Atheist wengi hawajui wanachokitafuta

Atheist wengi hawajui wanachokitafuta

Haingii akilini mtoto wa darasa la pili kuadhibiwa kwa kosa la kufeli mathematics form six. Vile vile Mungu wetu hampi mtu adhabu ikiwa jambo fulani hakulijua ama hakuupata ujumbe. Lakini tambua kuwa, mfano ulioutoa hauendani na jibu nlilokupa.

Ishu sio kuupata ujumbe, hapo huna tofauti na huyo mwalimu aliyemuadhibu mtoto maana hata yeye atajitetea kua alitoa ujumbe siku tatu kabla ya mtihani ili kumpa mda huyo mtoto aweze kusoma vizuri past papers aweze kujibu vyema mtihani wake je utamuelewa??

Ona nlichokwambia;
Mfano, naweza kueka mazingira kuona kama je mtoto wangu wa kike atafanya zinaa au la

mpaka hapa mfano wako ni mfu, kwasababu hujajua kwa hakika kile kitachokwenda kutokea na ndio maana umesema atafanya zinaa au la. Hiyo inamaanisha huna uhakika unafanya betting au pata potea hivyo ikitokea jambo limeenda tofauti na ulivyotaraji kumuadhibu kwako mtoto utakua uko sahihi kwasababu ulichokitegemea kua kitakua kimeenda tofauti.

Lakini mungu yeye alijua kwa hakika na ujuzi wake ni 100% perfect kabla hata hujazaliwa alikwisha jua kua utakosea

baada ya tayari nishamwambia kuwa ukifanya zinaa nitakuchapa .Sasa kupitia mfano wako, mtoto huyo ulimsomesha izo hesabu za form six? hata umuadhibu?

kumsomesha mtu ni kitu kingine na kumsomesha mtu akajua ulichomfundisha ni ishu nyingine

Mungu kama anaadhibu watu kwasababu alishawafundisha basi sio mjuzi wa yote kwasababu hakujua kua watu wake hawakuelewa mafundisho yake, na kama ni mjuzi wa yote kwamba aliweza kujua kua watu wake hawajamuelewa kwenye mafundisho yake basi mungu sio muweza wa yote kwasababu alishindwa kufanya watu wote waelewe

Mwalimu akikwambia kua alimfundisha huyo mtoto utarizika na adhabu aliyopewa mwanao???

Allah anasema katika surat Israa aya ya 15; Anaye ongoka basi anaongoka kwa ajili ya nafsi yake. Na anaye potea basi anapotea kwa khasara yake mwenyewe. Wala habebi mbebaji mzigo wa mwengine. (184, 49, 47)]Wala Sisi hatuadhibu mpaka tumpeleke Mtume.

Haya sasa mahubiri, jenga hoja nje ya viroja
 
Hapa naongelea UKWELI mzee.

Nakukumbusha swali langu.
Na ndio maana nauliza ili nijue ukweli uli, Ukweli kwa muktadha wa dini ya kiisilam pamoja na kuran au?
 
Ishu sio kuupata ujumbe, hapo huna tofauti na huyo mwalimu aliyemuadhibu mtoto maana hata yeye atajitetea kua alitoa ujumbe siku tatu kabla ya mtihani ili kumpa mda huyo mtoto aweze kusoma vizuri past papers aweze kujibu vyema mtihani wake je utamuelewa??
Ishu ni kupata ujumbe, huwezi kumhukumu mtu akiwa hajapata ujumbe, na kama umempa ujumbe, je umemfudisha? Uislam umekufundisha usifanye Zinaa, jiepusha na mabaya ila wewe unatenda maovu basi adhabu inakuhusu tu. Na mtoto vile vile kama umemfundisha na akafeli, basi una haki ya kumuadhibu, lakini kwa sababu umekariri kuwa adhabu lazima kichapo ndio maana unahisi kuwa mtoto huyo mdogo atakuwa anaonewa, unaweza ukamuadhibu hamna kucheza tu.

mpaka hapa mfano wako ni mfu, kwasababu hujajua kwa hakika kile kitachokwenda kutokea na ndio maana umesema atafanya zinaa au la. Hiyo inamaanisha huna uhakika unafanya betting au pata potea hivyo ikitokea jambo limeenda tofauti na ulivyotaraji kumuadhibu kwako mtoto utakua uko sahihi kwasababu ulichokitegemea kua kitakua kimeenda tofauti.

