AZIM DEWJI: UHABA WA UMEME UNATOKANA NA MAENDELEO YA WANANCHI
Mfanyabiashara mkubwa nchini Mzee Azim Dewji ameongea na waandishi wa habari leo Januari 13, 2023 na kueleza kuwa amefanya utafiti mdogo na kugundua moja ya sababu zinazopelekea uhaba wa umeme nchini ni kuongezeka kwa mahitaji (matumizi ya umeme) kunakotokana na maendeleo ya wananchi
Mzee Azim Dewji ameeleza kuwa kwa kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Samia mahitaji na matumizi ya umeme yameongezeka maradufu kwani ndani ya kipindi hicho vituo vya mafuta zaidi ya elfu 10 vimefunguliwa nchini, pasi laki 8 zimeingia nchini, oven laki 7 na elfu 50, Friji na Friza karibu laki 6 na 60 na TV laki 6, vyote hivi vinaongeza matumizi ya umeme.
Kwa upande mwingine Dewji amesema sababu nyingine zinazopelekea uhaba wa umeme ni baadhi ya mikoa kuunganishwa kwenye Gridi ya Taifa ndani ya kipindi cha Rais Samia, viwanda vingi vipya kufunguliwa, hotel nyingi kujengwa, nyumba mpya kati ya laki 6 na laki 7 zimejengwa nchini, Kila Hospitali ya Mkoa kuwa na mashine kubwa za X Ray, CT Scan na MRI na kadhalika
Sambamba na hayo Mzee Azim Dewji ameipongeza Serikali ya Rais Samia kwa kukamilisha sehemu kubwa ya mradi wa Umeme wa Bwawa la Mwalimu Nyerere kwani utasaidia kupunguza uhaba wa umeme kwa kiasi kikubwa