Askofu Thomas Laizer: "Uchaguzi wa Meya Arusha Urudiwe"

Askofu Thomas Laizer: "Uchaguzi wa Meya Arusha Urudiwe"

mbona maasikofu wakiongea ina make headlines kwenu...hawampi mtu amri wanashauri tu....mbona masheikh wanongea kila siku na wala haiwi discussion material ....umenielewa lakini????
maaskofu ni viongozi wa dini kama wengine...hawana dola .,...ushauri wao sio amri labda mtu aichuukulie hivo!!

nyerere alichakufa miakainazidi kumi...rais sasa ni Kikwete ....ni aibu kama tutaangalia utendaji wake kwa kuangalia dini yake ...uangaliwe uwezo wake binafsi ...dini yake haihusu ...na wala isichajize kupingwa au kutetewa!



Sawa nyerere alikufa zamani but he is somehow responsible for the disease we have it now kataa ukubali. Muslims have long been silenced their voices not heard, they were being considered outcasted, people known as "Waswahili" kumaanisha hawajasoma. Purposely kuwafanya wasione wala kugundua haki zao za msingi. Sasa JK anajaribu kuleta uwiano mnaanza kumuandama na visababu vya kijinga mkijua kuna maovu mmeyaficha THE SLEEPING GIANT IS AWAKENING
 
Hizi ndio mentality zenu kudhani wakristo mpo wengi tanzania endeleeni kuota tu. Jiulizeni kwanini Nyerere alikataa sensa ya dini Tanzania alifahamu fika waislamu ni wengi na hilo lingelikuja kumpa tabu kuitawala Tanzania. Sasa kwani mwaka huu si mlimsusia kutompigia kura JK mbona amepata asilimia 60% jiulizeni zimetoka wapi? Kaa ukitafakari ndugu sijidanganyi bali nakuzindueni baadhi yenu mliolala.
Mi mkuu sitaki kukuelewesha maana kwanza umetoka nje ya mada halafu umebadilisha topic imekua ya kidini.....kwa hiyo unataka kutuchafua waislamu kwamba tunaunga mkono mauaji ya arusha?? Kama wewe unaunga mkono usiseme waislamu wala dini fulani kaa na umbumbu wako.
 
Nishakuambia mie sijasoma elimu za madrassa na niko makini kariri maneno yangu sizungumzi kama baadhi ya watu hapa.

Ukitaka reference naanza na hiyo:-

Kama huwezi kubonye kitufe nanukuu:-

Religions:
mainland - Christian 30%, Muslim 35%, indigenous beliefs 35%; Zanzibar - more than 99% Muslim


https://www.cia.gov/library/publications/the-world-factbook/geos/tz.html


Wewe unafanya mtandao wa kijasusi wa marekani kuwa reference..umepitwa ...kwenye CIA pages huweka taarifa kutokana na malengo yao ya wakati husika ....shangaa taarifa ambazo zipo hadi kwenye congress na white house ni hizi:- achaana na wamarekani...wewe amini tu kuwa hakuna taarifa rasmi...

The study of the United States Bureau of Democracy, Human Rights, and Labor for 2009 suggests that 62% of the population of Tanzania is Christian, 35% is Muslim, and 3% are members of other religious groups.[2]
 
Sawa nyerere alikufa zamani but he is somehow responsible for the disease we have it now kataa ukubali. Muslims have long been silenced their voices not heard, they were being considered outcasted, people known as "Waswahili" kumaanisha hawajasoma. Purposely kuwafanya wasione wala kugundua haki zao za msingi. Sasa JK anajaribu kuleta uwiano mnaanza kumuandama na visababu vya kijinga mkijua kuna maovu mmeyaficha THE SLEEPING GIANT IS AWAKENING

sipendi tabia hii mtu akikosea kwenye kazi ...anatetewa kwa misingi ya udini .....

kwani tunapoongelea inflation tumeongelea dini ya mtu ...kwani ni uwongo kuwa gharama za maisha zinapaa...kwani wewe unalipa umeme tofauti na mimi>?

kwani wewe unapenda serikali iwalipe DOWANS bilioni 96...tunapinga mambo ya msingi na hakuna aliyeongeelea diini ya mtu!!!....sasa kaama tutawatetea viongozi kwakuwa ni dini au kabila zetu waatakuwa na kiburi !!
 
