Haji Manara: Mo alitaka niwe balozi wa bidhaa zake badala ya Azam. Asema Mo anadai hapati faida ilhali jezi za Simba zimejaa matangazo yake

Joseverest

JF-Expert Member
Sep 25, 2013
51,985
69,376
Aliyewahi kuwa Msemaji wa Klabu Kongwe ya Simba Sports Club leo hii anazungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam juu ya Masuala mbalimbali ikiwemo ya yeye kuondoshwa katika klabu ya Simba

Kuwa nami hapa kwa updates/kinachoendelea


--------------------------------------------
Ameanza kwa kuwasalimu wanahabari...
Anawaomba radhi wanahabari wote wakati anatekeleza majukumu yake, anasema kuwa yeye ni binadamu anakosea...


Anaendelea kusema...nanukuu

HAJI MANARA: Yanga kama watani zangu. Kuna wakati kweli nilizidisha utani. IM SORRY. Lengo langu lilikuwa kuongeza hamasa kwenye mpira. Mashabiki wengi wa Yanga waliokuwa wakinizodoa mitandaoni ndio waliokuwa wananiomba 'Selfie' uwanjani. Mpira sio Uadui, sina chuki na Yanga."

=▷Vitu vilivyoniondoa Simba, moja ni Biashara na la pili ni Umaarufu. Sijui lini niliwahi kutamka mimi ni Mkubwa kuliko Simba. Wakati naanza kazi Simba niliambiwa nijitolee malipo yangefata baadae. Nilikubali huku nikijua aliyekuwepo kabla yangu alikuwa analipwa."

=▷ Msemaji niliyekuwa nafanya promo za mechi nilikuwa sikatiwi tiketi ya safari. Kote mlikokuwa mnaniona nilikuwa najitegemea kwa hela yangu mfukoni. Nilijitolea wakati wa shida, Neema ilipokuja Nikaonekana sifai

=▷ Senzo alipofika tu aliniambia moja ya jukumu alilopewa na mabosi ni kunifukuza kazi. Nikamuuliza kwanini? Akasema hakuna sababu, wanataka tu uondoke.

=▷ Mo alitaka nipewe mkataba niwe balozi wa bidhaa zake ili niache wa AZAM. Alimwambia Babra anipe mkataba lakini Babra alikaa miezi 6 bila kunipa. Alikuwa akipokea simu yangu anajibu tu 'I will call you back" halafu Anakata

=▷ Mo Dewji aliwahi kunipigia simu akaniambia watu wanasema nimekuwa maarufu kuliko yeye hivyo anataka kunitoa Simba

=▷ Babra alimpigia simu Diamond na kumwambia mtu pekee anayetakiwa kutajwa kwenye wimbo wa Simba ni MO peke yake. Diamond alikataa akawaambia njooni mchukue hela yenu, msinipangie kazi

=▷ Mo Dewji anasema hapati faida lakini mkiangalia jezi ya Simba ina matangazo mpaka ya Mo Foundation. Jezi imechafuka matangazo ya Mo kama timu za Sudan halafu mtu anasema hapati Faida.

=▷ Haji Manara amesema yeye ndiye aliyeanzisha kundi la Simba HQ ambalo lengo lake lilikua kuchangia pesa za bonasi za Wachezaji kipindi hicho Simba iko na hali mbaya.

=▷ Kundi hilo sasa ni kubwa sana linauwezo wa kuchanga zaidi ya Tsh milioni 30 kila mchezo wa Simba lakini leo hawataji kama ni hazina yake.

Pia kundi hilo hilo ndilo viongozi wa Simba wamesema amejiuzulu kupitia kundi hilo.

=> Mwezi wa kwanza mwaka huu (2021) tarehe 5 na mkataba ninao, Simba kupitia CEO Babra wamesaini na Azam mkataba utakaoisha msimu wa 2022/2023 wa Tsh milioni 385 kwa mwaka, Kashembe aliisema mahali lakini labda mlikuwa hamjaielewa vizuri. - Haji Manara.

CEO Babra toka ameingia ameishafukuza Wafanyakazi viongozi tisa mimi ni wa kumi. - Haji Manara.

=> Hatupo hapa bila Azam Tv, leo mpira umechangamka ligi ya Tanzania kwasababu ya Azam TV. Nilirudi wakati niko simba na narudia wakati sipo Simba.

=> Haji anasema mkataba ambao Hans Pope aliuzungumzia wa milioni nne ulikuja baada ya Mo Dewji kuomba Haji ampelekee mkataba wake wa kibiashara na kampuni ya Azam na hapo akiwa tayari ameitumikia klabu kwa miaka sita bila kuwa na mkataba.

=> Kwenye mkataba huo wa Azam ambao aliupeleka ulikuwa na kipengele kinachotaka kiasi cha shilingi milioni mia tatu hamsini kulipwa ili mkataba uvunjwe, Haji anasema sharti hilo ndilo lililopelekea Simba Sc kumuandalia mkataba ambao haukufikia kiasi cha shilingi milioni nne ukiwa na sharti la kutomtaka kufanya biashara na kampuni nyingine yoyote sipokuwa Mohamed Enterprises.

=> Simba tusikubali kudanganywa,bilion 21 tulizoambiwa zimetumika ni deni"

"Chuki yake kwa Azam ndiyo asili ya kunitengenezea mimi mtego wa kuihujumu timu" Manara.

"Nimeweka akiba mengine ninayo mengi kwasababu najua watatuma watu"
"Ipo siku haki ya Simba itarejea,
huwezi kuwaongopea watu siku zote ,utawaongopea katika kipindi kifupi tuu" MANARA

Anaendelea kufunguka

MANARA: MIAKA 6 BILA MKATABA

Haji Manara amesema mara nyingi uongozi wa Simba SC haukuwa ukimsafirisha kwenda kwenye michezo ndani na nje ya nchi, hivyo ilimbidi kujigharamia. Amesema kwa miaka sita amefanya kazi bila mkataba na posho, lakini alifanya sababu anaipenda Simba. Kuna kipindi alikuwa akilazwa kwenye makochi anakumbushia mechi ya Mbabane Swaziland

=▷Zile promotion zote nilizokuwa nazifanya Sijawahi kupata posho wala bonus yoyote kutoka Simba, na mara baada ya kusema haya najua watanitengenezea risiti feki nasema haya hili mjue kile kilichotokea Simba kiliniumiza kiasi gani? - Haji Manara

≒▷Senzo alipoingia akaniita ofisini akaniambia moja ya kazi yangu ya kwanza ni kukuondoa wewe ofisini lakini mimi nimewakatalia kwa sababu sijawahi kufanya kazi na wewe na alifanya kazi na mimi miezi miwili akaona msaada wangu

Senzo alifanyiwa figusi baadae uvumilivu ukamshinda Yanga wakampa ofa nzuri akaondoka na kiukweli niliumia sana nikaona nimeshaisha na nikalia sana- Haji Manara


“Waliniita ofisini nikaenda wakaniambia jana ulionekana umeenda kigamboni Kwa Ghalibu kutuhujumu, walinionyesha simu inayoonyesha kuwa nilikuwa Kigamboni lakini nilipoangalia tarehe ilinionyesha ilikuwa tarehe 7 muone jinsi hawa watu walivyokuwa wananichukia,” -Haji manara
 
Manara kama Manara
Jibi%20la%20CEO%20BABRA%20kwa%20Manara%20Ni%20_I%20WILL%20CALL%20YOU%20BACK_%20_grinning_%20(%...jpg
DUH%20..%20Bosi%20alimaindi%20Manara%20kuwa%20Maarufu%20kuliko%20yeye.._bow_%20(%20484%20X%206...jpg
Neno%20moja%20kwa%20DIAMOND%20PLATINUMZ%20_grinning_%20(%20642%20X%20640%20).jpg
 
Manara totally mswahili +mzaramo kuna haja gani ya kuongea yote haya, yaani leo ndio kaharibu reputation yake yote na ile sifa yake ya kujitamba eti ana UWELEDI mkubwa leo kajishusha mpaka chekechea.

Haya watani pamabaneni na SEMAJI LENU aka Buggati,mpaka hapo kawavua nguo kwamba timu yenu ina kuna tatizo la management kwani mambo aliyo yasema ni kweli sababu yy alikuwa jikoni.
 
Msimlaumu haji mambo mengi aliyosema ni kweli kabisaaa hasa masuala ya mkataba wa Azam, kimsingi anamaindi kutolewa lakini usemaji huohuo ndio umempa ulaji sehemu nyingine , jamaa anajiuza japo hana elimu usanii wake na utoto wake wa mjini umemsaidia sana, leo kawavua nguo hadharani, yaani Bilionea anaona wivu muuza maneno tu anakuwa juu kuliko yeye wakati hana pesa Hahahaaaaa Tanzania nchi nzuri sana
 
Huyu Haji na waliomtuma ni hovyo sana, na kajichanganya sana.

Kashashindwa. Simba sct msimjibu. Mwacheni abwabwaje mpaka aridhike na roho yake. Hana Nia njema na Simba na anaombea ipate mabalaa. Eti anaongea na mashabiki!

Azam nao kumbe ovyo sana kumtuma huyo ili kutangaza TV yao ndo nn sasa. Simba achaneni na Azam, ukimsoma vizuri manara kila mara Azam tv ndo waliomtuma kutukana live!

Serikali kwa nn mtu huyu atukane muwekezaji tena live kabisa?
 
Msimlaumu haji mambo mengi aliyosema ni kweli kabisaaa hasa masuala ya mkataba wa Azam, kimsingi anamaindi kutolewa lakini usemaji huohuo ndio umempa ulaji sehemu nyingine , jamaa anajiuza japo hana elimu usanii wake na utoto wake wa mjini umemsaidia sana, leo kawavua nguo hadharani, yaani Bilionea anaona wivu muuza maneno tu anakuwa juu kuliko yeye wakati hana pesa Hahahaaaaa Tanzania nchi nzuri sana
Mkuu wahindi ni wabinafsi sana wanaroho ya korosho. Haji angekuwa muhindi angekuwa analipwa mil 15.

Muhindi analipa mshahara ya kikatili sana kwa ngozi nyeusi.
 
Awekwe ndani tu, Simba mmeshindwa kumtafutia kosa huyu mwamba
,
Kwanza ni muongo ,halikuwa wapi siku zote kwa nini , hakunuka mapema, ? Anasubiri mpaka wamfukuze ndo anuke , dust
 
Back
Top Bottom