Lakini mungu yeye alijua kwa hakika na ujuzi wake ni 100% perfect kabla hata hujazaliwa alikwisha jua kua utakosea
Mfano haukuwa mfu, ni kwamba hupendi tu unapooneshwa uhalisia. Inawezekana mzee alikuwa na uhakika kuwa mwanawe atafanya zinaa ila amemetengezea mazingira kusudi amkamate akiwa na ushahidi ambao hatoweza kuupinga.

kumsomesha mtu ni kitu kingine na kumsomesha mtu akajua ulichomfundisha ni ishu nyingine

Mungu kama anaadhibu watu kwasababu alishawafundisha basi sio mjuzi wa yote kwasababu hakujua kua watu wake hawakuelewa mafundisho yake, na kama ni mjuzi wa yote kwamba aliweza kujua kua watu wake hawajamuelewa kwenye mafundisho yake basi mungu sio muweza wa yote kwasababu alishindwa kufanya watu wote waelewe

Mwalimu akikwambia kua alimfundisha huyo mtoto utarizika na adhabu aliyopewa mwanao???
Kumuadhibu mtu kwa sababu ulimfundisha hapo mwanzo hakuondoshi ujuzi wa Allah kama vile kujua kwake khatma yako hakuondoshi uhuru wako wa kufanya jema au ovu. Kwanini mimi nielewe mafundisho yake ila wewe usielewe? Kutowafanya watu wote wamuelewa kunaondosha uhuru, na hivo ungekuja kulia kuwa huna uhuru umelazimishwa umuelewa.

Haya sasa mahubiri, jenga hoja nje ya viroja
Hakuna kiroja hapo, ninakuonesha nini Allah ametufundisha kuwa yeye haadhibu mtu ikiwa ujumbe haujamfikia. Sasa labda wewe ulete kiroja tena. mana kile cha uhuru kimemalizwa
 
Na ndio maana nauliza ili nijue ukweli uli, Ukweli kwa muktadha wa dini ya kiisilam pamoja na kuran au?
Sasa rejea kwanza pale tulipa anzia kisha ujibu swali nililo kuuliza tupate kuendelee
 
Sasa rejea kwanza pale tulipa anzia kisha ujibu swali nililo kuuliza tupate kuendelee
Hapa tulipo bado tuko pale pale ukiona kama tumepiga hatua jitafakari umakini wako
 
Ishu ni kupata ujumbe, huwezi kumhukumu mtu akiwa hajapata ujumbe, na kama umempa ujumbe, je umemfudisha?
na huwezi kumhukumu mtu aliyepata ujumbe ambao ulijua kabisa kua hajauelewa na uwezo wa kumfanya aelewe unao. Mungu mjuzi wa yote na mwenye uwezo wote hatakiwi kutoa mafundisho, mungu akikupa mafundisho anapaswa kujua mfumo mzima wa ubongo wako bila hata kukupa mtihani.

Kama mungu akijua kua umeelewa katika mafundisho aliyokuatia je atakupa mtihani ili akupime kuangalia kama umeelewa???

Kama mungu akijua kua hujaelewa, je atakupa mtihani ili aweze kujua kua hujaelewa???

Vile vile mungu kama ni muweza wa yote kwanini ashindwe kukufanya ujue kila jambo analolitaka bila kukupima na mitihani ambayo hata baada ya kugundua kua hujaelewa hakuwezeshi ili nawe uweze kuelewa????