Hizi ndio mentality zenu kudhani wakristo mpo wengi tanzania endeleeni kuota tu. Jiulizeni kwanini Nyerere alikataa sensa ya dini Tanzania alifahamu fika waislamu ni wengi na hilo lingelikuja kumpa tabu kuitawala Tanzania. Sasa kwani mwaka huu si mlimsusia kutompigia kura JK mbona amepata asilimia 60% jiulizeni zimetoka wapi? Kaa ukitafakari ndugu sijidanganyi bali nakuzindueni baadhi yenu mliolala.

Duh we jamaa sikujua ni kilaza kiasi hiki.Unajenga hoja kwa imagination za ajabu kweli.Its shame kuropoka kwamba kikwete kapigiwa kura na waislamu tu, thats quite empty argument.Second ni asilimia ngapi ya watanzania walipiga kura? Do your homework before spiting crap here.. unajishushia heshima.
 
Heshima isivuke mipaka ya sheria. Nchi inaongozwa na mihimili mikuu mitatu, MAHAKAMA, SERIKALI NA BUNGE. Nikuulize Askofu anamamlaka gani ya kuicommand serikali????

Kwanza nirudie kusema hakui-comand serikali, HAYO NI MAWAZO YAKE AU MAPENDEKEZO YAKE. Pili, mihimili ya serikali haindoi wadau nchini, wala haina maana kuwa asiyekuwa sehemu ya serikali, mahakama, au bunge asichangie mawazo yake kwenye mustakabali wa taifa. Nomba nikuulize mkuu. Kuheshimu viongozi wa dini kunavukaje mipaka ya sheria? Je Askofu amevunja sheria gani kwa kusema aliyoyasema? Na je kama viongozi wa dini hawatambuliwi au hawana sehemu katika maswala ya taifa, ni kwa nini huitwa kuombea taifa nyakati za kuwakumbuka mashujaa wa taifa au nyakati za majanga?
 
Siasa yetu sijui inachukua uso gani kwa sasa. Hadi makanisa ni CHADEMA?

Makanisa ni nyumba tu. ikiwa bila watu itaitwa gofu. kuingia kanisani au msikitini, kuwa askofu au sheikh hakumuondolei uraia wake. na kazi kubwa na namba moja ya raia yeyote ni kutumikia taifa lake kwa haki na kweli. Laizer ametimiza wajibu wake kama raia kutoa rai haki itendeke ila kudumisha tunu ya amani nchini. Ni vyema ukajua amani haipatikana kwa maneno ya majukwaani ama mabavu ya vyombo vya dola, reje historia duniani kote hamna palipokuwa na amani isipokuwa ni kwa kutenda haki. AMANI NI ZAO LA HAKI. ukicheza na haki za raia, lazima upate mrejesho wa machafuko. Think big
 
United StatesBureau of Democracy, Human Rights, and Labor2009

Muslim communities are concentrated in coastal areas, with some large Muslim minorities also in inland urban areas.[1] Between 80 and 90 percent of the country's Muslim population is Sunni; the remainder consists of several Shi'a subgroups, mostly of Asian descent.[1]
The Christian population is composed of Roman Catholics, Protestants, Pentecostals, New Apostolic Christians, Seventh-day Adventists, members of the Church of Jesus Christ of Latter-day Saints (Mormons), and members of Jehovah's Witnesses.[1]
The Baha'i Faith is established in several hundred localities throughout the country.
 
Jibu swali kwanini Nyerere alikataa Sensa ya dini? Tizama kinachoendelea Ivory coast na Nigeria. For your information I may be more educated than you.

hata Kandahar kuna chuo kikuu
 
wenye busara huona na kusema yao then hukaa kimya ila wapumbavu huropoka na kutaka kuuona mwisho wa ubishi wao ambapo maranyingi huwa ni fedhea
 
sipendi tabia hii mtu akikosea kwenye kazi ...anatetewa kwa misingi ya udini .....

kwani tunapoongelea inflation tumeongelea dini ya mtu ...kwani ni uwongo kuwa gharama za maisha zinapaa...kwani wewe unalipa umeme tofauti na mimi>?

kwani wewe unapenda serikali iwalipe DOWANS bilioni 96...tunapinga mambo ya msingi na hakuna aliyeongeelea diini ya mtu!!!....sasa kaama tutawatetea viongozi kwakuwa ni dini au kabila zetu waatakuwa na kiburi !!

