kuna kitu kilicho nyuma ya pazia ambacho watu hawajakielewa. Tatizo mamlaka zetu zimeingia mikataba ya ajabu kabisa na multichoice inayofanya kisimbuzi pekee kinachoanzishwa nchini kikiwa na michuano ya ulaya ya soka kuwa ni dstv pekee, ambayo ndio hasa kwenye wateja wengi.
Kama unafuatilia mechi yoyote ya ulaya (isipokuwa ya fainali) inayooneshwa ss3 haiwezi kuoneshwa live na atn wenye leseni ya kuonesha mechi moja kwa wiki, au dtv nao wenye leseni ya kuonesha mechi moja ya ligi ya mabingwa ulaya.
Hivyo visimbuzi vingine vinavyoweza kuonesha mechi nyingi (au zote) za michuano ya ulaya huingizwa nchini kiaina aina tu, lakini kwa visimbuzi vinavyoanzishwa nchini ni lazima viwe na mechi chache sana kubwa au zikose kabisa kutokana na mamlaka zetu kuingia makubaliano hayo na multichoice.
kuna rafiki yangu mmoja anayefanya biashara zake norway alitaka kuleta nchini mradi mkubwa wa visimbuzi vyenye channel zote za sky sports,hukuvisimbuzi vyake vikiwa vya kipekee vya mtindo wa kuhamishika kirahisi, lakiniakawekewa ngumu na mamlaka zetu kuhusu haki za kuonesha mechi za ulaya kuwa ya multichoice, akaamua kufuta mradi wenyewe na anaendelea na mambo yake huko norway.mwanzoni nilihisi bakhressa angeweza kuvuka hiki kizuizi kutokana na uwezo wake mkubwa wa ushawishi lakini naye kakwama palepale, ila yeye amefanikiwa kupata haki ya kurusha ligi kuu ya tanzania bara, ambayo hutaweza kuiona live kokote bila kisimbuzi chao, na habari njema ni kwamba wameshamalizana na yanga.