Azam Pesa: Huduma mpya ya kifedha

Mkisema Azam Pesa makato yatakuwa less than what is charged by competitors then it would make alot of sense by now!
 
Kampuni kubwa na iliyoenea katika nchi ya Tanzania pamoja na nchi jirani 'Bakhresa Group' imeleta sokoni huduma mpya ya kifedha ijulikanayo kama 'Azam Pesa'.

Huduma hii ni kama zilivyo huduma nyinginezo za M-Pesa, Airtel Money, Tigo Pesa and the like.

Ili kuielewa zaidi huduma hii, nitaenda katika mtindo wa Maswali na kisha majibu.

Je, Azam wameanzisha mtandao wao wa simu?
Hapana. Azam bado hawajaanzisha mtandao wao kama zilivyo kampuni kadhaa za mawasiliano hapa nchini.

Bali AzamPesa wameingia makubaliano na baadhi ya mitandao kwa ajili ya kuwezesha upatikanaji wa huduma kupitia line za mitandao hiyo.

Mpaka sasa AzamPesa wameshakubaliana na Tigo, Airtel na Zantel. Hivyo huduma hii inapatikana katika line za mitandao tajwa.

Vodacom, Halotel na mitandao mingine bado wapo kwenye mazungumzo. Watakapokubaliana basi huduma hii itawezeshwa katika line hizo.

Je, huduma hi inahusika
na nini?
Kama ilivyo huduma zingine, huduma hii inahusika na;
1.Kutuma Pesa
2.Kutoa Pesa
3.Kulipia bili
4.Kulipia bidhaa za Azam

Je, huduma hii imeanza kufanya kazi?
Ndiyo, huduma hii imeshaanza kufanya kazi kwa wateja wote waliosajiliwa.

Je, najiungaje na huduma hii?
Fika katika duka la wakala na uweze kusajiliwa. Kinachohitajika ni namba yako ya simu pamoja na namba yako ya NIDA. Ndani ya dakika mbili tayari utakuwa umeshasajiliwa kuwa mteja wa AzamPesa.

Je, huduma naweza kupata vifurushi 'bundles' maalum vya Azam?
Hapana. Kama ambavyo nilijwishaeleza hapo juu kwamba Azam bado hawajaanzisha mtandao wao hivyo swala la vifurushi linabakia kuwa maamuzi ya mtandao husika.

Je, huduma hii naipata wapi?
Huduma hii inapatikana katika mikoa yote Tanzania. Ijapokuwa bado haijatapakaa kila mahali lakini upatikanaji wake katika maeneo mengi ya miji ni uhakika.

Je, menu 'ussd' ya AzamPesa ni ngapi?
Baada ya kusajiliwa, utabadili namba ya siri. Hivyo utabonyeza *150*08# na kuweza kupata huduma ya AzamPesa.

Kama una swali lolote kuhusiana na huduma za AzamPesa, basi karibu.

Wasalaam.
sawaaaaaaaaa
 
Gharama za kutuma na kutoa pesa ni chini kulinganisha huduma nyinginezo za kifedha

Gharama za kutuma na kupokea zipo chini na nafuu kuliko huduma zingine

Nimekuwekea mchanganuo Wa gharama za makato kwenye mtandao Wa Tigo. Naomba uniwekee gharama za Azam pesa ili nilinganishe..
tarif3.jpg
 
Inawezekana vp wewe unafanya biashara ya kuuza madawa, halafu anakuja mtu anakupatia dawa umuuzie zinazofanana na zako Tena kwa Bei ya chini...
Haiwezekani Azam awe na huduma ya fedha kwenye mtandao halafu akatumia mitandao mingine yenye biashara hyo hyo...
 
Nashukuru leo kwa kupata Usajili wa AZAM PESA....bado code number tuuu
 
Ili kuwa wakala wa AzamPesa, fika katika kibanda cha kusajili wateja wa kawaida wa AzamPesa.

Muombe akuelekeze kwa Wakala Mkuu wa AzamPesa. Ukifika, atakusajili kwanza kama mteja wa kawaida. Kisha atakupa form ya kujaza ukiambatanisha na vifuatavyo:
1. TIN NUMBER
2. LESENI YA BIASHARA
3.KITAMBULISHO CHA NIDA.

Ukishajaza na kusaini kukubaliana na vigezo na masharti, utamuachia Wakala Mkuu.

Naye atazikusanya na kuscan, zitatumwa kwetu. Tutakuandalia TILL number pamoja na vifaa vinginevyo.

Kisha, kumfikishia wakala Mkuu ambaye naye atakupigia simu ukafate documents zako tayari kama Wakala wa kawaida wa AzamPesa.

Karibu.
Hi inauza umeme na kulipia bills za maji?
Inatoa risiti Kama ilivyo kwa maxmalipo?
 
Naomba majibu haya kwa watu wa azampesa
1.tunaomba schedule ya makato???
2.je inawezekana kuhamisha pesa kwenda mtandao mwingine mfano tigo pesa au airtel money???
3. Je unaweza kuhamisha pesa kutoka azampesa kwenda bank gharama n shs ngapi???
4. Je mna lipa kwa azampesa???
5.je kwenye azampesa kuna tozo???
6. Je kiwango cha kuweka na kutoa mwisho n shs ngap????
 
Back
Top Bottom