli havitapitisha jina lake.

Mkazi mwingine alidai kuwa Shabiby pesa yake tunakula kipindi hiki cha uchaguzi akishapata ubunge huwa hatujui mpaka kipindi cha uchaguzi, huwezi kumfananisha na tajiri wa mabasi ya Abood mbunge wa Morogoro mjini ambaye kutokana na pesa yake amekuwa na msaada mkubwa binasi kwa jamii yake.

Mama mwingine ambaye alijitambulisha kwa jina moja la Hadija aliyekuwa akiuza karanga za kuchemsha kwenye ndoo alieleza kuwa tumesikia tetesi Shabiby anawasiliana na ndugu wa Dr. Joel akiwemo baba yake mzazi akiwashawishi kwa fedha ili mwanae ajitoe kwenye kinyanganyiro.

Aliendelea kueleza safari hii tutahakikisha anatoka hata kwa kuchagua upinzani. Mabasi yake hatupatii hata rifti ili tukauze karanga Dodoma kwa kudai tutachafua mabasi yake, ukikosa Abood na Nyehunge za Morogoro kwenda Mwanza siku hiyo hatuendi Dodoma.

Nilipompigia Dr. Joel J. Mmassa baada ya kujitambulisha aliniambia kuwa hakuwa tayari kunithibitishia kama atagombea uubunge wa Gairo, lakini alikiri kuwa huingia mara kwa mara Gairo kuwasalimia wazazi na marafiki zake na amekuwa anafanya hivyo kila wakati siyo kipindi hiki tu cha uchaguzi, kwani yeye amekulia hapo na ana ndugu na marafiki zake wengi.
 
mwayena

JF-Expert Member
Apr 21, 2016
2,792
2,000
Naifahamu Gairo, Namfahamu Dr Joel, Namfahamu A.M. Shabiby,...kwa Aina ya watu wa Gairo jina la Shabiby likirudi atapita asubuhi sanaaa. Ila awamu hii nna mashaka Kama atarudi maana kuna dalili hapatani na mwenye chama. Wakaguru hawahawa wampotezee Shabiby?
 
Bambushka

JF-Expert Member
Jan 9, 2020
728
1,000
Hivi hao wasomi wamesaidiaje hapo Gairo? Zile shida za maji atazimaliza?
Au anakuja kuchumia tumbo!
Wakaguru wanampenda mwarabu.. Dr wa uchumi sijui!

Everyday is Saturday........................... :cool:
 
Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
3,937
2,000
Mhhh! Usikute wewe mtoa mada ndiye huyo Dr. Joel Mmassa mwenyewe umekuja kujipigia chapuo na kupima kina cha maji.

Uzuri Mwenyekiti wenu anawachukia Matajiri na pia anawaamini na kuwabeba sana Madokta wenzake na Maprofesa kwenye teuzi zake! Kwa kigezo hicho tu, lolote linaweza kutokea.
 
Kadhi Mkuu 1

JF-Expert Member
Feb 4, 2015
8,576

Ndiye yeye Dr anapima upepo na kuweka mazingira ya rushwa labda shabiby atakata mshiko wa maana.

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
Munamuge

JF-Expert Member
Sep 22, 2014
610
1,000
Ukiwa safarini ulibahatika kupewa hizo story na hao wafanyabiashara bila hata kuwauliza? Mbona mimi hapo Gairo nimepita zaidi ya mara tatu kwa mwezi huu na sijabahatika hata kutajiwa hizo habari.
 
Mwendigwa

New Member
Jul 6, 2020
1
45
Shida Gairo hatujielewi kabisa. Huyo tajiri wenu amefanya nini cha maendeleo endelevu hapo Gairo? Au ni hivyo visenti mnavyogaiwa wakati wa uchaguzi? Hao wasomi mnaowaita wachumia tumbo wana mishahara mikubwa kuliko mnavyojua nyie. Hawaji kutafuta pesa za kula. Gairo inatakiwa itokehapo ilipo na iwe bora zaidi. Sasa huyo dkt kaongea, ila wasomi ambao hwajaongea lakini watachukua fomu za ubunge gairo wapo wengi safari hii..muda utaongea.....
 
Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
33,509
2,000
Na mwandishi wetu
Jimbo la Gairo mkoani Morogoro ni kati ya majimbo nchini yatakayokuwa na upinzani mkali. Tajiri wa kampuni ya mabasi ya abiria Ahmed Shabiby awamu hii anakabiliwa na upinzani mkali jimboni kwake.

Mtoto wa mwalimu mstaafu na mzee maarufu wa Gairo Mzee Johnson Mmassa, ajulikanae kama Dr. Joel J. Mmassa msomi wa kiwango cha PhD ya uchumi na mhadhiri wa chuo kikuu kikubwa hapa nchini maarufu kama UDOM ni mmoja kati ya watia nia kuwania ubunge wa jimbo la Gairo.

Wakazi wa mji wa Gairo uliopo mpakani mwa mkoa wa Morogoro na Dodoma barabara kuu ya Dar Es Salaam na Dodoma wanatabainisha kuwa kama Dr. Joel hatachomoa jina lake kwa ushawishi wa aina yoyote toka kwa tajiri Shabiby huenda ikawa ni mwisho wa ubunge kwa Mhe. Shabiby.

Nikiwa njiani kuelekea Dodoma kijana mmoja mkazi wa hapa aliniambia kuwa Gairo baada ya Dr. Chiduo tunakwenda kupata mbunge msomi mwingine mwenye kiwango cha juu cha elimu (Daktari).

Aliendelea kueleza kuwa kwa ushawishi wa pesa ya Shabiby tunaamini ataongoza kwa wingi wa kura ya maoni lakini hata hivyo tunauhakika vikao vya juu vya chama chini ya Mhe. Magufuli havitapitisha jina lake.

Mkazi mwingine alidai kuwa Shabiby pesa yake tunakula kipindi hiki cha uchaguzi akishapata ubunge huwa hatujui mpaka kipindi cha uchaguzi, huwezi kumfananisha na tajiri wa mabasi ya Abood mbunge wa Morogoro mjini ambaye kutokana na pesa yake amekuwa na msaada mkubwa binasi kwa jamii yake.

Mama mwingine ambaye alijitambulisha kwa jina moja la Hadija aliyekuwa akiuza karanga za kuchemsha kwenye ndoo alieleza kuwa tumesikia tetesi Shabiby anawasiliana na ndugu wa Dr. Joel akiwemo baba yake mzazi akiwashawishi kwa fedha ili mwanae ajitoe kwenye kinyanganyiro.

Aliendelea kueleza safari hii tutahakikisha anatoka hata kwa kuchagua upinzani. Mabasi yake hatupatii hata rifti ili tukauze karanga Dodoma kwa kudai tutachafua mabasi yake, ukikosa Abood na Nyehunge za Morogoro kwenda Mwanza siku hiyo hatuendi Dodoma.

Nilipompigia Dr. Joel J. Mmassa baada ya kujitambulisha aliniambia kuwa hakuwa tayari kunithibitishia kama atagombea uubunge wa Gairo, lakini alikiri kuwa huingia mara kwa mara Gairo kuwasalimia wazazi na marafiki zake na amekuwa anafanya hivyo kila wakati siyo kipindi hiki tu cha uchaguzi, kwani yeye amekulia hapo na ana ndugu na marafiki zake wengi.
Tupe matokeo
 
Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
33,509
2,000
Shida Gairo hatujielewi kabisa. Huyo tajiri wenu amefanya nini cha maendeleo endelevu hapo Gairo? Au ni hivyo visenti mnavyogaiwa wakati wa uchaguzi? Hao wasomi mnaowaita wachumia tumbo wana mishahara mikubwa kuliko mnavyojua nyie. Hawaji kutafuta pesa za kula. Gairo inatakiwa itokehapo ilipo na iwe bora zaidi. Sasa huyo dkt kaongea, ila wasomi ambao hwajaongea lakini watachukua fomu za ubunge gairo wapo wengi safari hii..muda utaongea.....
Utaongozwaje na mtu ambaye siyo mtanzania? hakuna wazawa?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom