Athari za ukatili zinavyowatesa walimu

kipoma

JF-Expert Member
Aug 27, 2012
325
169
Habarini,

Moja kwa moja kwenye uzi.

Chanzo cha walimu kuwa kwenye maisha magumu na maslahi duni ni kutokana na ukatili wa walimu wa mwanzo kabisa waliofundishwa na wakoloni kwa ukatili, yaani fimbo sana, manyanyaso kwa wanafunzi wa wakati huo ambapo urithi wa ukatili umeendelea mpaka zama hizi.

Kwanini walimu wawe duni kimaisha ni kwa sababu mtu akipata madaraka hawezi kupigania maslahi ya mwalimu maana anakumbuka kuwa alifanyiwa vibaya hivyo hakuna haja ya kumpigania mtu hatari, ndiyo maana kada duni ni ualimu kwa level zote yaani walimu wa msingi mpaka vyuo vikuu ni hoi.

Hapa ukatili upo mwingi hata kutungiwa mitihani migumu, kufelishwa, kutopewa alama za halali kwenye mitihani na nk. Walimu badilikeni na jamii ibadilike ili viongozi wawakumbuke katika tawala zao.
 
Finally mtu amesemema kilichokuwa behind hearts
Niseme ukweli, nikikutana na teacher yeyote anahangaika huwa simwonei huruma, kwasababu tangu nianze kusoma, maticha waliokuwa na upendo nikathibitisha wananipenda kama mtoto ninayewategemea wanifundishe, wachache sana.

Kuna ticha mmoja alinisaidia, alikuwa na moyo mwema, Mungu alishamwondoa siku moja nikakutana naye amekuwa Afisa Elimu wa Mkoa fulani hivi. inaonyesha watu wengi aliowafundisha kwa upendo ndo wamempigia mapande. Nilifurahi sana. Ukiwa na moyo mwema utafanikiwa, ukiwa mkatili wale unaowapiga ndo maboss wako au maboss wa watoto wako baadaye, utakutana nao tu.

Kuna siku nilichapwa na waalimu wengi fimbo hadi nilisahau idadi. siku hizi nakutana nao Mungu kanijalia maisha nimewazidi mbaliiiiiii, wanaishia kupunga mkono tu na kujichekelesha.
 
Imagine, kuna shule moja juzi nililazimika kupeleka binti yangu bording, darasa la nne wanalazimisha wakae boarding. Mtoto wangu ana mwili mdogo nilimuwahisha na hana nguvu za kupigana, kitu cha kwanza nilikuwa naogopa bullying shule (mateso toka kwa wenzake), pili matron wao nilisikia anafinya sana watoto na kuwapiga mkwara wasitoe siri, na watoto wengi wanatii amri hiyo ukiwauliza wanakwambia hatuteswi.

Nimelazimika kumfuata huyo matron na kumtoolea ya moyoni kwamba mimi naleta mtoto wangu hapa, najua mnawatesa, wakwangu uwe naye makini bora uwe rafiki yangu kuliko kuwa adui yangu ukimtendea baya hata ukisema asije kusema atanambia tu (na ndivyo mwanangu alivyo), nimekuja siku nyingie mwisho wa mwezi kumwangalia, nimejihakikisha kwa vyanzo vya intelijensia yangu kuwa mtoto wangu amemuweka dabodeka ya chini tena karibu na pale anapolala yeye ili amwangalia kwa ukaribu zaidi, ikabidi niongee naye kiume tu sasa uyo matron (biinti kama wa 30 hivi), na kumpa hela ya chai walau fifty.

Nitakuwa nampa za chai kumtia moyo hivyohivyo sio kwasababu hela haiumi lakini nahangaika mtoto wangu asiteswe na kunyanyasika nafsi. mambo kama hayo ndiyo yanafanya mtu akija kufanikiwa akiangalia wale waliokuwa wanamtesa, hana hamu nao kabisa.
 
Kiukweli kuna issue ya kum-discipline mtoto ila kwa shule zetu hii kitu hamna ni kukomoana waalimu wanaofundisha na ku-discipline watoto bila kuwaumiza ni wachache sana huwa hawafiki robo ya walimu katika shule hasa hizi shule za sekondari.
Niliwahi kuchapwa fimbo zaidi ya ishirini za makalio kisa nili escape kuchapwa,
Imagine mwanafunzi anapigwa fimbo 30 at the same time anashindwa hadi kukaa,
Teachers wengine wanatoa adhabu za kukomoa, mtoto mdogo wa kike anaambiwa achimbe mtaro umfikie magotini worse enough hizi adhabu wanajua kabisa hazijawahi kupandisha ufaulu wanajua ni nini wanatakiwa wafanye ili mwanafunzi afaulu
But walimu kumbukeni kuwa hata kama unamwadhibu mtoto ukizidsha kiwango ikawa ni ukatili karma huwa haichezi mbali hata iweje.
 
kweli kabisa walimu hua wanajiona wamefika sana kwa jinsi wanavyokomoa wanafunzi
 
Leo watu wameamua kusema ukwel wao.

Walimu njoo muone mikosi mnayojikusanyia huko mashuleni
 
Kuhusu walimu,jamii tunatia chumvi nyingi sana.
Walimu wa sasa si wa miaka ile.
Wengi wana maisha mazuri tu.
Pia,ni wana mchango mzuri
katika jamii.
Binafsi,bila fimbo na adhabu
za walimu nisingefika hapa.
IKUMBUKWE;
Matoto ya leo,na Mazazi ya leo
yaliyo mengi ni mashenzi.
USHAURI;
Nashauri walimu,wawapige
hadi wazazi,ili tuwe na jamii
yenye adabu.
Serikali,ione namna ya kuwapatia walimu mafunzo ya kijeshi ili uwepo ufanisi.
 
Unajua mimi ni mwalimu

Walimu wana professional ambitions zao ikiwemo kuona wanafunzi wao wanafanya vizuri

Hamna mwalimu anaefundisha mwanafunzi wake akitazamia kuwa ashindwe na kesho aone mwanafunzi wake aliemfundisha ameishia kuwa kilaza (kangi). Mwl. huwa anajisikia vibaya sana

Na labda niwaambie huwezi kulipa fadhira ya nguvu anazotumia mwalimu kumfundisha na kumlea mwanao
Itoshe tu kusema mwalimu ametimiza wajibu wake na wewe useme asante

Serikali ndio inapaswa kuangalia maswala ya motisha wewe unapelekaje mwanao kwa mtu usie na mkataba nae?

Halafu huko private mbona mnalipa mamilioni na watoto wenu wanapata matokeo yaleyale yanayopatikana katani (public schools)?

Sisi walimu bhana serikali imetudharau sana lakini huduma yetu mnainunua private schools kwa pesa mingi na mmetulia wala hamfurukuti.
 
Back
Top Bottom