AZAM na Baraka Mpenja punguzeni mahaba kwa Yanga, kuweni professionals

SAYVILLE

JF-Expert Member
Mar 25, 2010
5,129
7,898
Jana nilipokuwa nafuatilia gemu ya Yanga, nilikuwa nasikia mahaba ya kupitiliza kwa timu ya Yanga kutoka kwa mtangazaji Baraka Mpenja na hii siyo mara ya kwanza kuliona hili.

Jana alikuwa anatoa kauli kama "upande wa pili nao watakuwa wakienda chooni wanasema Yanga kweli anapiga mpira mwingi" na kauli aliyokuwa anairudia mara nyingi ni "huu ni mpira wa kitabuni, siyo mpira wa papatu papatu". Ulikuwa unawalenga kina nani kwa kauli hizo?

Viongozi wa Simba nao waamke, hali iliyokuwepo msimu uliopita ya kuishi kinyonge haitaifikisha hii timu popote. Karibia media zote sasa hivi ziko kwenye payroll ili kuichafua Simba. Mnaweza kuyaona haya mambo ni madogo ila media ina nguvu sana inaweza kuupamba uongo hadi ukaonekana kweli.

Azam kiujumla ni kama wamekuwa na bifu na Simba ndiyo maana wanasimba wengi wanafurahi mnapofanya vibaya. Uwanjani mnaikamia Simba halafu Yanga wanajipigia wanavyotaka.

Mechi zinazochezwa uwanja wa Uhuru hawafanyi coverage nzuri, Camera ya muhimu inawekwa chini na muda wote unaona kwanza mabenchi na nguzo kabla haujawaona wachezaji waliopo uwanjani. Mechi za mikoani hawaweki camera za kuonyesha offside, matokeo yake minong'ono kuwa Simba inabebwa na marefa inakuwa na nguvu bila ushahidi wa kutosha. Inabidi wawepo watu ndani ya Simba kuhakikisha mechi zake hasa zile za nyumbani zinatangazwa ipasavyo.

Kwa ujinga huu ndiyo maana wengine ikifika makundi tu ya CAF tunaswitch DSTV. Watangazaji wa nje wanatoa facts siyo mahaba binafsi na pia hawatangazi mpira kama wako redioni.

Nimemaliza.
 
Jana nilipokuwa nafuatilia gemu ya Yanga, nilikuwa nasikia mahaba ya kupitiliza kwa timu ya Yanga kutoka kwa mtangazaji Baraka Mpenja na hii siyo mara ya kwanza kuliona hili...
Dalili ya mvua ni mawingu, kulia lia kumeanza asubuhi na mapema 🤔,sijui itakuwaje pale ligi ikishika kasi,na wakati huo kule kimataifa,🦁 kashanyolewa mkia🤸🤸🤸🤸
 
Jana nilipokuwa nafuatilia gemu ya Yanga, nilikuwa nasikia mahaba ya kupitiliza kwa timu ya Yanga kutoka kwa mtangazaji Baraka Mpenja na hii siyo mara ya kwanza kuliona hili...
Duuh..!! nimejitahidi kusoma andiko lote lakini nikagundua mwandishi anamsongo wa mawazo coz anajaribu kusema majina yote mazuri aliyoyatoa Baraka Mpenja kwa wachezaji wa SIMBA SC pamoja na kuwapa wachezaji morali na mileage pamoja popularity nchini mfano mzuri MWAMBA WA LUSAKA, PUTIN, MK14, SHOW ME THE WAY THE LEFT FOOTER MAGICIAN

Pira BIRIANI na mengine mengi kumbe Alikuwa analipwa na SIMBA afanye yote hayo, harafu unataka kutumbia akina Saleh Jembe, bin Kazumari, Jef Lea, pamoja na wenzao wote wanalipwa na SIMBA?

Kinachotakiwa Viongozi wasajili vzr, walete walimu wazuri na timu icheze mpira mzuri pamoja na matokeo mazuri hivyo ndivyo vitu mashabiki wanataka.

#Poor thinking.
 
Wapi nimesema hivyo? Watangaze na waonyeshe mpira kwa weledi. Mechi za uwanja wa Uhuru mpira hautazamiki huwa tunajizalimisha tu
Uliposema watangazaji wapo kwemye payroll ya Yanga, ulitaka na Simba wafanye hivyo.
Ndio maana nikakuambia kesho utakuja utasema pia na waamuzi wanalipwa na Yanga
 
Back
Top Bottom