Atheist wengi hawajui wanachokitafuta

Atheist wengi hawajui wanachokitafuta

na huwezi kumhukumu mtu aliyepata ujumbe ambao ulijua kabisa kua hajauelewa na uwezo wa kumfanya aelewe unao. Mungu mjuzi wa yote na mwenye uwezo wote hatakiwi kutoa mafundisho, mungu akikupa mafundisho anapaswa kujua mfumo mzima wa ubongo wako bila hata kukupa mtihani.
Kwanini mimi niuelewe wewe usiuelewe?

Kama mungu akijua kua umeelewa katika mafundisho aliyokuatia je atakupa mtihani ili akupime kuangalia kama umeelewa???
Ndio, atakupa mtihani, na huo mtihani sio kwa ajili yake kujua kama wewe umeelewa au la, ni kwa ajili yako kujitambua na kujipima, yeye hana shida na sisi ila sisi ndio tuna shida na yeye.

Kama mungu akijua kua hujaelewa, je atakupa mtihani ili aweze kujua kua hujaelewa???
Ndio atakupa mtihani, ili wewe mwenyeo utambue kuwa umeelewa au hujaelewa, yeye hana shida ya kujua kama umeelewa au la, wewe ndie unaetakiwa kujua.

Vile vile mungu kama ni muweza wa yote kwanini ashindwe kukufanya ujue kila jambo analolitaka bila kukupima na mitihani ambayo hata baada ya kugundua kua hujaelewa hakuwezeshi ili nawe uweze kuelewa????
Mungu muweza wa yote, hufanya lile alitakalo na sio ulitakalo wewe. Hapo ndio mnafeli, yeye ameamua kila mtu awe na ujuzi wake. Hoja mfu kabisa. Angelifanya wote tuwe na ufahamu mmoja basi bado ungekuja kuhoji kwanini ametupa ufahamu mmoja.

uislam unauwezo wa kuniepusha zinaa bila kunifundisha namna ya kuepuka??? Kama hauna uwezo basi hata kukosea kwangu sitaulaumu kwasababu una imperfection, ila kama unao uwezo wa kunifanya niepuka bila kufundishwa basi ni ujinga kuendelea kunifundisha kitu ambacho kinaweza kuniepushia.

uislam kwanini usifanye mambo automaticaly bila kumfundisha mtu kama ilivyo mmen'genyo wa chakula unavyo fanyika tumboni bila kufundishwa???
Uelewavyo wewe, uislam ni nini kwani?

nijiepushe kivipi na mabaya wakati mungu tayari alishaona kua ntayakwaaa??? Kwaiyo mungu akijua kua nitafanya mabaya mimi naweza nikaepuka nikafanya mazuri???
Jiepusha kwa sababu hujui maono ya Mungu. Hujui mungu ameona vipi kama utafanya mema au mabaya. ungelikuwa unajua basi ingekuwa hamna maana, lakini the whole point ni kwamba wewe hujui anachokijua, ndio maana unatakiwa ustrive for the best.

Wakati huo baba yake sio mjuzi wa yote na muweza wa yote ni kweli nitamuadhibu maana hayakua mategemeo yangu kumuona mtoto wangu anafeli wakati nilimfundisha na itakua hukumu ya haki kwake.

Lakini kwa mungu mwenye sifa ya ujuzi wote na uwezo wote hapaswi kutoa mtihani wala kuadhibu mtu kwasababu hajaelewa wakati uwezo wa kumfanya aelewe bila mtihani anao
Adhabu ameziweka siku ya mwisho kwa watu kama nyie mnaompinga Mungu kwa sababu zilizokosa kichwa na miguu. Siku hio ikifika ndio mtapat uthibitisho mliokuwa mkiutafuta lakini itakuwa too late tena.

Adhabu ya mungu kwa watu wake ni moto kwaiyo hii adhabu utaifananisha na adhabu ya huyo mtoto aliyopewa na baba yake?? Yani mzazi kamzidi mungu huruma mzazi ndio kama mungu halafu mungu ndio kama shetani sasa
Hakuna kiumbe chochote ambacho kinaweza kumzidi huruma Allah. Na ndio maana Allah anakusamehe kwa kosa lolote utakalofanya ikiwa utatubia kabla siku yako ya kufa, tena unapotubu, anafuta dhambi hio kabisa, siku ya Akhera, hujikukumbushwa kama ulifanya kosa flani. Leo hii tunaona Msanii Diamon, mpaka leo anamchukia baba yake hata kama mzee ameomba msamaha, sasa unataka kufananisha na huruma za Mungu? Kuna kiumbe gani hasa chenye huruma zaid ya Allah aliemuumba? Na je Kuna kiumbe gani chenye kuadhibu kuliko Allah?

Atheist leo unaamini uwepo wa mashetani? 😀 😀 😀

kwa kusema tu inawezekana mzee alikua na uhakika umekua umefanya assumption ambayo sio uhalisia na kufanya mfano wako uwe mfu tena
Mfano haujawa mfu, kwa sababu ni kitu ambacho kipo na kinawezekana sana tu. Watu kuikewa mitego ipo sana tu.

Kuna muumini mwenzako alisema mungu akiwa na sifa hii ya ujuzi wote halafu akakuadhibu kwa kile alichokiona kua utafanya halafu wewe ukawa huna namna ya kukikwepa basi huyu mungu ni snitch.

Mimi nasema sio snitch kwasababu hayupo angekuwepo kusingekua na dhana ya kusema anatoa mitihani wala uhuru wa kuchagua halafu katika kitu alichokiona huwezi kuchagua tofauti na alivyoona
Huyo sio muumin, labda muumin wa atheism 😀

Hapa narudi pale pale, Mungu anajua khatma yako, wewe unajua khatma yako? UTAJUAJE KUWA YEYE ALIONA WEWE UTAINGIA MOTONI? Hebu naomba unijibu hili angalau.

Inamaana huelewi kua mungu alikwishajua kua sitaelewa mafundisho yake mpaka unauliza hili swali? Hujui kila kitu kinachofanyika hakifanyiki kwa bahati mbaya??
Hujajibu swali, kwanini mimi nielewe uwepo wake wewe ushindwe kuelewa? Au umechagua tu kutoamini uwepo wake kwa sababu humuoni? 😀

Kwanini yeye mwenye uwezo wote ambao angeweza kuutumia uwezo huo kunifanya namimi nielewe kama wewe, ameshindwa kunifanya nielewe?? kiasi kwamba hata wewe umeona umuhimu wa mimi kuelewa hayo mafundisho je inamaana huyu mungu ajaona umuhimu wa mimi kuelewa hayo mafundisho???
Mungu angekufanya uelewe, ile dhana ya uhuru yote ingefutika. Hata mimi Allah hajanifanya nimuelewe, ila amenipa akili ya kuchambua mambo na kujitafutia elimu. Hata mimi Allah hajanipeleka msikitini ila amenipa miguu niitumie kwenda uko.
Ujumbe ukishamfikia huyo mtu allah anakua hajui kua huyo mtu hajaelewa?? Akijua kua hajaelewa kwanini hakumfanya aweze kuelewa zaidi inamaana allah hana uwezo wa kumfanya mtu akaelewa nje ya adhabu???
Ubongo wako umepewa uufanyie nini? utafute pesa tu na ulewe?
 
