Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 71,279
- 105,481
Nimesikitishwa sana na msiba uliotokea kwa ajali ya gari Julai 8 2019 iliyochukua maisha ya wafanyakazi wa Azam watano na madereva wawili huko Shelui Singida, wakielekea Chato kikazi.
Inasikitisha zaidi kwa kuwa marehemu walikuwa vijana wadogo wanaoanza kujipatia umahiri kazini na kujenga familia zao na taifa. Nimeona, kwa mujibu wa maombolezo yaliyorushwa na Azam TV mitandaoni, kama nakumbuka vizuri, vijana wote wamezaliwa miaka ya 1980s, mmoja kazaliwa 1980 na wengine 1989 nafikiri. Kwa hiyo wengi wamefariki na miaka takriban 30, ambayo kwa mategemeo ya kuishi (life expectancy) ya dunia ya leo ni midogo sana. Nchi kama Japan watu wamefikisha mategemeo ya kuishi takriban miaka 84.
Kuna mengi ya kuwekea mkazo, habari za usalama barabarani ni moja naliona la muhimu. Wenyewe kuheshimu thamani ya maisha na kukemeana tunapoona thamani hii inashushwa ni jambo lingine.
Lakini pia, mengine hayaepukiki. Sasa haya nayo tumejipanga vipi? Kutakuwa na ajali zinazotokea kazini, watu watafariki kutokana na ajali hizi, hata tukiwa waangalifu vipi. Sasa tunajipanga vipi kusaidiana ikiwa hilo litatokea?
Nimesikia Azam imetoa rambirambi za shilingi milioni moja kwa mfanyakazi mmoja kupitia matangazo ya mtandaoni. Kwanza nataka kuishukuru Azam kwa kuweza kutusitiri kufanikisha mazishi.Bila shaka kuna gharama nyingi zimetumika kusafirisha miili na kufanya logistics nyingine mpaka mazishi yakafanikiwa
Ila, kiasi hiki cha shilingi milioni moja kwa dunia ya leo kilinipa maswali sana.
Tukumbuke wengine hawa walikuwa baba wa familia changa, kuna mmoja ana mtoto wa miezi michache na kafunga ndoa mwaka huu tu. Wwengine wanategemewa na "extended family" kama ilivyo kawaida sehemu nyingi kwetu. Rambirambi ni pole tu, kwa hivyo haina kiwango, ila, kiwango kikiwa kikubwa kinaweza kusaidia zaidi.
Swali hili lilinipeleka kwenye kufikiria Life Insurance sehemu za kazi. Kwa Tanzania jambo hili linaangaliwa vipi?
Ikiwa waajiri wengi watakata Life Insurance policy kwa waajiriwa wao, hata ile basic tu, na kulipia kiasi kidogo tu kwa mwezi, inawezekana kabisa wafanyakazi wanaofariki kazini wakapata kuwachia ndugu zao wa karibu Life Insurance benefit zilizo nzuri zaidi.
Marekani kwa mfano, ni jambo la kawaida kwa muajiriwa kukatiwa life insurance inayolingana na mshahara wake wa mwaka mzima automatically anapoajiriwa. Kwa kuwa waajiri wengi wanakata insurannce hii, na wafanyakazi wanaofariki kazini ni wachache, basi malipo ya mwezi anayolipa muajiri yanakuwa madogo sana, na muajiriwa akifariki anahakikishiwa kwamba ndugu zake aliowachagua wanalipwa mshahara wake mwaka mzima.
Kitu kama hiki hakipo/hakiwezi kufanyika Tanzania?
Nimewaangalia wale kinamama na watoto walioachwa nikawaonea huruma sana, wamepata msiba wa kuondokewa na waume zao, na hapo hapo wana msiba wa kuyakabili maisha ya kiuchumi upya.
Tujadiliane tafadhalini.