ibanezafrica
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,261
- 6,556
Kwenu Waandishi Wa Habari. Toka jana tunaomboleza vifo vya ndugu zetu waliopoteza maisha huko mkoani Singida,lakini ka hitilafu kadogo ni vema kangerekebishwa pale ambapo panatangazwa marehemu watano tu wakati waliopoteza maisha ni saba,kwanini wale wawili hawawi covered?
Nasikitika hata majina yao sijayasikia tangu msiba huu ulipotokea... Tunawaomba waandishi rekebisheni hili.
Ikumbukwe wote waliokuwemo ndani Ya ile coaster tayari walikua timu moja yenye lengo moja la kufanikisha shughuli iliyolengwa, ila kwa mapenzi yake mola hawakuweza kutimiza lakini wote mule ndani ya gari walikua kazini wakienda kutekeleza jambo la kitaifa
Hivyo Dereva na Msaidizi wake nao wanastahili kutangazwa, kujulikana, kupewa pole hata rambirambi au msaada wowote maana hatujui hata uwezo wa family zao na jambo hili ni zito na humfika kila mja
Hivyo kwenu waandishi liangalieni Hili, hatujui hata misiba yao ipo wapi pia mazishi yao, pia tujulishwe maendeleo Ya Majeruhi.
Mungu aziweke roho za marehemu wote saba mahala pema peponi na awape nafuu majeruhi wapone haraka.