Mkuu muundaji wa gari tuseme Ferrari linalokimbia kilomita labda 500 akisema alijua gari hilo lingekimbia umbali huo lakini akasema hakulitengeneza likimbie hivyo ataonekana punguani kama siyo muongo.
Hawezi kuwa punguani, jaribu kutolea mfano mwengine, nahisi kwenye magari hujui kitu. Waundaji wa magari wanaweza kujua kuwa engine za gari zinatoa power fulani lakini wanatengeza zisiwe na hio nguvu.

By the way unaweza kufafanua mfano wako unalingana vipi na Mungu mjuzi wa yote?
 
Kwanini mimi niuelewe wewe usiuelewe?
Nikisema sijaelewa kwasababu sijapewa uwezo wa kuelewa utasemaje???

Mungu wako alijua kua mimi sitaelewa na yeye ndiye mwenye uwezo wote anaweza kufanya kila kitu nisichokiweza kikawezekana sasa kwanini hakuniwezesha ili nami nijue kama wewe???

Ndio, atakupa mtihani, na huo mtihani sio kwa ajili yake kujua kama wewe umeelewa au la, ni kwa ajili yako kujitambua na kujipima, yeye hana shida na sisi ila sisi ndio tuna shida na yeye.

Inamaana huyu mungu hajui kua mimi najitambua au lah na ndio maana ananipa mtihani?

Kwanini watu wahitaji mtihani
Inamaana mungu alishindwa kunipa uwezo wakujua vitu automatically bila mtihani? Kwanini mungu hakuwaumba watu waweze kujitambua bila mtihani wakati?

Kama mungu aliwapa watu mitihani ili wajitambue, inamaana hakujua kua kunawatu hata akiwapa mitihani hawatajitambua??

Inamaana mitihani ndio njia pekee yakumuwezesha mtu ajitambue hakuna mbadala wake???
 
Nikisema sijaelewa kwasababu sijapewa uwezo wa kuelewa utasemaje???
Unajuaje kama hujapewa uwezo wa kuelewa?

Mungu wako alijua kua mimi sitaelewa na yeye ndiye mwenye uwezo wote anaweza kufanya kila kitu nisichokiweza kikawezekana sasa kwanini hakuniwezesha ili nami nijue kama wewe???
Unajuaje kama Mungu amejua kama hujaelewa? kama amejua kuwa umeelewa ila hutaki je?

Inamaana huyu mungu hajui kua mimi najitambua au lah na ndio maana ananipa mtihani?
Hujajaaliwa kuelewa jibu? Nimekwambia kuwa Mitihani ni kwa ajili yako na sio yeye. rudia ulichoquote.

Kwanini watu wahitaji mtihani
Inamaana mungu alishindwa kunipa uwezo wakujua vitu automatically bila mtihani? Kwanini mungu hakuwaumba watu waweze kujitambua bila mtihani wakati?

Kama mungu aliwapa watu mitihani ili wajitambue, inamaana hakujua kua kunawatu hata akiwapa mitihani hawatajitambua??

Inamaana mitihani ndio njia pekee yakumuwezesha mtu ajitambue hakuna mbadala wake???
Allah anafanya lile litakalo
 
Kwanini mimi niuelewe wewe usiuelewe?

Ndio atakupa mtihani, ili wewe mwenyeo utambue kuwa umeelewa au hujaelewa, yeye hana shida ya kujua kama umeelewa au la, wewe ndie unaetakiwa kujua.

Kama Lengo la mtihani ni kunijuza halafu mungu alijua kua akinipa mtihani sitaweza kujua, kwanini atoe hukumu kwa kosa ambalo lipo nje ya uwezo wangu ambalo sikuwa na uwezo wa kuliepuka???

Mungu muweza wa yote, hufanya lile alitakalo na sio ulitakalo wewe. Hapo ndio mnafeli, yeye ameamua kila mtu awe na ujuzi wake. Hoja mfu kabisa. Angelifanya wote tuwe na ufahamu mmoja basi bado ungekuja kuhoji kwanini ametupa ufahamu mmoja.
Kama mungu kaamua kila mtu awe na ujuzi wake aliopangiwa na watu wametofautiana katika huo ujuzi, inakuaje tena atoe hukumu kwa watu ambao wana ujuzi mdogo kwa kutoelewa mafunzo yake wakati yeye ndiye aliyewapa ujuzi huo mdogo usioweza kuelewa vitu vikubwa???

Uelewavyo wewe, uislam ni nini kwani?
taasisi tu ya upigaji

Jiepusha kwa sababu hujui maono ya Mungu.
Kutokujua maono ya mungu sio kigezo cha kutojua sifa ya mungu kua yeye ni mpangaji wa maisha ya binadamu

na hakuna jambo linalotokea kwa bahati mbaya everything is part of his plans. Kujiepusha au kutokujiepusha hakubadili kitu

Hujui mungu ameona vipi kama utafanya mema au mabaya.
najua kua mungu ameona vipi kwasababu kila kitachotokea tayali alikwishakiona sasa kusema kua hujui mungu ameona vipi inamaana hujui kua unapinga kua mungu si mjuzi wa yote aliyajua maisha yako yote kabla hujazaliwa???

ungelikuwa unajua basi ingekuwa hamna maana, lakini the whole point ni kwamba wewe hujui anachokijua, ndio maana unatakiwa ustrive for the best.
na mungu angekuja hajui, concept ya kumuadhibu mtu ingekua na maana kwasababu tutasema tu hakujua kua tutakosea.

Lakini hata kama aliweza kujua, ila hakua na uwezo wa kurekebisha alichokijua pia hatutamlaumu akituadhibu tutasema tu alitamani tusifanye mabaya aliyoyaona kabla hayajatokea ila hakuwa na uwezo wa kutuepusha nayo.

Lakini tumeambiwa mungu ni muweza wa yote na mjuzi wa yote sasa kwanini ahukumu? Kuna maana yoyote juu ya hili?

Adhabu ameziweka siku ya mwisho kwa watu kama nyie mnaompinga Mungu kwa sababu zilizokosa kichwa na miguu. Siku hio ikifika ndio mtapat uthibitisho mliokuwa mkiutafuta lakini itakuwa too late tena.
Adhabu hizo nazijumlisha kama myths kwasababu hakuna maana yeyote mungu kutoa adhabu kwa viumbe wake katika dhambi alizozijua kua zitafanywa na hakuwapa nafasi ya kuwaepusha.

Ushawahi jiuliza mungu anafaidika nini kukuchoma moto na atapata hasara gani endapo akikuacha bila kukuchoma moto??

