Azam huu nao ni ubaguzi

Azam huu nao ni ubaguzi

basi Kama ndo hivyo,AZAM itaifishwe mara moja maana hii ni hujuma na pia ni moneylaundry kabisa
 
ila mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, kila siku tulikuwa tuna aminishwa wafanyakazi karibia woote wa wa azam media ni ma ustaadhi tuu, kumbe na sisi tumo pia ndani ya azam media, huu msiba ndiyo umenifungua macho!, na inawezekana kabisa sisi akina john na catherine ndiyo wadini zaidi yao………………!
Unachoongea ni Kweli kabisa
 
Sasa wanakishambulia kituo cha azam kisa mwenye kituo muislam
afute!!!..udini unamsumbua,maana cha kukosoa hana,walidai azam inaajiri kidini,lakini katika marehemu..wengi ni wa dini isiyo ya azam
 
Azam wamekosea sana, warekebishe hilo kosa haraka sana kwani uwezo wa kufanya hivyo wanao tena mkubwa tu.

Habarini wakuu...?

Poleni wafiwa wote kwanza

Mie nimeliona hili toka jana azam mnavyotangaza kufiwa na staff wenzenu

1. Kwanza mnatangaza sana watu watano badala ya 7, hata kama wale wawili sio staff wenu lakini mkumbuke ndio walikua wamewabeba staff wenu.

2. Mmefata miili ya staff watano tu, yan mmeshindwa hata kusaidia hiyo miili miwili ya wenzetu...

Mkumbuke lakini hata hao madereva ukute walikua wateja wenu kwa namna moja, lakini ninyi mmejiangalia kama ninyi tu kwenye shida.

Mungu mkubwa kupitia clouds fm nimewasikia madereva wa coaster wa biafra na external nao wamesema wanajipanga kusafirisha miili ya wenzao hao pia wizara ya utalii imesema itawasaidia....

NOTE
Azam kumbukeni hata msiba wa lucky Vicente serikali haikubagua kwamba huyu ni dereva alisababisha ajali au hawa ni wanafunzi na walimu, bali ilitoa heshima ya maziko kwa wote.View attachment 1149596
 
Waafrika tumelogwa na aliyetuloga alikufa kitambo hivi ata ungekuwa na roho ya shetani unaweza fanya jambo kama ilo? Kwamba ufike eneo last ajari ubebe mili ya wafanyakazi wako tu nyingine uiache hapo? Think twice bro ilo aliwezekani mnawabebesha watu lawama za bule kabisa.
Jambo ninalojiuliza kwanini siku zote baseless blaming zinaelekezwa Azam ??
 
Hivi mna uhakika na povu mnalotoa au ndio kumaliza stress?
Hao madereva na konda wake wana ajira yao na taratibu zao za kazi
La muhimu ni kua Azam wamezika wafanyakazi wao kwa heshima.zote kila.marehemu kulingana na imani yake
 
Kwani hao wa5 wote waislamu? Mbona naona Silvanus hapo, ni jina la kikristo hilo.
 
Na madereva wamesafirishwa pamoja na wafanyakazi wa Azam.

Labda kwa kuwa matangazo yao yanawataja wafanykazi hao watano ukahisi hao madereva wamewaacha.

Nipo karibu na familia ya dereva mmoja aliyefariki. Maiti imesafirishwa na Azam na imefika jana kwa njia ya ndege.
Tusipende kulaumu bila ya uthibitisho
Uthibitisho wako ni upi sasa au kuwa karibu, azam wamesema wamesafirisha miili 5 au wewe ndio ulikua rubani
 
Kama mind zetu ndio hizi zimejaa udini,sizani kama tutakuwa na vision kwa ajili ya maendeleo ya taifa letu.
 
Mkuu Nimepitia Pitia Comment Za Wajuzi Wa Mambo Hapo Juu Nimegundua Kuwa Katika Kusafirisha Miili Ya Marehemu Hakuna Ubaguzi Uliotokea Maana Wajuzi Wa Mambo Wanasema Miili Ilikuwa Saba Kunako Ndege Iliyosafirisha Miili Hiyo!!!!......Ila Mimi Nilipoumia Na Nlipoona Ubaguzi Ulipotokea Ni Jinsi Azam Wanavyotangaza Vifo Vya Staff Wao Watano Tu Na Huyo Dereva Na Msaidizi Wake Wanawekwa Kando Tafikiri Hata Wakitangazwa Watapata Kiki Kupitia Media Yao Ilihali Watu Wenyewe Washajipumzikia Zao Na Matatizo Ya Hapa Duniani Na Hakuna Faida Yoyote Watakayopata Marehemu Hao Wawili Hata Hao Watano Wao
 
Mkuu Nimepitia Pitia Comment Za Wajuzi Wa Mambo Hapo Juu Nimegundua Kuwa Katika Kusafirisha Miili Ya Marehemu Hakuna Ubaguzi Uliotokea Maana Wajuzi Wa Mambo Wanasema Miili Ilikuwa Saba Kunako Ndege Iliyosafirisha Miili Hiyo!!!!......Ila Mimi Nilipoumia Na Nlipoona Ubaguzi Ulipotokea Ni Jinsi Azam Wanavyotangaza Vifo Vya Staff Wao Watano Tu Na Huyo Dereva Na Msaidizi Wake Wanawekwa Kando Tafikiri Hata Wakitangazwa Watapata Kiki Kupitia Media Yao Ilihali Watu Wenyewe Washajipumzikia Zao Na Matatizo Ya Hapa Duniani Na Hakuna Faida Yoyote Watakayopata Marehemu Hao Wawili Hata Hao Watano Wao
Mkuu ukweli ni kwamba miili iliyokuja ni mitano,hiyo miwili imefatwa na kosta nyingine ya tajiri.

Kosta inapaki mabibo sio biafra au ubungo external
 
Back
Top Bottom