AZAM mnapoteza kuwa na Balozi kama Manara. Hajui Ethics za Biashara

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
36,870
2,000
Nimeshangazwa sana na aina hii ya tangazo la biashara ya vifurushi vya king'amuzi chenu kutoka kwa munayemuita balozi wa AZAM.

Unatangazaje bidhaa ya Azam kama vile bidhaa hiyo ni mali ya Yanga hivyo unaiponda Simba? Huwezi kuwajulisha watu wanunue kifurushi hicho huku unawakebehi Simba na kuwaita Makolo wakati nao ni miongoni mwa watumiaji.

Hivi mpenzi wa Simba atajisikia vyema kununua bidhaa za Azam kwa kebehi hizo za Manara anazo changanya katika biashara ya Azam?

Huko ni kuyokujua ABC za kibiashara, Manara amekosa Ethics za kazi yake nadhani kwa vile hana elimu na kwa kampuni kubwa kama AZAM hiyo ni miscalculation ya hali ya juu sana.
Screenshot_20210923-134112_Instagram.jpg
 

joseph1989

JF-Expert Member
May 4, 2014
8,049
2,000
Leo mnaumia, kwa zamani alivyokuwa akiiponda Yanga mbona mlikaa kimya, mmemlea wenyewe huyo ,kwenye page yake Yanga alikuwa anaita Utopolo, vumilia tu ndugu yangu kama mashabiki wa Yanga walivyokuwa wakivumilia wakiitwa Utopolo na bado walikuwa wakilipia na kununua ving'amuzi na uwanjani wanaenda kwa wingi.
 

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
36,870
2,000
Leo mnaumia, kwa zamani alivyokuwa akiiponda Yanga mbona mlikaa kimya, mmemlea wenyewe huyo ,kwenye page yake Yanga alikuwa anaita Utopolo, vumilia tu ndugu yangu kama mashabiki wa Yanga walivyokuwa wakivumilia wakiitwa Utopolo na bado walikuwa wakilipia na kununua ving'amuzi na uwanjani wanaenda kwa wingi.
Tatizo ni uelewa wenu ndio shida. Hapo tunazungumzia biashara ya Azam inahusianaje na utani na kebehi za Simba na Yanga?
Wanaoelewa ethics za biashara wanaelewa nazungumzia nini.
 

made

JF-Expert Member
Jun 29, 2010
820
1,000
Weee Kolo leo ndio unaona hizo ethics?tulia dawa iwaingie na ndio mjue malipo hapahapa....Yanga likuwa 8nawauma hivyohivyo kwa muda wote aliokuwa kwenu Makolokolo Fc.
 

joseph1989

JF-Expert Member
May 4, 2014
8,049
2,000
Tatizo ni uelewa wenu ndio shida. Hapo tunazungumzia biashara ya Azam inahusianaje na utani na kebehi za Simba na Yanga?
Wanaoelewa ethics za biashara wanaelewa nazungumzia nini.
Kipindi alipokuwa akitukana Yanga, hakuwa balozi wa Azam?

Maswala ya biashara ya Azam Bakheresa anayajua kuliko wewe na anayajua tokea Manara alipokuwa akiitukana Yanga na hajawahi kumtoa ukiona hivyo Bakheresa anaijua faida ya Manara kuwa balozi wa Azam.

We vumilia mwenye biashara yake kishamkubali kama balazi wabidhaa zake za Azam.
 

idawa

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
24,354
2,000
Hilo neno halina shida kama vile neno Utopolo. Lakini kuna haja ya kuliingiza hapo kwenye biashara ya mtu mwingine?
Utani wa Simba na Yanga iweje uathiri biashara ya mwingine?
Azam ndio anajua mkataba alioingia na Manara, yaye ndio anajua faida na hasara ya anachofanya Manara.
 

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
36,870
2,000
Azam ndio anajua mkataba alioingia na Manara, yaye ndio anajua faida na hasara ya anachofanya Manara.
Nakushangaa hata wewe umeshindwa kuelewa mantiki ya hoja.
Hapa sio suala la ubaya wa utani au kebehi, bali ni utani na kebehi kwa kundi fulani kwa bidhaa isiyo wahusu (kama wazalishaji) Simba au Yanga.
Ni kweli mwenye kujua biashara hiyo itaathirikaje ni wenyewe Azam, lakini tabia hii hakuwa nayo zamani ya kutumia bidhaa anazotangaza kama balozi kukashifia wengine!
Mfano hajawahi kutumia ASAS MILK kutukania Yanga! Maana watumiaji wa maziwa hayo wapo wanayanga pia!
Jee sasa anaweza kutangaza maziwa ya ASAS na kusema "kunyweni maziwa ya ASAS ili mjenge afya msiwe kama Makolokolo wa Msimbazi?"
Utani wa Simba na Yanga haufi lakini huwezi kuziingiza kampuni zingine kwenye kejeli wakati pande zote zina wateja wake. That's what I mean.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom