Baada ya Bilionea Shami kudai kutishiwa maisha, wanaomdai wajitokeza na kumwambia alipe deni

DodomaTZ

Member
May 20, 2022
71
107
Baada ya Mfanyabiashara maarufu wa Magari Jijini Dar es Salaam, Samweli Shami maarufu kwa jina la Bilionea Shami kudai kuwa ametishiwa maisha na watu aliodai ni vigogo wa Polisi, amejibiwa na waliojitambulisha kuwa ni wahusika aliofanya nao biashara wakimtaka alipe fedha alizopewa na sio kulalamika mitandaoni.

Wasikilize mwenyewe hapa
Habari ya kwanza ni hii > Mfanyabiashara bilionea Dar es Salaam, adai kutishiwa maisha, akimbia kwa pikipiki kutoroka asiuawe hadi Arusha
 
Watu wanataka uwaonyeshe documents unawapa feki, watu wanataka document unaleta Konakona...bilionea unashindwa kulipa 100m unaharibu jina lako.

Bilionea wa mchongo huyo!! Anasema alipanda boda boda toka Dar mpaka Wami kukwepa police kumbe alikuwa anakimbia deni!! Kajificha vichakani huko Arusha. Asakanywe popote alipo arudishwe Dar kwa gharama zake. Kafanya mambo ya kingese sana.
 
Hata kama, yeye awaletee magari au awarudishie fedha zao.

Ulimsikiliza vizuri bilionea? Hao jamaa ndani ya week wameghairi kukamilisha malipo na kumtaka jamaa bilionea arudishe fedha wakati yeye kashayaagiza....Kuna watu wana wenge sana wakishika hela yaani ni kubadilikabadilika kama vinyonga...Dawa yao kwenye mkataba ni kuwaandikia kwamba wakighairi fedha hairudishwi.
 
Muhindi wa kwanza
Baada ya Mfanyabiashara maarufu wa Magari Jijini Dar es Salaam, Samweli Shami maarufu kwa jina la Bilionea Shami kudai kuwa ametishiwa maisha na watu aliodai ni vigogo wa Polisi, amejibiwa na waliojitambulisha kuwa ni wahusika aliofanya nao biashara wakimtaka alipe fedha alizopewa na sio kulalamika mitandaoni.

Wasikilize mwenyewe hapa
Habari ya kwanza ni hii > Mfanyabiashara bilionea Dar es Salaam, adai kutishiwa maisha, akimbia kwa pikipiki kutoroka asiuawe hadi Arusha
kupigwa kama ngoma 😂
 
Back
Top Bottom