Azim Dewji: Lissu amuombe radhi Biteko; Matamshi wanayotoa wapinzani hayapaswi kuumiza watu wengine

Pfizer

JF-Expert Member
Mar 25, 2021
304
518
Mfanyabiashara maarufu nchini Mzee Azim Dewji amezungumza na vyombo vya habari kuhusu tukio la maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kukataa kupisha msafara wa Naibu Waziri Mkuu, Mhe. Dotto Biteko aliyekuwa jijini Mbeya kikazi, Februari 20, 2023

"Mimi ni mshabiki wa vyama vya upinzani na kila mara huwa nasema Simba haiwezi kuwa imara bila kuwa na Yanga imara, hivyohivyo CCM inahitaji wapinzani imara ili kuwa imara zaidi, lakini saa nyingine wapinzani wanajisahau wanazungumza maneno ya kuleta fujo" - Alisema Mzee Azim Dewji

Mzee Azim Dewji amesisitiza ni muhimu wapinzani kuwa wastaarabu, wakikosa ustaarabu Serikali ikazuia maandamano wasipige kelele

Hata hivyo, Mzee Azim Dewji amesema kuwa Lissu ni Mnyaturu mwenzake na wote wametokea Singida, lakini kwenye hili ni vizuri akaomba radhi.
 
Mimi ni Ofisa wa Serikali mstaafu na si shabiki wa chama cho chote wala Simba au Yanga. Nashangaa ofisa gani Mwandamizi wa Serikali anaweza kumpitisha Kiongozi ye yote wa kitaifa katikati ya halaiki ya maandamano ambayo ni rasmi, achilia mbali ya kiongozi mwenyewe kuafiki huo utaratibu. Ni aibu tupu kwa Tanzania kuwa hatuko chini katika viwango vya elimu tu lakini hata katika viwango vya utawala na uongozi!! Jambo hilo si la kutetewa hata kidogo. Rais mwenyewe anatakiwa alikemee jaribio hilo kwa sababu misiba inayoweza kuzuiliwa kabla ya kutokea mchezo huo ukienda kombo!
 
View attachment 2913636
Mfanyabiashara maarufu nchini Mzee Azim Dewji amezungumza na vyombo vya habari kuhusu tukio la maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kukataa kupisha msafara wa Naibu Waziri Mkuu, Mhe. Dotto Biteko aliyekuwa jijini Mbeya kikazi, Februari 20, 2023

"Mimi ni mshabiki wa vyama vya upinzani na kila mara huwa nasema Simba haiwezi kuwa imara bila kuwa na Yanga imara, hivyohivyo CCM inahitaji wapinzani imara ili kuwa imara zaidi, lakini saa nyingine wapinzani wanajisahau wanazungumza maneno ya kuleta fujo" - Alisema Mzee Azim Dewji

Mzee Azim Dewji amesisitiza ni muhimu wapinzani kuwa wastaarabu, wakikosa ustaarabu Serikali ikazuia maandamano wasipige kelele

Hata hivyo, Mzee Azim Dewji amesema kuwa Lissu ni Mnyaturu mwenzake na wote wametokea Singida, lakini kwenye hili ni vizuri akaomba radhi.
Kwani aliyekuta mwenzake ni nani, waandamanaji walikabidhiwa barabara na polisi, polisi walitakiwa wamuelekeze Biteko kutumia njia nyingine na si vinginevyo, hivyo Biteko awaombe msamaha Chadema kwa kuyavamia maandamano yao.
 
Nilichokielewa kikubwa kabisa ni...

Kama mh Tundu lisu siku awe kiongozi, angependa kuitwa majina ya hovyo kama anavyowaita viongozi wengine, Je angependa tumdharau kama anavyoonyesha kuwadharau viongozi wengine?

Dewj kaongea point
 
View attachment 2913636
Mfanyabiashara maarufu nchini Mzee Azim Dewji amezungumza na vyombo vya habari kuhusu tukio la maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kukataa kupisha msafara wa Naibu Waziri Mkuu, Mhe. Dotto Biteko aliyekuwa jijini Mbeya kikazi, Februari 20, 2023

"Mimi ni mshabiki wa vyama vya upinzani na kila mara huwa nasema Simba haiwezi kuwa imara bila kuwa na Yanga imara, hivyohivyo CCM inahitaji wapinzani imara ili kuwa imara zaidi, lakini saa nyingine wapinzani wanajisahau wanazungumza maneno ya kuleta fujo" - Alisema Mzee Azim Dewji

Mzee Azim Dewji amesisitiza ni muhimu wapinzani kuwa wastaarabu, wakikosa ustaarabu Serikali ikazuia maandamano wasipige kelele

Hata hivyo, Mzee Azim Dewji amesema kuwa Lissu ni Mnyaturu mwenzake na wote wametokea Singida, lakini kwenye hili ni vizuri akaomba radhi.
Kila tukio liliratibiwa kutokana na muda uliopangwa ili lifanyike. Muda wa maandamano ulipangwa vyema na ulifahamika kwa jeshi la polisi pamoja na waandamanaji, lakini msafara wa NWM haukuwa kwenye ratiba inayofahamika.

Huwezi kuja na "an ad hoc timetable amid of the prior known and ongoing official timetable". Waliogonganisha haya matukio mawili walikuwa na nia ovu ili kuikomoa CDM ili ipambane na vyombo vya dola.
 
Mfanyabiashara maarufu nchini Mzee Azim Dewji amezungumza na vyombo vya habari kuhusu tukio la maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kukataa kupisha msafara wa Naibu Waziri Mkuu, Mhe. Dotto Biteko aliyekuwa jijini Mbeya kikazi, Februari 20, 2023

"Mimi ni mshabiki wa vyama vya upinzani na kila mara huwa nasema Simba haiwezi kuwa imara bila kuwa na Yanga imara, hivyohivyo CCM inahitaji wapinzani imara ili kuwa imara zaidi, lakini saa nyingine wapinzani wanajisahau wanazungumza maneno ya kuleta fujo" - Alisema Mzee Azim Dewji

Mzee Azim Dewji amesisitiza ni muhimu wapinzani kuwa wastaarabu, wakikosa ustaarabu Serikali ikazuia maandamano wasipige kelele

Hata hivyo, Mzee Azim Dewji amesema kuwa Lissu ni Mnyaturu mwenzake na wote wametokea Singida, lakini kwenye hili ni vizuri akaomba radhi.
asubiri shombo la mipasho ya kisiasa Dewej🐒

wanyaturu hawakosolewagi hadharani ata kama amekosea kweli 🐒
 
Anawashwawashwa sana huyu, itakuwa wametega dish penyewe awamu hii, chaneli za upigaji zanashika bila chenga.

Ikitokea mtu yeyote anasema mambo yanayohatarisha kutikisa dish basi mzee anatoka na kutoa kauli.
 
Back
Top Bottom