Hapana hata kidogo Marekani hawa kutawaliwa na Malkia bali walikuwa watawala na walipigana sambamba na mwingireza kuwaondoa wahindi wekundu, hii ilikuwa hatua ya pili baada ya kuichukua nchi..Sisi tuliupata Uhru wetu kutoka kwa wageni waliotutawala tofauti kabisa na wao ambao walikuwa ndio wageni walioitawala nchi hiyo. Kilichotokea tu ni kwamba hawakutaka tena kurudi kwao wala kutambulika kama waingereza bali WATU wa taifa jipya.
Pili, Walipoitangaza nchi yao na kuweka Azimio hilo ndilo lililojenga katiba na sheria, lengo likiwa kuwa guide wananchi ktk sheria na Political culture. Hivyo utunzi wa katiba hii ni technical kama unavyotumia vitabu vya elimu kujielelimisha haina maana unaiga bali unaelimika. Hakuna kitu kuiga ktk ELIMU bali unapanua fikra zako ktk kuitambua dunia iliyokuzunguka na sii wewe na who U are isipokuwa elimu inatuelimisha kwamba kuna watu kama wewe na ktk mazingira tofauti ambayo tutakuja kabiliana nayo. Na unaposema Mfumo mzima wa Elimu ni wa Muingereza hata sikuelewi maana utaanza hata kusema hata nguo tunazovaa ni za muingereza hivyo hakuna kosa kuwa waingereza - Sijui kama hii ndio maana yako!
Hawa viongozi wetu ni watumwa wa akili na pengine athari za utumwa ndio hizi tunazoziona, haikatazwi kuweka malengo ya kufikia kuendesha magari hayo isipokuwa kinachokatazwa ni ULIMBUKENI, Wamarekani wenyewe wanaita WONNA BE.. kwa maana kwamba wonna be are those who act and live like someone else they aren't!. Hawa wanaishi ktk dunia ya kusadikika ndio kina sisi, Lakini haina maana U can't be that person in terms of his/her success. Na hapa ndipo wengi wanaposhindwa kuelewa kwamba WATU hawawezi kubadilika! lakini wanaweza badilisha utawala na mazingira yao - LIBERTY. Kama unakumbuka niliwahi kukwambia kwa mtoto anayewezka azimio la kuwa daktari akikua hana ujinga wa kuiga pindi anapoenda shule kwa malengo ya kufikia azma hiyo, tofauti na wale wanaojiita madaktari ilihali wamepachikwa ujinga fulani - kina fulani. Kwa jinsi tunavyoendesha nchi yetu leo hii ni ulimbukeni mtupu yaani wonna bees kujivika nguo za Michael Jackson ili dunia ituone tunafanana naye..Hii inatokana na kupoteza dira yetu sisi wenyewe..
- Kwani lini huko nyuma Viongozi wetu waliwahi kuwajibika under Azimio la Arusha?
Kuomba omba nje tulianzia kwenye awamu ya kwanza sio leo tu,
Viongozi wabovu tulionao ni tatizo la wananchi tunaowachagua.
mengine tumeyarithi toka wamu ya kwanza hakuna mapya hapa!
. Lakini muhimu ni kwamba hatuwezi kulirudia Azimio la Arusha tena maana limetuletea maafa makubwa sana!
William.
Unaongelea kuomba kwa namna gani? Kweli kama Tanzania under Mwalimu ingekuwa inaomba kwa namna unavyotaka kuniaminisha, Mwalimu angekuwa na guts za kupingana waziwazi na hao "wakubwa"? Mwalimu alitaka kuitoa TZ kwenye Commonwealth kama Uingereza ingekubali Apartheid South Africa kuwa mwanachama. Mifano mingine unaifahamu. Angalia hali ilivyo sasa,taifa halina kauli tena katika anga za kimataifa,kisa kuna "wakubwa" watanuna.?
Niliyasema yanauma sana na nilitaka sana ufahamu hivyo maana sikutegemea kusikia vitu hivi toka kwako hata kidogo..Wewe ni Azimio la Arusha lililokukuza hadi umefikia leo kugombea ubunge leo unaliponda bro, kusema kweli ikifikia mimi kuanza kuropoka vitu vya ajabu kama hivi inabidi unitafute haijalishi niko ktk hai gani maana uzima wa mwili hauna maana yoyote ikiwa naanza kuchanganyikiwa...- Bob wacha haya mambo ya kitoto, kama umeishiwa hoja haina tatizo kukaa pembeni kuliko kukoseana heshima hivi wakati mimi na wewe ni close people, I mean ate the end of the day hii ni siasa yaani kwa sababu wewe hukubaliana hoja na mimi ndio unakuwa umechanganyikiwa nianze kukutafuta?
Vipi bob mbona unashuka sana mkuu? kama huna hoja kwani ni lazima uchangie mkuu?
William.
- Mkuu Jasusi, heshima yako sana America kuna sheria, hakuna miiko ya uongozi you know better huko taifa huongozwa kwa sheria, matatizo ya Clinton na Monica yalitatuliwa na sheria sio miiiko ya uongozi, hapana!
- Kenya wamekwua mabepari kwa muda mrefu kuliko sisi, ndio maana wana viwanda vingi kuliko sisi na pesa yao ni kubwa kuliko yetu, na pia Watalii wanawajali wao kuliko sisi, yaaani haya hata bila shule yanaeleweka sana kuwa ni matunda ya ubepari!
William.
Mkandara,
Unaposema tumepoteza dira yetu. Umepoteza na nani? Je ni dira gani hiyo? Au mwenzetu ni magamba? Au CCM. Azimio la Arusha ni document ya TANU na baadaye CCM.
Mimi sifuati chama chochote cha siasa na kwanini unaniingiza kwenye upotevu wa dira ya chama cha siasa? Au mwenzetu bado hupo kwenye mfumo wa chama kimoja?
Naona sasa hata watu wa CHADEMA, CUF, TLP wanalazimishwa? Unazungumza LIBERTY na unakuwa wa kwanza kuikiuka, typical of tyranny of majority.
Kobello,[SIZE=-1]Adopted July 11, 1958 [/SIZE]
[SIZE=+1]Code of Ethics for U.S. Government Service [/SIZE]
[TD="bgcolor: #cc0000, colspan: 2"][/TD]
Resolved by the House of Representatives {the Senate concurring}, That it is the sense of the Congress that the following Code of Ethics should be adhered to by all Government employees, including officeholders. CODE OF ETHICS FOR GOVERNMENT SERVICE
[Source: U.S. House of Representatives Ethics Committee]
Mkuu wangu kwani Jefferson alipoandika Declaration of Independence hakuwa na chama? Je, walikuwa democratic au labda soma hapa Na Je, mabadiliko yoyote yalibadilisha declaration of Independnce?Mkandara,
Unaposema tumepoteza dira yetu. Umepoteza na nani? Je ni dira gani hiyo? Au mwenzetu ni magamba? Au CCM. Azimio la Arusha ni document ya TANU na baadaye CCM.
Mimi sifuati chama chochote cha siasa na kwanini unaniingiza kwenye upotevu wa dira ya chama cha siasa? Au mwenzetu bado hupo kwenye mfumo wa chama kimoja?
Naona sasa hata watu wa CHADEMA, CUF, TLP wanalazimishwa? Unazungumza LIBERTY na unakuwa wa kwanza kuikiuka, typical of tyranny of majority.
Ukitazama Azimio la Arusha kama ni sera ya TANU/CCM, ina maana unaanzisha mjadala mpya kabisa kwa maana kwamba mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 ulihitaji kwenda sambamba na kitu kipya kabisa nje ya azimio la arusha? Je unataka kutuaminisha kwamba mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 na Azimio la Zanzibar mwaka 1992 did not happen by coincidence? Kwa sababu ni dhahiri kwamba tangia kufutwa kwa azimio la arusha, hakuna sera yoyote ya kitaifa ambayo inatokana na self - determination juu ya wapi tunataka kwenda na tufanye nini kufika huko, kinachoendelea tangia kipindi hicho ni utekelezaji wa sera za soko huria kiholela huku WorldBank, IMF waki determine out future. Inawezekana sijaeleweka vyema lakini ni kutokana na kuchanganywa kidogo na hoja yako inayoashiria Azimio la Arusha should remain as a partisan issue.