Uislam umekufundisha usifanye Zinaa,
uislam unauwezo wa kuniepusha zinaa bila kunifundisha namna ya kuepuka??? Kama hauna uwezo basi hata kukosea kwangu sitaulaumu kwasababu una imperfection, ila kama unao uwezo wa kunifanya niepuka bila kufundishwa basi ni ujinga kuendelea kunifundisha kitu ambacho kinaweza kuniepushia.

uislam kwanini usifanye mambo automaticaly bila kumfundisha mtu kama ilivyo mmen'genyo wa chakula unavyo fanyika tumboni bila kufundishwa???

jiepusha na mabaya ila wewe unatenda maovu basi adhabu inakuhusu tu.
nijiepushe kivipi na mabaya wakati mungu tayari alishaona kua ntayakwaaa??? Kwaiyo mungu akijua kua nitafanya mabaya mimi naweza nikaepuka nikafanya mazuri???

Na mtoto vile vile kama umemfundisha na akafeli, basi una haki ya kumuadhibu
Wakati huo baba yake sio mjuzi wa yote na muweza wa yote ni kweli nitamuadhibu maana hayakua mategemeo yangu kumuona mtoto wangu anafeli wakati nilimfundisha na itakua hukumu ya haki kwake.

Lakini kwa mungu mwenye sifa ya ujuzi wote na uwezo wote hapaswi kutoa mtihani wala kuadhibu mtu kwasababu hajaelewa wakati uwezo wa kumfanya aelewe bila mtihani anao

lakini kwa sababu umekariri kuwa adhabu lazima kichapo ndio maana unahisi kuwa mtoto huyo mdogo atakuwa anaonewa, unaweza ukamuadhibu hamna kucheza tu.

ikishaitwa adhabu no matter what punishment is, mtoto kama alishazoea kucheza na katika mchezo huo ndio mchezo pekee unaompatia furaha halafu wewe ukaja kumkataza asicheze utakua umemfanya akose raha ambayo alikua akiipata kipindi anacheza huo mchezo.

Adhabu ya mungu kwa watu wake ni moto kwaiyo hii adhabu utaifananisha na adhabu ya huyo mtoto aliyopewa na baba yake?? Yani mzazi kamzidi mungu huruma mzazi ndio kama mungu halafu mungu ndio kama shetani sasa

Mfano haukuwa mfu, ni kwamba hupendi tu unapooneshwa uhalisia. Inawezekana mzee alikuwa na uhakika kuwa mwanawe atafanya zinaa ila amemetengezea mazingira kusudi amkamate akiwa na ushahidi ambao hatoweza kuupinga.[/QUOTE]
kwa kusema tu inawezekana mzee alikua na uhakika umekua umefanya assumption ambayo sio uhalisia na kufanya mfano wako uwe mfu tena

Kumuadhibu mtu kwa sababu ulimfundisha hapo mwanzo hakuondoshi ujuzi wa Allah kama vile kujua kwake khatma yako hakuondoshi uhuru wako wa kufanya jema au ovu.
Kuna muumini mwenzako alisema mungu akiwa na sifa hii ya ujuzi wote halafu akakuadhibu kwa kile alichokiona kua utafanya halafu wewe ukawa huna namna ya kukikwepa basi huyu mungu ni snitch.

Mimi nasema sio snitch kwasababu hayupo angekuwepo kusingekua na dhana ya kusema anatoa mitihani wala uhuru wa kuchagua halafu katika kitu alichokiona huwezi kuchagua tofauti na alivyoona

Kwanini mimi nielewe mafundisho yake ila wewe usielewe?
Inamaana huelewi kua mungu alikwishajua kua sitaelewa mafundisho yake mpaka unauliza hili swali? Hujui kila kitu kinachofanyika hakifanyiki kwa bahati mbaya??

Kwanini yeye mwenye uwezo wote ambao angeweza kuutumia uwezo huo kunifanya namimi nielewe kama wewe, ameshindwa kunifanya nielewe?? kiasi kwamba hata wewe umeona umuhimu wa mimi kuelewa hayo mafundisho je inamaana huyu mungu ajaona umuhimu wa mimi kuelewa hayo mafundisho???

