streat Anthem
JF-Expert Member
- Nov 28, 2016
- 395
- 474
Kiukweli wanaojiita hawaamini uwepo wa Mungu hawajui wanachokitafuta.Na shida ni kwamba wanaowajibu pia hawajui wanachokijibu.
.
Uwepo wa Mungu upo ndani ya Mtu. Na ili Mungu awepo kwako ni lazima utimize mapenzi yake.
Sasa inashangaza anatokea kiumbe anasema " Mungu hayupo" na kwa wakati huo hatimizi mapenzi ya Mungu na wala hajishughulishi kuyajua mapenzi ya Mungu Bali anafuata mapenzi yake mwenyewe.
Halafu wanatokea watu wanaowajibu kuwa Mungu yupo,huku watu hao wakiwa hawayatimizi mapenzi ya Mungu yaani na wenyewe wanafuata mapenzi yao tu!
Mungu anadhihirishwa kwa matendo mema na kuishi vyema. Wote tunaoamini uwepo wa Mungu tungeishi kwa mapenzi ya Mungu hawa wanaojiita Atheists wala hata tusingewasikia.
Tujitahidi jamani kuwasaidie wenzetu kwa matendo yetu mema na upendo ili tuwajibu kwa tunayoyafanya.
Na kizuri zaidi tunajua Cha kufanya yaani tumpende Mungu,tujipende na kuwapenda wote Kama tujipendavyo