Kabla hujanunua Azam TV pitia hapa; Usije kujuta

kidadari

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
8,647
9,595
Ni matumaini yangu kuwa wengi ni buheri wa afya na manaendelea vema na majukumu ya kila siku!

Ukweli kuwa wengi wetu tuna mategemeo makubwa kutoka Azam tv tofauti na ukweli ulivyo...

Lengo la Uzi huu si kuharibu biashara ya Azam Bali kueleza uma ukweli halisi wa mambo!

So nitaelezea mambo muhimu ya kuyafahamu kabla ya kununua Azam TV.

1. Bei ya decoder hubadilika wakat wowote bila taarifa! mwezi wa 1,2016 nimenunua 140,000 hadi sasa tar 7 Marc imefika 170,000.

2. Channel ya kawaida tuu kama BBC, Fox, CNN, AL-Jazeera, France 24, mpaka ulipe 20,000 kwa mwezi.

3. Sinema zetu utapata bongo movie za 2005 kushuka chini Mara nyingine movie hurudiwa kwa week Mara 3, No latest movie ujue hivyo!

4. Organization ya channel iko hovyo! Unaweza kulipwa kifurushi cha 12,000 lakini kupata channel moja hadi nyingine ni shughuli! Channel za kihindi tu ndo ziko pamoja!

5. Tegemea kupata channel kibao za kiarabu na nyingine zisizoeleweka ni lugha gani!

6. King'amuzi kikiharibka jiandae kununua kingine.... hakitngenezeki

7. Ukienda kununua watakuambia vipeperushi vya list za channel na bei ya vifurushi vimeisha maana wanajua ukiangalia channel zao na bei utaghairi kununua" maana haviendani!

............ ......
22 Oct 2018
UPDATES
8.Azam wamefanya mabadiliko ambayo wameongeza gharma ya tsh 3,000 kwa kila kifurushi hivyo kufanya kifurushi cha bei ya CHINI KABISA kuwa 15,000 ambacho ni Sports.

>kimsingi gharama hizi ni kwa ajili ya channel moja tuu ya Azam sports ambayo huonyesha La Liga kwa kuwa channel za Man u, Liverpool na Madrid hazionyeshi mech live zaidi ya marudio na kutangaza Club zao
Thanks..

.......................
UPDATES
Azam wameongeza bei tena ambapo kifurushi kitakuwa 18,000 badala ya 15 000 ambapo wameongeza channel 1 ya azam Sport 2. Ikumbukwe mechi kubwa kama Yanga Simba na Azam Zitaonyeshw hapa so lazima ulipe 18,000 badala ya 15,000
.....TV 1 wameitoa
.................
UPDATES
local channel zilizilobaki ni TBC na channle za Azam tuu kutokana na mgogoro wa kisheria.Kama mpenzi wa vipindi vya nyumbani kama taarifa ya habari imekula kwako labda TBC tuu mechi za mpira wa bongo na Sinema zetu
Bei za vifurushi ziko pale pale licha ya local channel kutolewa!! Hakuna updates yotote kutoka Azam juu ya mabadiliko haya!
 
Azam wamelewa sifa

chanel e wameondoa tu bila kujali wateja wake

za kihindi ndo wamejaza kuliko za aina zingine
ajabu unazipata hata kama huzilipii..

mpira hata chan tu au cecafa hakuna
kuna ndondo cup tu na vodacom...

azam washajifanya 'wamefanikiwa'
 
Kwani CNN siku hizi iko Azam?? Kifurushi gani??
Kama nikipata CNN, BBC, AL JAZEERA, DOSCOVERY CHANEL, NAT GEO na ZILE za muziki nafikiri itanitosha zaidi! NITALIPIA.
Siku hizi silipii kifurushi chochote.
Za kibongo na CCTV zote, RT, CHANEL FRANCE 24 English ktk other chanels zinanitosha sana! Nikilipiaga kifurushi naonaga kama wananiibia, huwa siinjoi kivile, hakukuwa na cnn.
 
Nimatumaini yangu kuwa wengi ni buheri wa afya na manaendelea vema na majukumu ya kila siku! .....Ukweli kuwa wengi wetu tuna mategemeo makubwa kutoka Azam tv tofauti na ukweli ulivyo...Lengo la Uzi huu si kuharibu biashara ya Azam Bali kueleza uma ukweli halisi wa mambo! so nitaelezea mambo muhimu ya kuyafahamu kabla ya kununua Azam TV.
1. Bei ya decoder hubadilika wakat wowote bila taarifa! mwezi wa 1,2016 nimenunua 140,000 hadi sasa tar 7 Marc imefika 170,000.
2. Channel ya kawaida tuu kama bbc,fox ,CNN ,aljezeera, France 24, mpaka ulipe 20,000 kwa mwezi.
3.sinema zetu utapata bongo movie za 2005 kushuka chini Mara nyingine movie hurudiwa kwa week Mara 3, No latest movie ujue hivyo!
3.organization ya channel iko hovyo! unaweza kulipwa kifurushi cha 12,000 lakini kupata channel moja hadi nyingine ni shughuli! channel za kihundi tuu ndo ziko pamoja!.
4.Tegemea kupata channel kibao za kiarabu na nyingine zisizoeleweka ni lugha gani!
5. Wapenzi wa channel "e" mujue kuwa haipo Azam TV!
Mkuu kunasiku nilibeba pesa kabisa kununua, asee baada ya kufika kwa muuzaji, wakara akanipigia hesabu ikafika 230000, na hicho ni kifurushi cha 12000, asee nlirudi na kuendelea na king'amzi changu cha startimes, maana nliona ni uhalooo mtupu, bei zao zinabadilika kama kinyonga, tena ukienda umevaa tai hata laki3, wanakugonga,

Kibaya zaidi hao wauzaji, asee wanampozi balaa, nlimkuta dada mmoja pale kimara mwisho kama unaenda sokon duh, ni shidaaaa, ila walekebishe bei na vifurushi, kisha hao wauzaji wafundishwe kuongea na wateja..

Halafu bei ya kufunga hlo dishi et 30000, jaman huu ndo ujasiliamali,? Halafu nikamwambia basi niuzie nnafundi wangu, akaniambia kikiharibika hawatahusika, mpaka leo sitaki kuwasikia azam, mpra ntaangalia ukumbini, newz itv na startive
 
af nasikia usipolipia wanakata hadi channel za ndani aisee wakat mi startimes mwaka sasa sijalipia na kula channels za ndani mpk rahaa

Kweli mkuu wanakata mpaka upige simu customers care ndo wakufungulie! so ndugu zetu wasio na taarifa wanalazimika kilipia wakati local channel ni bure
 
Back
Top Bottom