Kutowafanya watu wote wamuelewa kunaondosha uhuru, na hivo ungekuja kulia kuwa huna uhuru umelazimishwa umuelewa.

Hakuna kiroja hapo, ninakuonesha nini Allah ametufundisha kuwa yeye haadhibu mtu ikiwa ujumbe haujamfikia. Sasa labda wewe ulete kiroja tena. mana kile cha uhuru kimemalizwa
Ujumbe ukishamfikia huyo mtu allah anakua hajui kua huyo mtu hajaelewa?? Akijua kua hajaelewa kwanini hakumfanya aweze kuelewa zaidi inamaana allah hana uwezo wa kumfanya mtu akaelewa nje ya adhabu???
 
Hapa tulipo bado tuko pale pale ukiona kama tumepiga hatua jitafakari umakini wako
Hatujaanzia hapa. Unakumbuka ulisema hakuna kisicho kiumbe ? Kisha ukataja vigawanyo vya kiumbe ?

Mimi nikaja nikakuuliza nini maana ya kiumbe na nikauuliza kwa ufafanizi juu ya kiumbe ili kiwe kiumbe huwa kina sifa gani kuu ?

Mgawanyo wa kiumbe hai na kinyume chake baada ya kuwepo kiumbe,sasa nataka uniambie kabla ya mgawanyo wa kiumbe hai na kisicho hai,mlijuaje kipi ni kiumbe na kipi si kiumbe ? Swali rahisi sasa kupoteza muda hakusaidii na kama swali ukiwa huelewi ni bora uulize.

Sasa nimekufafanulia na kukuonyesha hapa ni baada ya kutoka huko.

Nasubiri jibu la swali langu.
 
Hatujaanzia hapa. Unakumbuka ulisema hakuna kisicho kiumbe ? Kisha ukataja vigawanyo vya kiumbe ?

Na ndio maana nakuambia bado tunacheza kwenye duara lile lile la kiumbe

Mimi nikaja nikakuuliza nini maana ya kiumbe na nikauuliza kwa ufafanizi juu ya kiumbe ili kiwe kiumbe huwa kina sifa gani kuu ?

bado uko palepale kwenye "kiumbe" hujavuka border

Mgawanyo wa kiumbe hai na kinyume chake baada ya kuwepo kiumbe,sasa nataka uniambie kabla ya mgawanyo wa kiumbe hai na kisicho hai,mlijuaje kipi ni kiumbe na kipi si kiumbe?

Mgawanyo wa kiumbe hai wewe unauelewaje??? na uligawanywa na nini?

Swali rahisi sasa kupoteza muda hakusaidii na kama swali ukiwa huelewi ni bora uulize.
na ndio maana natoa majibu marahisi

Sasa nimekufafanulia na kukuonyesha hapa ni baada ya kutoka huko.

Nasubiri jibu la swali langu.

Hujafafanua vizuri ukaeleweka kiasi cha kujibiwa swali lako
 
Na ndio maana nakuambia bado tunacheza kwenye duara lile lile la kiumbe

bado uko palepale kwenye "kiumbe" hujavuka border

Unapenda kupoteza muda sana,jambo jepesi ni kujibu lakini unakimbia kimbia,kama hujui sema tu hujuo,hakuna atakae kulaumu kwa kutokujua kwako.

Poa,sasa nijibu swali langu,kwamba Kiumbe ni nini na ili kitu kiwe kiumbe kinatakiwa kiwe na sifa gani kuu,sifa ambayo inaingia katika hiyo migawanyiko miwili.
 
Hii ni mara ya pili nakujibu labda niweke msisitizo kua kila kinacho exist ni kiumbe eidha kiwe hai au sio hai kwa mantiki hiyo hakuna kisicho kiumbe na hii ndiyo nature
 
Hii ni mara ya pili nakujibu labda niweke msisitizo kua kila kinacho exist ni kiumbe eidha kiwe hai au sio hai kwa mantiki hiyo hakuna kisicho kiumbe na hii ndiyo nature
Kwanza maana yako si sahihi.