Hakuna kiumbe chochote ambacho kinaweza kumzidi huruma Allah.
Na hakuna kiumbe ambacho kikatili kumzidi allah, Kila kiumbe ambacho kikatili ni lazima kitauliwa au kilishauliwa na allah.

yaani anajua utafanya kosa halafu uwezo wa kukuepusha usifanye hilo kosa analo halafu anakuacha ufanye hata kama dhambi hiyo unayoifanya ni kuua mwingine asiye na hatia allah hakuepushi nayo. Halafu ukifanya hiyo dhambi allah anakasirikau na anakuadhibu kwa dhambi ya kuua mtu asiye na hatia

Kwa sifa hii huyu si mungu mwenye upendo wote

Na ndio maana Allah anakusamehe kwa kosa lolote

angekua anasamehe kwa kosa lolote basi kusingekua na habari za moto, moto upo kwasababu allah hawezi kusamehe kosa lolote.

utakalofanya ikiwa utatubia kabla siku yako ya kufa, tena unapotubu, anafuta dhambi hio kabisa, siku ya Akhera, hujikukumbushwa kama ulifanya kosa flani.
Mungu angeumba ulimwengu usioruhusu dhambi kutubu wala misamaha isingekuwepo

Kuna jambo lolote linaweza kutokea bila mungu kuliruhusu litokee?? Bilashaka hakuna, na kazi ya mola si haina makosa?? sasa kwa uwepo wa dhambi unataka kumlaumu mungu kua alibugi kuruhusu dhambi iwezekanike kuwepo??

Kama mungu karuhusu dhambi iwepo ili wewe na mimi tuweze kuifanya basi kutofanya dhambi ni dhambi kubwa sana, kwasababu mungu amekuumbia dhambi ili uitumie halafu wewe unaikwepa

Kama hakuna kitu kinachotokea kwa bahati mbaya
mungu akishaona kua kuna dhambi itakayo nikabili mbele halafu yeye akaiacha bila kuizuia nisiifanye wakati alikua na uwezo wa kuiepusha mbali na mimi, mimi kufanya dhambi hiyo si dhambi hapo mwenye dhambi ni mungu kwasababu karuhusu dhambi itendeke wakati aliweza kuizuia isitendeke

Leo hii tunaona Msanii Diamon, mpaka leo anamchukia baba yake hata kama mzee ameomba msamaha, sasa unataka kufananisha na huruma za Mungu?
kwasababu diamond hana upendo wote vilevile ana madhaifu yake na pengine kawa deluded na maneno ya mama yake so it is hard to stop holding a grudge against his father

Kwaiyo mungu mwenye upendo wote hawezi kua mnafiki kukuhukumu kwa kigezo cha kusema kua hakujua na hawezi kukuhukumu kwa kigezo cha kusema hakuwa na uwezo wa kukuepusha usifanye dhambi.

Kuna kiumbe gani hasa chenye huruma zaid ya Allah aliemuumba? Na je Kuna kiumbe gani chenye kuadhibu kuliko Allah?

Chenye kuhukumu hukumu za kikatili hadi kwa watoto wasiojua lolote hakiwezi kua na huruma. Kusema mungu anahuruma alafu ni mkatili unafanya mungu huyu asieleweke kama sigara kali

Atheist leo unaamini uwepo wa mashetani? 😀 😀 😀
najadiliana kwa kuchukua upande wako unaosimamia ili tuweze kuelewana na ndio maana hakuna sehemu nimekuambia uthibitishe mungu yupo kwasababu najua tu hayupo na huwezi kuthibitisha

Mfano haujawa mfu, kwa sababu ni kitu ambacho kipo na kinawezekana sana tu. Watu kuikewa mitego ipo sana tu.
unabahatisha?

Huyo sio muumin, labda muumin wa atheism 😀
hii ni juu yako

Hapa narudi pale pale, Mungu anajua khatma yako, wewe unajua khatma yako?

ukijua kua mungu alijua hatma yako yote kabla hata hujazaliwa hivyo huna haja ya kujisumbua kujua kwasababu kila kitu ni mipango yake na hakuna jambo utakalolifanya liwe geni kwake.

Mungu akijua hatma yako kua ni motoni basi ni wajibu wake yeye kukufanya usiende motoni kwasababu ana uwezo wote sio juhudi zako za kwenda kusali kanisani ndizo zitabadili hatma yako, wewe hata ukiwa na uwezo wa kujua hatma yako bado huwezi kuibadilisha kwasababu huna mamlaka na uwezo wote wakubadili hilo kwaiyo ishu sio kuona ishu ni kilichoonwa kua kitatokea kinaweza kuepukika endapo ukipewa nafasi ya kukiona?

UTAJUAJE KUWA YEYE ALIONA WEWE UTAINGIA MOTONI?
Hebu naomba unijibu hili angalau.
[/QUOTE]
wakati huo nakua najua kua mungu ni mjuzi wa yote na alishaona kila kitu kabla sijazaliwa na kwakujua huko siwezi nikaepuka chochote niende tofauti na yeye alivyoona??

Pili kama wanaoenda motoni ni wale wenye dhambi na katika sheria zake zimesema usiue na pia zimesema usijue, halafu ikatokea mtu anajua hizo sheria akaua kwa makusudi bila kutubu. Anajua kua amefanya dhambi kwa kosa la kuua then akaamua kujiua

Jiulize

Inamaana huyo mtu kafa bila kujua hatma yake kua ataenda motoni ilihali anavyofanya hizo dhambi alikua akijua kabisa kua hiii ni dhambi na itamsababishia kwenda motoni??

Pia je kwa kufanya hivyo huoni kwamba mungu alikwisha kuona tukio hilo la mauaji kabla kua litakuja kutokea, na kwanini hakuliepusha lisifanyike kwa kunusuru maisha ya huyo muuaji na huyo aliyeuawa bila hatia???

Na kwanini mungu aliruhusu jambo hilo lifanyike huku akijua kua kuna mtu asiye na hatia atauliwa bila sababu yeyote inamaana naye mungu alifurahia kuona mtu mwingine anauliwa kwasababu tu ya hulka ya kuua kutoka kwa mtu mwingine???

Hujajibu swali, kwanini mimi nielewe uwepo wake wewe ushindwe kuelewa? Au umechagua tu kutoamini uwepo wake kwa sababu humuoni? 😀

Hapo juu Umesema kua mungu ndiye mtoaji wa ujuzi kwa viumbe vyake sasa ikitokea kuna mpishano wa huo ujuzi baina ya watu wake hiyo inamaana kua mungu hajanipa ujuzi wa kutosha kuniwezesha nami ni jue kama wewe

Vuta picha mimi nawewe tumeenda kununua iPhone 11 wote tumebeba pesa sawa sawa na kila mtu kauziwa simu sawa sawa kimuonekano halafu kiutendaji kazi zikawa zimepishana

yani hii iPhone yangu ikawa ina ram 200MB na internal storage pia ni 5KB wakati wewe iphone yako ina ina specifications zilizo bora na kubwa kuliko yangu. Mimi nalaumu kua nimeuziwa gaka wewe unasema sio gaka mbona mimi kwangu inafanya kazi vizuri? Umesahau kwamba simu yako kufanya kazi vizuri hakuondoi maana kua sijauziwa gaka

Mimi nakuambiwa sijapewa ujuzi wa kutosha kuweza kuelewa, wewe unasema mbona mimi naelewa! Dude are you stoned?

Mungu angekufanya uelewe, ile dhana ya uhuru yote ingefutika.

Dhana ya uhuru ili iwepo basi mungu asijue kila kitu na kama akijua basi niweze kubadilisha alicho kijua nikaenda tofauti na alivyojua, na nikienda tofauti na alivyojua basi hawezi kua mjuzi wa yote. Kwaiyk mungu akiwa na sifa hizo hapo uhuru haupo

Hata mimi Allah hajanifanya nimuelewe, ila amenipa akili ya kuchambua mambo na kujitafutia elimu.
Kwanini hajakupa uelewa wa kumuelewa?? Huyu mungu kumbe hataki tumuelewe sasa usipomuelewa kwasababu hajakupa uelewa atakuhukumu vipi kua hujamuelewa??

Hata mimi Allah hajanipeleka msikitini ila amenipa miguu niitumie kwenda uko.
Kakupa miguu kakunyima uelewa sasa hata ukienda msikitini kama huna uelewa hiyo si kazi bure?

Ubongo wako umepewa uufanyie nini? utafute pesa tu na ulewe?

ubongo wangu unamapungufu mengi ambayo hata yeye anayajua ila hajataka nisiwe na mapungufu kwasababu uwezo wa kunifanya nisiwe na maoungufu anao ila kaamua tu kutonipa uwezo huo. Hata wewe una ubongo ila huna uwezo wa kuhifadhi kila kitu au hata uwezo wa kukumbuka matukio yaliyofanyika wakati unazaliwa.

Ubongo wako una imperfections nyingi ambazo mungu huyu alitakiwa azi fix lakini ushajiuliza kwanini amekuacha ukiwa hivyo?? Maana yake kakupangia uwe hivyo inamaana unapokutana na magumu ambayo ubongo wako hauwezi kupambanua hapo sio kosa lako kwasababu umewekewa limit mungu hataki wewe ujue angetaka ni lazima wewe ungejua. Na kutokujua huko kunaondoa dhana ya uhuru wa kuchagua kwasababu unachotaka kukichagua kimepigwa pin hakiwezi kufanyika kama unavyotaka
 
wengine wanateseka wengine wanakula bata mungu mmoja huyohuyo
 
Unajuaje kama hujapewa uwezo wa kuelewa?

kwasababu naelewa kwamba anaelewa, umeelewa??

Unajuaje kama Mungu amejua kama hujaelewa?
Ni kwasababu bado naendelea kuhoji kuhusu yeye na sipati majibu ya kuridhisha

kama amejua kuwa umeelewa ila hutaki je?
Hapana atakua naye hajajua nacho kielewa. Ikiwa kama mungu amejua akili yangu kua ili nimuelewe sihitaji vitabu kwasababu havijajitosheleza kunifanya nielewe na ili niweze kumuelewa vyema bila bugdha nitamuhitaji yeye ashuke sio kunipa maandishi ya kina yesu na mudy kua niwatume wake kwasababu kaishajua sitaamini

atangaze hadharani wote tumuone kua yeye ni mungu ili wote tusiomuamini. Sasa kama anajua nacho kiwaza kwanini hajashuka ili nimuone uso kwa uso ili nami niweze kujua??

Hujajaaliwa kuelewa jibu? Nimekwambia kuwa Mitihani ni kwa ajili yako na sio yeye. rudia ulichoquote.
Umesema "Mungu anatoa mtihani ili watu waweze kujitambua" inamaana bila mtihani hawawezi kujitambua??

Kwanini mungu hakuumba watu waweze kujitambua bila kupewa mitihani??

Kwanini mungu anahukumu katika mambo ambayo hayamuhusu ikiwa kama mtihani ni kwaajili yetu??

Anakuhukumu kwamba umekosea katika mtihani aliokupa wakati alishajua kua utakosea, huyu mungu au robot?

Allah anafanya lile litakalo
sawa ila akifanya kinyume na sifa zake alizojiwekea na zinazotangazwa na nyie waumini lazima tutie mashaka
 
kwasababu naelewa kwamba anaelewa, umeelewa??
Kama unaelewa kwamba anaelewa, sasa unapinga nini uwepo wake ikiwa unaelewa kuwa yeye anaelewa?

Hapana atakua naye hajajua nacho kielewa. Ikiwa kama mungu amejua akili yangu kua ili nimuelewe sihitaji vitabu kwasababu havijajitosheleza kunifanya nielewe na ili niweze kumuelewa vyema bila bugdha nitamuhitaji yeye ashuke sio kunipa maandishi ya kina yesu na mudy kua niwatume wake kwasababu kaishajua sitaamini

atangaze hadharani wote tumuone kua yeye ni mungu ili wote tusiomuamini. Sasa kama anajua nacho kiwaza kwanini hajashuka ili nimuone uso kwa uso ili nami niweze kujua??
Hoja mfu, vitabu vya dini vimeshasema kuwa haiwezekani kumuona kwa sababu ya utukufu wake. Kawatuma Issa a.s na Muhammad s.a.w kuwafikishia ujumbe Binaadam wenzao, Hakumtuma mbuzi wala kondoo kuja kufikisha ujumbe.

Utakavyo wewe sivyo atakavyo yeye, kwamba eti ashuke aje akwambie kama "mimi hapa" umepewa ubongo uufanyie kazi, fanya kazi ujue uchungu wa kutafuta ili ukipatapo ujue kufurahia. Wewe ni nani eti utake Mungu ajitangaze hadharani? 😀

Naona sasa umekosa hoja unahamia utotoni.

Umesema "Mungu anatoa mtihani ili watu waweze kujitambua" inamaana bila mtihani hawawezi kujitambua??
Ndio, huwezi kujitambua. hivi utajuaje kama wewe muadilifu kwa mkeo ikiwa hujapata mtihani wa kukutana na mwanamke wa kukulaghai? au ulifikiri mtihani ni kwamba mateso tu? 😀

Kwanini mungu hakuumba watu waweze kujitambua bila kupewa mitihani??
Yeye ndio Muumbaji, yeye ndio anaamua anataka kuumba kiumbe gani na kiwe vipi.

Kwanini Steve Jobs ameita kampuni Apple na asiite NANASI au EMBE DODO? Na kwanini IOS haitumiki kwenye Samsung?

Kwanini mungu anahukumu katika mambo ambayo hayamuhusu ikiwa kama mtihani ni kwaajili yetu??
Kwanini asihukumu ikiwa mtihani unatoka kwake? Kwani mashuleni mkipewa mtihani huwa kwa faida ya nani?

Anakuhukumu kwamba umekosea katika mtihani aliokupa wakati alishajua kua utakosea, huyu mungu au robot?
Kama umekosea mtihani alokupa tena kwanini asikuhukumu kuwa umekosea? Mifano hai, hivi unadhani walimu hawajui kama kuna wanafunzi watafeli tu? sasa kwanini wanawapa mitihani halafu na kuwahukumu kuwa wamefeli?

sawa ila akifanya kinyume na sifa zake alizojiwekea na zinazotangazwa na nyie waumini lazima tutie mashaka
Sifa gani ambayo anayo halafu anafanya kintume?
 
Kama Lengo la mtihani ni kunijuza halafu mungu alijua kua akinipa mtihani sitaweza kujua, kwanini atoe hukumu kwa kosa ambalo lipo nje ya uwezo wangu ambalo sikuwa na uwezo wa kuliepuka???
Ulijuaje kama huna uwezo wa kuliepuka?

Kama mungu kaamua kila mtu awe na ujuzi wake aliopangiwa na watu wametofautiana katika huo ujuzi, inakuaje tena atoe hukumu kwa watu ambao wana ujuzi mdogo kwa kutoelewa mafunzo yake wakati yeye ndiye aliyewapa ujuzi huo mdogo usioweza kuelewa vitu vikubwa???
Kuelewa uwepo wa Mungu haihitaji elimu ya juu, na Mungu hajakupangia ujuzi, ila amekupa ubongo tena kila mtu na ujuzi wake kwa vile atakavotafuta elimu. Haiwezekani ukae kitako nyumbani useme ah mi sijapewa ujuzi wa kutafuta kazi, nani atakuelewa.

taasisi tu ya upigaji
Imesaliwa na nani?