- Again sina shida ya kusoma Azimio ambalo nimembishwa kwa nguvu maisha yangu yote ya utotoni hapa bongo, Jefferson Declaration ilikuwa inagusia sana kuondolewa utumwa kumbuka Jefferson alikuwa na fuatilia sana siasa za kukataa utumwa za France ambazo alijua kuwa zipo njiani kwenda US with the fact kwamba mazungumzo ya UN yalikuwepo tayari. Lincoln alipoamua kutekeleza maazimio ya Jefferson, ikatokea a Civil War lakini in the end mawazo ya Jefferson yakashinda utumwa ukaisha,
- Sisi wananchi wakahamishwa kwenye miji yao kwa nguvu kutekeleza maazimio ya Arusha, matokeo wengi wao wakapoteza maisha yao lakini results mpaka leo hakuna!
- Sihitaji u-intelect wa kusoma Azimio maana it was designed kupumbaza na usiulize faida wala hasara zake, ama sivyo unawekwa rumande, kweli ulitegemea mimi niisome hiyo kitu ambayo imetufikisha hapa taifa letu hatujijui tunatoka wapi wala tunakokwenda, pleasee!
William.
Mkuu wangu kwani Jefferson alipoandika Declaration of Independence hakuwa na chama? Je, walikuwa democratic pia labda soma hapa Mbona hata sikuelewi elewi vile, maana tulikuwa na chama kimoja hii haina maana Azimio lile halingeweza kufikiwa kaa tungekuwa na vyama vingine.. Kumbuka tu Azimio litu lililenga kuwabadilisha watun na sio vitu mnachotazama nyie ni kubadilisha vitu ili watu wafaidike na hiyo concept ndio inapingana na Azimio lile. Makosa ya kiutendaji hayawezi kuondoa ukweli wa dhamira ya Azimio la Arusha na hata wewe leo unapinga Technicality tu..lakini bado unaamini vitu vyote vilivyoorodheshwa..
Yesiu wakati anaondoka alikuwa na wafuasi chini ya 20 leo hii tuna waumini zaidi ya billioni nne na hata kama ni asilimia 20 tu ndio wanasali na kufuata mafundisho yake haina maana he failed. Wewe ndiye ulofail kutoweza kuokoka wakati maandishi yapo ya kukuelekeza.
Nakuomba kalisome tena Azimio la Arusha na pengine ksukutua na mawaidha ya mwalimu bofya halafu tutaendelea kutazama wapi tulikosea lakini sintokubali kabisa kwamba malengo ya azimio lile yalikuwa na makosa, unless wewe ni kizazi kipya mlokuta kina Mengi na Lowassa matajiri.
Kobello,
Umefunga mjadala juu ya miiko. Kumbe Marekani wana miiko. Ni mleta mada tu ndiye alikuwa halijui hilo.
Jasusi,
Kama nilivyoeleza mwanzo. Katiba ya nchi haitakiwi kuwa na code of ethics. Kwa sababu zinabadilika badilika. Code of ethics ziwe kwenye sheria za nchi au kanuni za kazi za sehemu husika. Pamoja na hayo bado kuna watu wanaotaka mabadiliko ya kikatiba yajumlishe kanuni za uongozi zilizo kwenye Azimio la Arusha.
Kama zinatakiwa basi zipitishwe bungeni na kujadiliwa kama miswada mingine. Na sio kukurupuka tu. Mwishowe wasukuma watachomoa utamaduni na jadi zao na kutaka ziwe code of ethics.
Niyasema yanauma sana na nilitaka sana ufahamu hivyo maana sikutegemea kusikia vitu hivi toka kwako hata kidogo..Wewe ni Azimio la Arusha lililokukuza hadi umefikia leo kugombea ubunge leo unaliponda bro, kusema kweli ikifikia mimi kuanza kuropoka vitu vya ajabu kama hivi inabidi unitafute haijalishi niko ktk hai gani maana uzima wa mwili hauna maana yoyote ikiwa naanza kuchanganyikiwa... Trust me, unachoandika hata hakieleweki, mara upinge miiko wakati unaitaka sheria, mara sijui mambo ya UN na Jefferson yaani hata sikuelewi elewi vile..Utanisamehe lakini sintokuacha japokuwa hupendi nayoandika.
