Athari za Majaji walioteuliwa na Hayati Magufuli

Mindi

JF-Expert Member
Apr 5, 2008
3,523
4,991
Tumewahi kusikia malalamiko kuhusu kada ya majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania. Malalamiko hayo, kwamba kuna majaji hawana viwango vya kiweledi vinavyotakiwa, yalitolewa bungeni, na mh. Tundu Lissu enzi hizo.

Nakumbuka Spika wa wakati huo, Anne Makinda, alikasirishwa sana na kauli hiyo ya Mh. Lissu, kwamba inadhalilisha majaji wetu, na akamtaka Lissu athibitishe au kufuta kauli yake. Lissu aliapa kuthibitisha. Kilichofuatia ni Lissu kuandika kitu unachoweza kuita ni Thesis, ilikuwa ni kali mno. Spika Makinda alipokabidhiwa wala hakuthubutu kumpa nafasi Lissu aiwasilishe bungeni. Ingeingia kwenye kumbukumbu za bunge ingekuwa aibu zaidi. Lissu kuona hivyo akaamua kushusha kitu kizima mitandaoni.

Lakini siku za karibuni kumetokea malalamiko zaidi kuhusu uhuru wa mhimili wa mahakama kwa ujumla, na kwa maana ya mada ya uzi huu, majaji walioteuliwa na Rais Magufuli , rais wa awamu ya 5.

Inaonekana majaji walioteuliwa na Rais huyu, licha ya matatizo ya weledi pengine kwa baadhi yao, lalamiko kubwa ni kwamba wana mtindo wakupendelea serikali, hasa kwa kesi za "watu wakorofi" kama kina Mbowe, CAG mstaafu Assad, nk.

Tuangalie jopo la majaji wa mahakama kuu walioamua kesi ya kupinga kuhojiwa prof. Assad na kamati ya bunge. Nina uhakika na wawili ambao ni wateule wa Rais Magufuli. Jaji Elinaza Luvanda, ambaye ndiye alikuwa jaji wa kwanza kusikiliza kesi ya kubumba ya "Ugaidi" dhidi ya Mh. Mbowe.

Jaji Luvanda anakumbukwa kwa maamuzi ya kustaajabisha juu ya mapingamizi ya Utetezi. Kwamba alikubali pingamizi moja kwamba hati ya mashitaka ina walakini, bado akaagiza washitakiwa warudi rumande na hati ya mashitaka irekebishwe!

Huyu ni mteule wa Magufuli na kwa kweli analipa fadhila.
Jaji wa pili, Yose Mlyambina. Namheshimu Jaji huyu, lakini ni kweli kwamba amekuwa wakili kwa muda mfupi sana. Wakati Shangazi Fatuma Karume anatuambia huko Uingereza, Jaji hanabudi awe ametumikia uwakili si chini ya miaka 20.

Nadhani sifa kuu iliyotumika kumteua Yose Mlyambina kuwa jaji, ni sababu moja tu. Ameoa binti wa Rais Magufuli (siye mtoto wa Janet). Yaani Jaji Yose anamwita Magufuli baba mkwe. Hiyo ndiyo ilimfanya apande haraka kufikia ujaji.

Sina taarifa za jaji wa tatu, lakini kwa hao wawili, ni hakika hakuna haki.

Majaji wateule wa Magufuli wanajitofautisha kwa kuwa watiifu kwa serikali, tena kama vile wamekula yamini. Majaji wa enzi za Nyerere, akina jaji Nyalali, walikuwa wengi wao ni wasimamizi wa haki. Hawasiti kuiadabisha hata serikali na mamlaka iliyowateua.

Akina jaji Barnabas Samatta, jaji Lugakingira, jaji Amiri Manento. Ilikuwa mihimili, Pillars of Justice. Kila mtanzania anaweza kujivunia miamba hiyo. Hawa wa Magufuli ni maumivu matupu.

Wanahitajika kuzomewa kwa nguvu zote, waache kuinajisi mahakama. Uwepo wao ni kuendeleza UMAGUFULI bila Magufuli .
 
Ina maana majaji wote wameteuliwa na Magufuli, au una chuki na Magufuli! Uamuzi unapotolewa na jopo la majaji ambao hata hawakuteuliwa na Magufuli, wewe unasema nini juu yao!
Soma vizuri uzi. Magufuli ameteua majaji, wengi kawakuta. Nazungumzia wale aliowateua. Majaji wapumbavu wapo tu, hata enzi za Nyerere walikuwepo. Lakini Hawa wa Magufuli wametia fora
 
Ina maana majaji wote wameteuliwa na Magufuli, au una chuki na Magufuli! Uamuzi unapotolewa na jopo la majaji ambao hata hawakuteuliwa na Magufuli, wewe unasema nini juu yao!
😍😍😍😍😍😍kuna watu wasiotaka kuumiza vichwa kufikiri. Hivyo, hutafuta njia za mkato na rahisi kwa kutoa hitimisho jumuishi wasijue madhara yake. Angejua sheria, asingesema haya yote anayosema.
 
Ni aibu sana sana sana....majqjo wa kulipa fadhila hawa Luvanda. Sasa Siyayi huyo kazi kubwa sana amepewa JK hawezi kukataa hongo kubwa hiyo sababu ya Haki yaani dhambi kubwa sana haitamuacha milele
 
Mzimu unakutesa kudadeki. Badala ya kuongelea jaji mwenyewe. Umeona hadi utaje marehemu.

Hatari sana.
 
Umechemka kwenye utawala wa Magufuli Spika hakuwa Anna Makinda
Hujasoma vizuri. Kauli ya Tundu Lissu aliitoa enzi za Spika Makinda. Fast Forward awamu ya Magufuli , niakaongelea teuzi zake za majaji
 
Kwanini walioteuliwa na Magufuli hsiwafananishe na wa Kikwete, Mkapa na Mwinyi!

Why Magufuli vs Nyerere?

Kwamba walioteuliwa na hao watatu wanatenda haki? au hao watatu hawakuteua!
 
Mzimu unakutesa kudadeki. Badala ya kuongelea jaji mwenyewe. Umeona hadi utaje marehemu.

Hatari sana.
Kwa nafasi yake ya urais, Magufuli ataongelewa sana tu, awe hai au marhum. Mbona Nyerere anaongelewa sana tu? Mnataka kumficha Magu tusiongelee madudu yake kisa marhum? Hiyo haipo.
 
23 Reactions
Reply
Back
Top Bottom