Niseme ukweli, nikikutana na teacher yeyote anahangaika huwa simwonei huruma, kwasababu tangu nianze kusoma, maticha waliokuwa na upendo nikathibitisha wananipenda kama mtoto ninayewategemea wanifundishe, wachache sana.
Kuna ticha mmoja alinisaidia, alikuwa na moyo mwema, Mungu alishamwondoa siku moja nikakutana naye amekuwa Afisa Elimu wa Mkoa fulani hivi. inaonyesha watu wengi aliowafundisha kwa upendo ndo wamempigia mapande. Nilifurahi sana. Ukiwa na moyo mwema utafanikiwa, ukiwa mkatili wale unaowapiga ndo maboss wako au maboss wa watoto wako baadaye, utakutana nao tu.
Kuna siku nilichapwa na waalimu wengi fimbo hadi nilisahau idadi. siku hizi nakutana nao Mungu kanijalia maisha nimewazidi mbaliiiiiii, wanaishia kupunga mkono tu na kujichekelesha.