Kutokujua maono ya mungu sio kigezo cha kutojua sifa ya mungu kua yeye ni mpangaji wa maisha ya binadamu

na hakuna jambo linalotokea kwa bahati mbaya everything is part of his plans. Kujiepusha au kutokujiepusha hakubadili kitu
Narudia tena, Mungu hajakupangia kuwa wewe unaingia peopni au motoni. Na kujua kwake khatma yako hakujahalalisha wewe kukaa ndani tu. Kama huna purpose, si ujiue tu yaishe? ukae uteseke, uje upate maradhi uhangaishe watu, jiue kabisa tu.

najadiliana kwa kuchukua upande wako unaosimamia ili tuweze kuelewana na ndio maana hakuna sehemu nimekuambia uthibitishe mungu yupo kwasababu najua tu hayupo na huwezi kuthibitisha
Sina haja ya kukuthibitishia uwepo wa Mungu, kwa sababu umechagua kutoamini uwepo wake bila hoja yoyote ya elimu. Hata mimi najua ukiendelea ivo utaingia motoni tu 😀 Huwezi kumtolea mfano Mungu na kiumbe chengine ikiwa huamini uwepo wa Mungu na hicho kiumbe kingine. Ikiwa umemtolea mfano Mungu kuwa kama shetani, basi bila shaka shetani unamjua wewe 🙂 Atheist kwa kujigonga gonga bana....

unabahatisha?
Mitego ipo

hii ni juu yako
Sio juu yangu, ni juu yako kuthibitisha kama ni muumin au sio muumin, wewe ndio uliepewa habari na huyo unaemuita muumin. Yawezekana hata maana ya muumin hujui lakini. Anaweza kuwa muumin wa ujinga?

ukijua kua mungu alijua hatma yako yote kabla hata hujazaliwa hivyo huna haja ya kujisumbua kujua kwasababu kila kitu ni mipango yake na hakuna jambo utakalolifanya liwe geni kwake.

Mungu akijua hatma yako kua ni motoni basi ni wajibu wake yeye kukufanya usiende motoni kwasababu ana uwezo wote sio juhudi zako za kwenda kusali kanisani ndizo zitabadili hatma yako, wewe hata ukiwa na uwezo wa kujua hatma yako bado huwezi kuibadilisha kwasababu huna mamlaka na uwezo wote wakubadili hilo kwaiyo ishu sio kuona ishu ni kilichoonwa kua kitatokea kinaweza kuepukika endapo ukipewa nafasi ya kukiona?
Ipo haja kubwa ya kufanya ibada ikiwa wewe hujui hatma yako. Ama kama wewe unajua hatma yako na kwamba unajua ni motoni tu, basi huna haja ya kufanya ibada.

Mungu akijua khatma yako kuwa ni motoni, hana wajibu wa kukufanya wewe usiende motoni, ni wajibu wako mwenyewe uliepewa uwezo wa kutofautisha zuri na baya kuchagua kama unataka kwenda peponi au motoni.

wakati huo nakua najua kua mungu ni mjuzi wa yote na alishaona kila kitu kabla sijazaliwa na kwakujua huko siwezi nikaepuka chochote niende tofauti na yeye alivyoona??

Pili kama wanaoenda motoni ni wale wenye dhambi na katika sheria zake zimesema usiue na pia zimesema usijue, halafu ikatokea mtu anajua hizo sheria akaua kwa makusudi bila kutubu. Anajua kua amefanya dhambi kwa kosa la kuua then akaamua kujiua

Jiulize

Inamaana huyo mtu kafa bila kujua hatma yake kua ataenda motoni ilihali anavyofanya hizo dhambi alikua akijua kabisa kua hiii ni dhambi na itamsababishia kwenda motoni??

Pia je kwa kufanya hivyo huoni kwamba mungu alikwisha kuona tukio hilo la mauaji kabla kua litakuja kutokea, na kwanini hakuliepusha lisifanyike kwa kunusuru maisha ya huyo muuaji na huyo aliyeuawa bila hatia???

Na kwanini mungu aliruhusu jambo hilo lifanyike huku akijua kua kuna mtu asiye na hatia atauliwa bila sababu yeyote inamaana naye mungu alifurahia kuona mtu mwingine anauliwa kwasababu tu ya hulka ya kuua kutoka kwa mtu mwingine???
Bado hujajibu swali, unajua kuwa Mungu anajua Khatma yako lakini hujajua kile anachokijua, sasa je unajua khatma yako ya mwisho ni ipi?

Huyo mtu aloua na akajiua, si tayari anazijua sheria na hukumu zake? Sasa akienda kinyume chake mana yake amejichagulia mwenyewe njia ya kwenda motoni kwani alikuwa na uwezo wa kuepuka kufanya ivo.

Pia Hakuliepusha hilo kutokea kwa sababu lau kama angeliepusha maana yake ile sifa yake ya kuwa anajua kila kitu kabla hakijatokea ingefutika. Pia lau kama angeliepusha kutokea, wewe ungekuja kuhoji kwanini hajaliachia tu litokee?

Hapo juu Umesema kua mungu ndiye mtoaji wa ujuzi kwa viumbe vyake sasa ikitokea kuna mpishano wa huo ujuzi baina ya watu wake hiyo inamaana kua mungu hajanipa ujuzi wa kutosha kuniwezesha nami ni jue kama wewe

Vuta picha mimi nawewe tumeenda kununua iPhone 11 wote tumebeba pesa sawa sawa na kila mtu kauziwa simu sawa sawa kimuonekano halafu kiutendaji kazi zikawa zimepishana

yani hii iPhone yangu ikawa ina ram 200MB na internal storage pia ni 5KB wakati wewe iphone yako ina ina specifications zilizo bora na kubwa kuliko yangu. Mimi nalaumu kua nimeuziwa gaka wewe unasema sio gaka mbona mimi kwangu inafanya kazi vizuri? Umesahau kwamba simu yako kufanya kazi vizuri hakuondoi maana kua sijauziwa gaka

Mimi nakuambiwa sijapewa ujuzi wa kutosha kuweza kuelewa, wewe unasema mbona mimi naelewa! Dude are you stoned?
I am not stoned, because i know, you chose not to believe, it is not like you do not understand. Kwa sababu kama wewe unaamini kuwa Ulimwengu haukuwa na muumbaji na hauna purpose, basi kwanini sisi tusiwe tunaishi maisha sayari ya Mars? kwanini kwenye solar system yetu tuko peke yetu? Kwanini position ya dunia iko on the right place to support life, kwanini isiwe venus? Hivi unataka kunambia kuwa lile jengo la ikulu magogoni limejijenga wenyewe bila ya fundi?

Uwepo wa Mungu hauhitaji kusoma mabuku, uwepo wa Mungu ni LOGIC tu. HAKUNA KIUMBE KILICHOKUWA HAKINA MUUMBAJI, NA HAKUNA KILICHOUNDWA KIKAKOSA MUUNDAJI. Kama vipo thibitisha!