Unakubali kwamba Jua ni kiumbe ? Upepo nao ni kiumbe ?

Sharti kuu ya Kiumbe lazima kiwe kimeumbwa. Nashangaa ukawa unakimbia kimbia.
 
Kwanza maana yako si sahihi.

Unakubali kwamba Jua ni kiumbe ? Upepo nao ni kiumbe ?

Sharti kuu ya Kiumbe lazima kiwe kimeumbwa. Nashangaa ukawa unakimbia kimbia.

Nikikwambia kua hakuna kisicho kiumbe maana yake you have to stop asking such kind of silly questions
 
Kwanza maana yako si sahihi.

Unakubali kwamba Jua ni kiumbe ? Upepo nao ni kiumbe ?

Sharti kuu ya Kiumbe lazima kiwe kimeumbwa. Nashangaa ukawa unakimbia kimbia.
Hilo sharti la kusema kila kiumbe ni lazima kiwe kimeumbwa umetoa wapi???? Hicho kilichoumbwa na kilichoumba both are either livings things or non living things. Hakuna kisicho kiumbe labda kisiwepo
 
Nikikwambia kua hakuna kisicho kiumbe maana yake you have to stop asking such kind of silly questions
Na mimi ndio nakuonyesha uongo wa kauli yako,na usiwe una andika jambo usilo kuwa na ujuzi nalo sababu unakuwa unaiokosea adabu elimu.

Lazima uulizwe maswali na uyajibu ili ujue uongo na ujinga wako ulipo,na ujue kutofautisha mambo na uijue mipaka yake,sio kila linalo kujia akili mwako unaliandika,wenye akili timamu lazima wachuje.

Na usiwe unasema hovyo bila kuhakiki kauli zako,ulitakiwa ujue ukweli wa kauli yako kabla ya kuiandika. Lazima ujue kutofautisha uumbaji,uundaji na utengenezaji. Wewe kwa akili yako ya kitoto unaweza kusema Gari nalo ni kiumbe ? Ukiulizwa utasema ni kiumbe kisicho hai,hivi una akili wewe ?

Hakuna lugha yoyote inayoyaweka sehemu moja kujenga,kutengeneza na kuumba kisha yakaleta maana moja. Misingi ya lugha nayo uhukumu.

Kila siku nakwambia juu ya umakini na kuhakiki mambo kabla ya kuandika,ili uepuke kuonekana kituko na mjinga.
 
Hilo sharti la kusema kila kiumbe ni lazima kiwe kimeumbwa umetoa wapi????
Acha utoto wa kukwepa maswali unayo ulizwa,jibu maswali yangu kisha nikujibu yako.

Hilo sharti nimelipata katika misingi ya lugha na matumizi ya tamko hilo na asili yake.

Hicho kilichoumbwa na kilichoumba both are either livings things or non living things. Hakuna kisicho kiumbe labda kisiwepo
Hii kauli unatakiwa uithibitishe na kuonyesha ukweli wake,usitumie tamko "Labda" katika uhalisia.
 
Acha utoto wa kukwepa maswali unayo ulizwa,jibu maswali yangu kisha nikujibu yako.

Hilo sharti nimelipata katika misingi ya lugha na matumizi ya tamko hilo na asili yake.

Hii kauli unatakiwa uithibitishe na kuonyesha ukweli wake,usitumie tamko "Labda" katika uhalisia.

Ok na ndio maana tulikua hatuelewani kumbe wewe umelichukua neno kiumbe kwa dhana ya kuumbwa na sio kiumbe kama kitu chochote kisicho maanisha kuumbwa

Mimi sizungumzii kiumbe kwa maana ya creation, nazungumzia kiumbe kwa maana ya living&non living things na ndio maana nasema hakuna kisicho kiumbe umeelewa??
 
Back
Top Bottom