Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 16,303
- 33,758
Mkuu.
Viongozi wetu wengi wa Afrika ni 10% type.
Pili wengi wanabaki madarakani kwa wizi wa kura.
Tatu, wanapopata hiyo 10% wanaificha katika mabenki ya mataifa ya West na kwa hiyo siri zao zinajuulika vyema na serikali za nchi hizo. Ndio sababu huwa rahisi kurubuniwa.
Nne, Bajeti za nchi nyingi ingawa zina utajiri wa rasilimali za asili lakini zinategemea ufadhili na misaada ya West na US.
Last but not least, wameingiwa na woga, wasiwasi na kiwewe. Hawajijui wala hawajitambui wanaogopa hii njia mpya ya Maandamano ya kudai haki katika nchi, pia hawajui nani atakuwa target baada ya Gaddaffi.
sisi wengine tunafurahia ,tunacheka kwa kuletewa demokrasi na west na US. Wengine tunaposema hawa West na US hawana kawaida ya kutetea maslahi ya wananchi wa nchi wanazozilenga ni mbinu tu ya kupandikiza "watumishi wao". Ukisema hivi unaambiwa unamsapoti Gaddaffi.
kwa vile wengi wa wanachi tuko usingizini basi kwa nguvu za kijeshi walizonazo hawa waharibifu wa dunia, wanarudi tena kwa aina mpya kujigawia Afrika na mataifa ya dunia ya tatu vile wapendavyo....tukae mkao wa kuliwa.
AU haina 'credibility' mbele ya jumuiya ya kimataifa. Hii si OAU ya kina Nasar, Nkrumah, Nyerere, Kaunda, Sellaise, Tolbert n.k.
Waziri Membe aliulizwa AU wanafanya nini kuhusu Libya (BBC swahili) wiki nne baada ya mapambano, jibu lake ni kuwa wanaunda tume kwenda kuchunguza mgogoro! Sasa siku tano zilizopita nchi za magharibi zikaamua kupiga, eti ndio ujumbe wa AU ulikuwa unakwenda Libya. Walikaa kimya kwasababu bwana mkubwa na mfadhili alikuwa anaelekea Benghaz.
Lakini pia tujiulize, somalia walisema ni tatizo la Afrika na linahitaji Africa solution, nini kinaendelea kule kama si mauji ya Al shabaab na AU.
Wametaka Ivory coast, nini kinaendelea kama si ubabaishaji. Kama humuwezi Bagbo utamwezaje Ghadaffi japo kumkemea.
Kwa ufupi AU ni felia kubwa sana, na haina maana katika medani za kimataifa.
Tatizo langu na Ghadaffi ni pale alipoifanya nchi kama familia yake, ubabe dhidi ya raia wake.
Malikia Elizabeth amekaa miaka zaidi 40 kama 'ceremonial figure' na serikali zimebadilika zaidi ya mara 10. Demokrasi ya UK haifanani na Ghadaffi hata moja ya kumi.
Tukumbuke watu wanaopigana ni Walibya na wanakufa na wapo tayari kufa kumuondoa Ghadaffi. Ni waislam na wanataka kumuondoa mwislam Ghadaffi. Hii dhana ya hujuma zidi ya uislam inatoka wapi. Mtu akisema Oil interest tunaweza kumsikiliza la udini ni kutojua.
Ghadaffi amesaidia sana AU, vikundi vya ukombozi kama ANC na vya waasi kama Afrika magharibi, misikiti n.k. Ametumia hela ya mafuta kujenga umaarufu. Haya yote hayahalalishi udhalimu wa kuwapiga mabomu kwa ndege raia wake wala kufuta maovu ya kuwaficha wapinzani wake daima milele kusikojulikana. Tukianza kumkubali kwa hisani zake, sioni kwanini Sadaka za majambazi walioua kwa uporaji zikataliwe misikitini au makanisani.