Nikurudishie huwo mfano wako wa iphone 11.
Basi ni wajibu wangu mwenye iphone original kukuambia kuwa simu yako feki kwa sababu fulani na fulani. Siwezi kukwambia kuwa umeziwa simu chaka ikiwa sijui tofauti ya chaka na original. Ninapokwambia kuwa simu yako kimeo na wewe ukabisha, hasara anaipata nani? au nani atakuwa mjinga in this case? Itakuwa umechagua kuamini utakavyo wewe na sio vile ilivyo ukweli, kwa sababu ya wewe kukataa kuwa simu yako sio kimeo hakuondoshi kuwa simu yako ni kimeo.

Dhana ya uhuru ili iwepo basi mungu asijue kila kitu na kama akijua basi niweze kubadilisha alicho kijua nikaenda tofauti na alivyojua, na nikienda tofauti na alivyojua basi hawezi kua mjuzi wa yote. Kwaiyk mungu akiwa na sifa hizo hapo uhuru haupo
Nilikuletea maana ya freedom/uhuru. Sivyo hivo unavojaribu kuaminisha watu. naileta tena;
Freedom - the power or right to act, speak, or think as one wants. kwa kiswahili tu ni kusema kuwa Uhuru ni uwezo wa kufanya lile utakalo. Sasa mtu kujua utafanya nini kunaondoaje uhuru? Hapa utaona kuwa umechagua kutoamini uwepo wake bila ya kuwa na hoja yoyote kiasi kwamba hata maana ya uhuru sasa unaipindisha.

By the way, ukienda tofauti na alivyojua? wewe utajuaje kuwa umeenda tofauti, kwani umejua? 😀

Kwanini hajakupa uelewa wa kumuelewa?? Huyu mungu kumbe hataki tumuelewe sasa usipomuelewa kwasababu hajakupa uelewa atakuhukumu vipi kua hujamuelewa??
Kwa sababu Ametupa ubongo/akili za kutumia ili tumuelewe. Mungu ndivyo ALIVYOTAKA YEYE sio UTAKAVYO WEWE.

Mbona wewe hujajiumba mwenyewe utakavyo basi? 😀

Kakupa miguu kakunyima uelewa sasa hata ukienda msikitini kama huna uelewa hiyo si kazi bure?
Utaendaje msikitini ikiwa hujamuelewa? unaenda kufanya nini na kilichokupeleka msikitini nini? :O

ubongo wangu unamapungufu mengi ambayo hata yeye anayajua ila hajataka nisiwe na mapungufu kwasababu uwezo wa kunifanya nisiwe na maoungufu anao ila kaamua tu kutonipa uwezo huo. Hata wewe una ubongo ila huna uwezo wa kuhifadhi kila kitu au hata uwezo wa kukumbuka matukio yaliyofanyika wakati unazaliwa.

Ubongo wako una imperfections nyingi ambazo mungu huyu alitakiwa azi fix lakini ushajiuliza kwanini amekuacha ukiwa hivyo?? Maana yake kakupangia uwe hivyo inamaana unapokutana na magumu ambayo ubongo wako hauwezi kupambanua hapo sio kosa lako kwasababu umewekewa limit mungu hataki wewe ujue angetaka ni lazima wewe ungejua. Na kutokujua huko kunaondoa dhana ya uhuru wa kuchagua kwasababu unachotaka kukichagua kimepigwa pin hakiwezi kufanyika kama unavyotaka
Allah ametaka kuumba kiumbe ambacho kitaitwa Binaadamu/Human. Sasa mwenyewe alichagua kuwa kiumbe hichi ili kiitwe human, basi kitakuwa na sifa kadhaa wa kadhaa. Sasa kama hakutuumba ivi tulivyo, maanake sisi sio binaadamu tena, ni kiumbe kingine. Kwaio ili tuwe binaadamu basi hivi ndivyo alivotuumba, angetuumba na pembe kichwani basi ingekuwa kiumbe kingine. Pia ameumba kiumbe aina ya Malaika, hawa kawaumba wakiwa hawana matamanio ya nafsi kabisa na hawana free will, wao ni kutii amri tu, sasa hawa sio binaadamu, hawa tunawaita Malaika, sifa za malaika ndio hizo, sasa ikiwa ana sifa ya free will huyo sio tena malaika.

Sasa kama unajua kuwa Mungu angetaka hivi basi kwanini ukatae kuwa ndio hakutaka sasa? Hakutaka kukulisha kila kitu kwa sababu amekupa ubongo ufanyie kazi. Angetaka Mungu dunia angeligeuza kuwa pepo lakini HAKUTAKA na AMETAKA DUNIA IWE MAPITO NA SEHEMU YA KUCHUMA THAWABU, AMETAKA IVO. Sasa wewe nani hata umpangie UTAKAVYO wewe? Wewe ukitengeza robot si unamtengeza utakavyo? kwa purpose uitakayo?
 
Kama unaelewa kwamba anaelewa, sasa unapinga nini uwepo wake ikiwa unaelewa kuwa yeye anaelewa?

inaonekana bado hujaelewa

Nimekuambia nimechukua upande wako unaosimamia kua mungu yupo ili nikuoneshe madhaifu wa huyo mungu ilihali nikijua kabisa kua mungu huyu hayupo zaidi ya hadithi.

Ni sawa na mtu ambaye ameleta hadithi ya panya aliyemfunga paka kengele ili tuijadili, japokua najua panya na paka huyo ni hadithi zakutungwa nitaendelea kutoa hoja za kupinga endapo kutakua na mtu anaepindisha stori hiyo hata kama ni hadithi ya kufikirika.

Hoja mfu, vitabu vya dini vimeshasema kuwa haiwezekani kumuona kwa sababu ya utukufu wake. Kawatuma Issa a.s na Muhammad s.a.w kuwafikishia ujumbe Binaadam wenzao, Hakumtuma mbuzi wala kondoo kuja kufikisha ujumbe.
Mungu mwenye uwezo wote inaama hawezi kutumia uwezo wake kufanya nimuone bila tatizo lolote???

Unajuaje kwamba vitabu vya dini vimezungumza ukweli kuhusu hilo na sio kwamba vimeongopa ili watu wasihoji kuhusu hilo kwasababu mungu hayupo???

Utakavyo wewe sivyo atakavyo yeye, kwamba eti ashuke aje akwambie kama "mimi hapa" umepewa ubongo uufanyie kazi, fanya kazi ujue uchungu wa kutafuta ili ukipatapo ujue kufurahia. Wewe ni nani eti utake Mungu ajitangaze hadharani? 😀

hapa unaonesha wewe ndio hutaki iwe hivyo, inamaana mungu hawezi kufanya hivyo na bado ikawa sehemu ya matakwa yake??

mungu kama kaiona akili yangu inavyofikiri na akajua kabisa ili mimi niweze kumjua njia pekee ni yeye kushuka nimuone ana kwa ana kuna sababu yeyote ya msingi inayomkwamisha huko juu ashindwe kuja nimuone?

Ndio, huwezi kujitambua. hivi utajuaje kama wewe muadilifu kwa mkeo ikiwa hujapata mtihani wa kukutana na mwanamke wa kukulaghai? au ulifikiri mtihani ni kwamba mateso tu? 😀

Kama huwezi kujitambua bila kupewa mtihani basi huyu si mungu mwenye uwezo wote kwasababu kashindwa kukufanya ujitambue bila kukupa mtihani

Hata baada ya kupewa mtihani bado kuna watu hatujitambui, hiyo pia inathibitisha kua njia ya mungu kutumia mtihani ili watu wake waweze kujitambua ni dhaifu

Yeye ndio Muumbaji, yeye ndio anaamua anataka kuumba kiumbe gani na kiwe vipi.

Kwanini Steve Jobs ameita kampuni Apple na asiite NANASI au EMBE DODO? Na kwanini IOS haitumiki kwenye Samsung?
hujajibu swali, kama mungu ni muweza wa yote alishindwa kufanya watu waweze kujitambua bila kupewa mtihani??

Steve jobs ni mjuzi wa yote na muweza wa yote??

Kwanini asihukumu ikiwa mtihani unatoka kwake? Kwani mashuleni mkipewa mtihani huwa kwa faida ya nani?

na kwanini ahukumu wakati alikwisha jua kua utakosea ilihali uwezo wa kukuepusha usikosee alikua nao??? Kama kosa likifanywa ni wajibu wa aliyefanya aadhibiwe basi mungu ndiye kinara wa makosa je yeye anaadhibiwa na nani??

Mashuleni tunapewa mtihani kwa faida ya walimu na wanafunzi, mwalimu kupitia mtihani wako anapata mshahara pia akifaulisha vizuri hupewa tuzo na kupandishwa cheo.

mwalimu pia hupata hasara endapo ikatokea amefelisha wanafunzi huonekana hayuko makini au hana uwezo wa kitaaluma hivyo hupelekea kushushwa cheo au kufukuzwa kabisa.

Swali langu hili hujajibu

Je mungu anapata faida gani kuchoma watu motoni au hupata hasara gani endapo hatowachoma watu motoni??

Kama umekosea mtihani alokupa tena kwanini asikuhukumu kuwa umekosea?

na kakishajua kua nitakosea kwanini asinipe uwezo wa kufauru mtihani bila kukosea wakati uwezo wote wa kufanya hilo anao??

Nijuavyo mimi Kusudio la adhabu ni kwasababu kosa likifanyika haliwezi kusawazishika yani kurudi nyuma ya muda ulirekebishe kosa ulilofanya ili lisiwe kosa.

Kwaiyo adhabu hutolewa na watu ambao hawana uwezo wa kusawazisha mabaya ambayo hawayawezi kuyapindua yasiwe mabaya na ndio maana wanakua hawana namna ya kuridhisha nafsi zao zaidi ya kutoa adhabu. Lakini mungu uwezo wa kusawazisha hilo baya ulilolifanya lisiwe baya anao kwanini ameacha mabaya yafanyike wakati uwezo waku undo mabaya yaliyofanyika yasifanyike??

Mifano hai, hivi unadhani walimu hawajui kama kuna wanafunzi watafeli tu?
wanajua kua kuna watu watafeli kwasababu wanajua wapo miongoni mwa wanafunzi ambao hawana uwezo wa kufaulu vizuri ila hawajui kwa hakika kua wangapi watafeli na ndio maana wanatoa mitihani, hawajui kwa hakika kwasababu inaweza ikatokea yule ambaye alikua akiongoza darasani nafasi ya ukwanza akaja kuwa mtu wa 10

Lakini pia walimu pamoja na kujua huko kua wanafunzi watafeli, walimu hawana uwezo wa kubadili hili kufanya wanafunzi wote wafauru. Kwaiyo mfano wako ulilenga khonesha mungu ni mjuzi wa yote lakini hana uwezo wa kubadilisha alichokiona na ndio maana anatoa mitihani kama mwalimu???

sasa kwanini wanawapa mitihani halafu na kuwahukumu kuwa wamefeli?

wanawapa mitihani kwasababu hakuna namna nyingine ya kumfanya mwanafunzi aelewe bila mtihani, wanawapa mitihani kwasababu hawajui kwa hakika nini kitatokea mbele.

Wanawapa hukumu kwasababu hawana uwezo wa kuwafanya wanafunzi wafanye yale wanayoyataka nje ya mtihani

Walimu wanatoa adhabu kwa wanafunzi kwasababu wanakua wameshushwa CV na wanafunzi kua hawana uwezo wa kufundisha darasani

Mungu anatoa adhabu kwa sababu zipi?

Sifa gani ambayo anayo halafu anafanya kintume?

mjuzi wa yote muweza wa yote

Amejua kua nitaiba halafu akaacha tukio hilo lifanyike badala ya kulizuia wakati uwezo wakuzui anao.

NB:Mungu hayupo zaidi ya stori tu
 
Kuna kila dalili kwamba Mungu Hayupo na kama kweli yupo basi yawezekana hawezi yote_Wapinga uwepo wake wanahoja zisizopaswa kupuuzwa kwa kweli

Sijaona mfia dini mwenye hoja zenye mashiko kuliko wapingaji wa uwepo wa Mungu

Nadhani mzigo umewaelemea yapaswa huyo Mungu ajitete mwenyewe tu_hakuna namna
 
inaonekana bado hujaelewa

Nimekuambia nimechukua upande wako unaosimamia kua mungu yupo ili nikuoneshe madhaifu wa huyo mungu ilihali nikijua kabisa kua mungu huyu hayupo zaidi ya hadithi.

Ni sawa na mtu ambaye ameleta hadithi ya panya aliyemfunga paka kengele ili tuijadili, japokua najua panya na paka huyo ni hadithi zakutungwa nitaendelea kutoa hoja za kupinga endapo kutakua na mtu anaepindisha stori hiyo hata kama ni hadithi ya kufikirika.
Kikubwa utakachopinga kwenye hio hadithi ni panya kumfunga kengele paka, lakini hutopinga uwepo wa panya na paka.

Mungu mwenye uwezo wote inaama hawezi kutumia uwezo wake kufanya nimuone bila tatizo lolote???

Unajuaje kwamba vitabu vya dini vimezungumza ukweli kuhusu hilo na sio kwamba vimeongopa ili watu wasihoji kuhusu hilo kwasababu mungu hayupo???
Mungu ametuumba ivo kutokuwa na uwezo wa kumuona. Wapo wanaoamini kuwa watamuona siku ya akhera watakapoingia peponi ambapo atavua pazia ambalo linatuzuia kumuona na wapo ambao wanaamini hatoonekana kabisa. All in all, ametuumba kutokuwa na uwezo wa kumuona.

ili kujua kuwa kitabu kinasema uongo, basi unapima hali halisi. Mimi nakupa challenge, lete aya kwenye Quran ambayo unaona ina mashaka na uongo. Ama wewe unapimaje kujua ukweli na uongo?

hapa unaonesha wewe ndio hutaki iwe hivyo, inamaana mungu hawezi kufanya hivyo na bado ikawa sehemu ya matakwa yake??

mungu kama kaiona akili yangu inavyofikiri na akajua kabisa ili mimi niweze kumjua njia pekee ni yeye kushuka nimuone ana kwa ana kuna sababu yeyote ya msingi inayomkwamisha huko juu ashindwe kuja nimuone?
Sio mimi sitaki uwe ivyo, ila wewe ndio hutaki atakavyo Mungu ila unataka utakavyo wewe.

Ukiona kuwa hajaja ivo unavotaka wewe basi ujue kuwa anajua kuwa unaelewa ila hutaki na hata kama ungemuona ungemkataa, sasa tena kwanini akujie akwambie mie hapa?

Kama huwezi kujitambua bila kupewa mtihani basi huyu si mungu mwenye uwezo wote kwasababu kashindwa kukufanya ujitambue bila kukupa mtihani

Hata baada ya kupewa mtihani bado kuna watu hatujitambui, hiyo pia inathibitisha kua njia ya mungu kutumia mtihani ili watu wake waweze kujitambua ni dhaifu
Huyo ndio Mungu haswa, kwa sababu anafanya vile atakavyo yeye na sio utakavyo wewe. Sasa kama ukichepuka unasema kuwa hujui kama umechepuka, nani atakuamini? Yaani unajua kama una mke, kwa choice yako mwenyewe unaamua kuchepuka, halafu unawaambia watu hujui kama unachepuka ukiwa unazini na huo mchepuko 😀

hujajibu swali, kama mungu ni muweza wa yote alishindwa kufanya watu waweze kujitambua bila kupewa mtihani??

Steve jobs ni mjuzi wa yote na muweza wa yote??
Swali limejibiwa kiuwazi kabisa, ila nakujibu tena, Hakushindwa kufanya ivo, bali ametaka iwe hivo.

Steve Jobs sio mjuiz wa yote na muweza wa yote, alikuwa hajui kama kuna tunda jengine isipokuwa Apple? Naomba unijibu tafadhali.

na kwanini ahukumu wakati alikwisha jua kua utakosea ilihali uwezo wa kukuepusha usikosee alikua nao??? Kama kosa likifanywa ni wajibu wa aliyefanya aadhibiwe basi mungu ndiye kinara wa makosa je yeye anaadhibiwa na nani??
Makosa gani Mungu amefanya? Naomba uyaorodheshe tafadhali.

Je mungu anapata faida gani kuchoma watu motoni au hupata hasara gani endapo hatowachoma watu motoni??
Hili Swali umeuliza wapi? Anyways jibu lako ni hili, Mungu ameweka taratibu za maisha na ameshaweka bayana ukienda kinyume nazo, basi kuna adhabu na ameshasema adhabu gani. Mungu hapati hasara yoyote akiwachoma ama asipowachoma, ila kwanini Waliodhulumu, walioua waliotenda maovu wasiadhibiwa wawe sawa na wale ambao walifanya ibada na kuwa wachamungu? How can he be the Most Just?

na kakishajua kua nitakosea kwanini asinipe uwezo wa kufauru mtihani bila kukosea wakati uwezo wote wa kufanya hilo anao??
Na akishakupa uwezo wa kufaulu huo mtihani, kuna haja gani basi ya wewe kuumbwa tangu hapo mwanzo? Hivi unajua lengo la Kuumbwa mwanadamu?

Kwaiyo adhabu hutolewa na watu ambao hawana uwezo wa kusawazisha mabaya ambayo hawayawezi kuyapindua yasiwe mabaya na ndio maana wanakua hawana namna ya kuridhisha nafsi zao zaidi ya kutoa adhabu. Lakini mungu uwezo wa kusawazisha hilo baya ulilolifanya lisiwe baya anao kwanini ameacha mabaya yafanyike wakati uwezo waku undo mabaya yaliyofanyika yasifanyike??
Yaani unasema kuwa Mungu asawazishe mauaji yako ya we halali? Na yule alieuliwa atalipwa nini? Hasira zake juu yako uliemuua ataridhika kukuona wewe ukila raha? Sasa moto na pepo ameumbiwa nani ikiwa sote tuwe tunafanya mazuri? Ile sababu ya kuumbwa kwetu itakuwa na maana gani ikiwa kila tulifanyalo ni zuri tu?

wanajua kua kuna watu watafeli kwasababu wanajua wapo miongoni mwa wanafunzi ambao hawana uwezo wa kufaulu vizuri ila hawajui kwa hakika kua wangapi watafeli na ndio maana wanatoa mitihani, hawajui kwa hakika kwasababu inaweza ikatokea yule ambaye alikua akiongoza darasani nafasi ya ukwanza akaja kuwa mtu wa 10

Lakini pia walimu pamoja na kujua huko kua wanafunzi watafeli, walimu hawana uwezo wa kubadili hili kufanya wanafunzi wote wafauru. Kwaiyo mfano wako ulilenga khonesha mungu ni mjuzi wa yote lakini hana uwezo wa kubadilisha alichokiona na ndio maana anatoa mitihani kama mwalimu???
Walimu wanao uwezo wa kubadili hilo, ni kuwapa 100 chini ya 100 wanafunzi wote ili waendelee na masomo yao, na kupata ajira. Vile vile hata serikali inao uwezo wa kuwalipa raia wake milioni 10 kila mmoja bila kufanya kazi yoyote, lakini cha kushangaza hawalipi, wanataka lazima ufanye kazi ndio ulipwe, walimu wanataka lazima usome kwa bidii ufanye mtihane na upewe marks unazostahili. Vyuo wanataka mpaka upasi wakupe degree, wakati ni karatasi tyu unaweza kupewa kwenda kuombea kazi.

Wapo walimu ambao wanaona hasa fulani anafeli na huwa na uhakika kabisa. Lakini bado anampa mtihani, anapofeli kwenye mtihani huo na kupata zero, atamlaumu nani? atamlaumu mwalimu kuwa mbona hujanielewesha? akiambiwa mbona kuna 99 walielewa yeye atajibu nini?

Kujua outcome haimaniishi kuwa ndio ukae kitako tu, ile outcome itatokeaje ikiwa chanzo hakijafanyika?

wanawapa mitihani kwasababu hakuna namna nyingine ya kumfanya mwanafunzi aelewe bila mtihani, wanawapa mitihani kwasababu hawajui kwa hakika nini kitatokea mbele.

Wanawapa hukumu kwasababu hawana uwezo wa kuwafanya wanafunzi wafanye yale wanayoyataka nje ya mtihani

Walimu wanatoa adhabu kwa wanafunzi kwasababu wanakua wameshushwa CV na wanafunzi kua hawana uwezo wa kufundisha darasani

Mungu anatoa adhabu kwa sababu zipi?
- Anatoa adhabu kwa sababu umechagua kumuasi.

Kwani si hata mimi najua kuwa ukiendelea kumpinga utaingia motoni tu. Je kuna kuhalalishia wewe kuacha kufanya ibada?

mjuzi wa yote muweza wa yote

Amejua kua nitaiba halafu akaacha tukio hilo lifanyike badala ya kulizuia wakati uwezo wakuzui anao.
Ni Mjuzi wa yote na muweza wa yote, lipi aliloshindwa?

Amejua kuwa utaiba na akakuachia uibe wakati alikuwa na uwezo wa kulizuia. umesahau kuwa ulisema "AKAACHA"? hakushindwa ila alifnya nini? 😀

NB: Mungu yupo na atabaki kuwepo, huna hoja za kupinga uwepo wa Mungu na huwezi kuthibitisha Uwepo wetu bila kuwepo Muumbaji. Na kama huna purpose kwenye life, kwanini uendelee kuishi na kutetseka? usipumzike tu kwa kula sumu ukaondoka ulimwenguni?
 
Back
Top Bottom