Hii topic nimeingia nikiwa nimechelewa sana, kwa hiyo itanichukua muda kidogo ku-catch up. Ila siyo kweli kuwa katiba haitakiwi kuwa na code of ethics eti kwa vile zinabadilika kila wakati kwani hata Katiba ina amendments nyingi. Kwa hiyo kubadilika kwa code of ethics kunaweza kuwa reflected kwenye hizo amendments.
Hapana, Jefferson hawezi kupewa sifa zozote kwa juhudi za kuondoa utumwa. Yeye alijikita zaidi kwa maslahi ya wazungu. Kumbuka ni wewe hapa umetufahamisha kwamba alipokuwa anatunga declaration alikuwa na watumwa. Wakati huo weusi hawakuwa full humans kwa macho ya wazungu. Ni kweli aliguswa na kanuni za Ufaransa za liberte et egalite, uhuru na usawa lakini hii haiku apply kwa weusi. Na Lincoln, alipopigana kulinda muungano alikuwa hatekelezi maazimio ya Jefferson. It was simply common sense. The south wanted to break away to continue with slavery na walikuwa na jeshi lao na nchi isingeweza kuendelea kukiwa na confederates na jeshi la taifa ( northerners.) Umerudia tena kuwa kuna wananchi waliopoteza maisha yao katika uhamiaji wa vijijini lakini hujatuambia ni akina nani na wapi. Bila kutoa ushahidi tutakuona kwamba wewe ni muongo na mtu mwenye chuki tu juu ya azimio. Kama azimio limetupumbaza, kwa nini tunalalamikia madudu wanayofanya akina Kikwete na Mkapa? Kwa sababu azimio lilitupa matumaini ya liberte et egalite.
Leo Tanzania egalite hakuna. Kuna tabaka la watawala ambalo naona kila mtu analikimbilia kwa kuwania ubunge ili waweze kuitafuna nchi. Hapana azimio lilitufungua macho na ndiyo sababu tunawapigia kelele wale ambao leo wameua azimio ili waitafune nchi yetu mchana kweupe. Kama wewe hujui unakotoka na unakokwenda, speak for yourself. Sisi wengine tumeshaona the promised land na tumaanini, we will get there.
Je ni wapi kuna ushahidi kwamba wananchi walilazimishwa ujamaa? na kwanini waukatae wakati ule wakati hivyo ndivyo wali ishi kabla ya ujio wa mkoloni? kwani ujamaa simply means undugu/familyhood tofauti na wachache wanavyojaribu kuharibu maana yake halisi. Leo hii kuna mwanachama wa TLP, CHADEMA n.k kweli ambae akieleweshwa maana ya ujamaa atapingana nao?
Hii topic nimeingia nikiwa nimechelewa sana, kwa hiyo itanichukua muda kidogo ku-catch up. Ila siyo kweli kuwa katiba haitakiwi kuwa na code of ethics eti kwa vile zinabadilika kila wakati kwani hata Katiba ina amendments nyingi. Kwa hiyo kubadilika kwa code of ethics kunaweza kuwa reflected kwenye hizo amendments.
Katiba yetu inatakiwa ifuate MISINGI YA AZIMIO LA aRUSHA.Mkuu Kichuguu,
Ni kweli katiba inaweza kuwa na code of ethics, na kufanyiwa amendments. Lakini sifa ya katiba ni kuwa kitabu kifupi chenye kuwezesha watu wote kukielewa haki zao na muundo wa shughuliza za kiserikali.
Sifa nyingine ya katiba ni lazima iwe ni sheria kuu ya nchi. Sheria zingine za nchi zinakuwa extension ya katiba. Hivyo code of ethics unaziweka kwenye sheria ya nchi.
Kwa mfano sheria inaweza kupitishwa kuwa rais anapopiga kampeni ya kuchaguliwa tena asitumie vyombo vya dola kumsaidia. Ukiiweka kwenye vifungu vya sheria za nchi, hakutakuwa na haja ya kufanya amendment yoyote hile.
Vilevile katiba ni lazima iwe neutral document kwa kiasi kikubwa. Unaporuhusu kila kitu kiwe kwenye katiba, utaruhusu tyranny of majority kama inavyotokea Tanzania. CCM wana wabunge wengi na wana rais. Hivyo wanaweza kubadilisha vitu kukidhi mahitaji yao.