ATCL yaanza kukata tiketi kwenda India

esther mashiker

JF-Expert Member
May 29, 2018
616
552
1100582

SAFARI ya kwanza ndege za Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL) kwenda Mumbai, India itazinduliwa Julai 17, mwaka huu huku dirisha la kukata tiketi kwa safari hizo tayari limefunguliwa rasmi.

Akizungumza na gazeti hili jana, Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Ladislaus Matindi alisema hatua hiyo ni mafanikio ya Mpango Mkakati wao ulioanza mwaka 2017, waliojiwekea kuhakikisha shirika hilo linapata mafanikio kwenye usari wa anga kwa kufungua vituo vingi vya biashara nje ya nchi.

Matindi alisema kwa sasa wamefungua rasmi dirisha la kukata tiketi kwa safari za Mumbai, India, ambapo wasari wanaweza kununua tiketi hizo kupitia mtandao wa shirika hilo, kwa mawakala wa ndege na pia wanaweza kufanya malipo kwa kutumia kadi za benki, Mpesa au Tigopesa na kulipa papo hapo wakati wa kununua tiketi dirishani.

Awali, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa ATCL, Josephat Kagirwa alisema bei za kuanzia zitakuwa kati ya Dola za Marekani 286 hadi 460 kwa ruti moja, ambapo kwa fedha ya nchini safari ya kwenda na kurudi kwa daraja la kawaida itakuwa Sh milioni 1.4. Aidha kwa daraja la juu safari ya kwenda na kurudi, itakuwa Sh milioni 4.3 na kwamba bei hiyo ni nafuu ukilinganisha na bei za kampuni nyingine za ndege kwenda safari kama hiyo.

“Tumeamua kuanzia na bei hiyo ya promosheni kwa muda kama njia ya kuitangaza ndege yetu ya Boeing 787-8 Dreamliner yenye uwezo wa kubeba abiria 282,” alisema Kagirwa. Alisema ndege hiyo ya Dreamliner itakuwa ikifanya safari hizo mara tatu kwa wiki na kwamba maandalizi yake yamekamilika.

Wakati huo huo, Matindi alizungumzia kuzinduliwa kwa safari za kwenda Afrika Kusini katika Jiji la Johannesburg na kusema Juni 28, mwaka huu, watazindua safari katika jiji hilo ambapo nauli ya kwenda na kurudi itakuwa Dola za Marekani 300 takribani Sh 700,000. Alisema safari katika ruti hiyo itahusisha ndege mpya za Air Bus A220-300 na kwamba uzinduzi wa tiketi kwa ajili ya safari hizo, umefunguliwa rasmi na kuwataka wananchi na wasari kutumia fursa hiyo kupanda ndege hizo mpya.
 
Aiseee nauli iko vizuri natumai wengi watapendezwa na huduma ili wawe wateja wa kujirudia
 
Mnaipeleka wenyewe kwa kina manji!!!!

Msije kutupuliza makofi tukiwa tunacheka mkidhani tunawajoki!!!
 
Habari mbaya sana hii kwa chadema
Halafu Tundu Lissu siku hizi mbona hasikiki au maneno yamemuishia?
 
Lipia halafu safari inakuwa cancelled, sasa kudai hela yako hapo! Utaambiwa hela yote ishaenda kulipia deni la matibabu ya Ndugai.
Umenikumbusha lile basi kwenye miaka ya themanini au tisini. Lilikatisha tickets za kwenda Bukoba wakati wa noel halafu wakasepa. Bijampola liliitwa au?? Mwenye kumbukumbu anisaidie. Subiri Any Time Cancellation.
 
Back
Top Bottom