Labda yeye yuko tofauti na sisi maana inabidi nimshangae sana kama haya uliyoyaandika hatakuwa hajaelewa hata moja kwa kuwa ameng'ang'ania udini ugumu wa maisha, kupanda kwa bei ya umeme, DOWANS kutaka kulipwa hilo halioni na haoni kuwa tunapinga mambo ya msingi hapa rather than talking UDINI
 
Source ITV:

Taarifa ya saa 2 usiku.

Baba Askofu
Tanzania inaongozwa na sheria na utaratibu. Wazo lako liwasilishwe MAHAKAMANI chombo pekee chenye uwezo wa kuamrisha uchaguzi urudiwe. Waombe waumini wako wakafungue kesi mahakamani. Matamshi ya uchaguzi urudiwe yanayotolewa katika jukwaa za kisiasa ni matamshi ya kisiasa na hayatasaidia kutatua tatizo lililopo. Matamshi haya ya kisiasa yanaweza kukuweka wewe Baba Askofu katika Chama cha siasa au siasa za vyama wakati wewe ni baba mlezi wa wananchi wote Tanzania. Kwa nafasi yako Baba Askofu unaweza kuwashauri watanzania watumie Mahakama zetu. Na ni vyema kuwahi Mahakamani wakati kumbukumbu za watu bado ni kubwa.
 
MSIBA WA MASHUJAA: CHADEMA wailiza Arusha
• Mbowe atoa tamko zito, ahamasisha maandamano nchi nzima

na Waandishi wetu


amka2.gif
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), jana kililiteka tena Jiji la Arusha katika ibada, maandamano na mazishi ya mashujaa wake, ambayo yalifanyika kwa amani bila ulinzi wowote wa polisi.
Polisi pekee waliooekana ni wale tu wa usalama barabarani. Barabara kadhaa za jiji la Arusha zilifungwa, na maelfu ya wananchi walitanda kando ya barabara hizo, kushuhudia msafara wa miili ya marehemu ikitoka chumba cha maiti kuelekea viwanja vya NMC, na baadaye kuelekea eneo la mazishi, USA River alikozikwa Ismaili Omar. Mmoja wa marehemu hao, Denis Michael, atazikwa leo Rombo, mkoani Kilimanjaro.
Mashujaa hao waliuawa na polisi waliokuwa wanapambana na wafuasi na viongozi wa CHADEMA katika kuzuia maandamano na mkutano wa hadhara uliopangwa kufanyika viwanja vya NMC, Januari 5, mwaka huu, kudai marudio ya uchaguzi wa meya wa Jiji la Arusha na naibu wake.
Zizi la Arusha lilizizima kwa maelfu ya wananchi waliojitokeza kwa kishindo katika ibada maalum ya kuaga miili ya marehemu hao.
Katika ibada hiyo, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, alitoa tamko zito lililolaani vikali mauaji hayo, huku akitangaza maandamano mapya yatakayofanywa na chama hicho nchi nzima yakibeba madai kuu nane likiwamo la kutaka kuitishwe mkutano wa kitaifa utakaofanikisha kuandikwa kwa katiba mpya.
Katika madai hayo, Mbowe alitangaza msimamo mkali wa kutaka mashitaka yote yaliyofunguliwa dhidi ya viongozi wa ngazi zote wa chama hicho - wanachama, wafuasi na wananchi wengine wote waliokumbwa na kumba kumba ya Jeshi la Polisi - yafutwe bila masharti yoyote, vinginevyo hawatahudhuria mahakamani tena, hata kama kwa kufanya hivyo kutafanya wakamatwe na kurudishwa tena gerezani.
"Tunasisitiza katika jambo hili kwamba viongozi, wanachama na wafuasi wetu wote waliokamatwa na kufunguliwa mashtaka haya hawatahudhuria mahakamani tena kuhusiana na kesi iliyofunguliwa dhidi yao, hata kama kwa kufanya hivyo kutafanya wakamatwe na kurudishwa tena gerezani," alisema Mbowe.
Alitaka kuundwe tume huru ya uchunguzi ya kimahakama (Judicial Commission of Inquiry) itakayoongozwa na majaji wa Mahakama ya Rufani ili ifanye uchunguzi huru, wa kina na wa wazi wa matukio yote yaliyosababisha IGP Mwema kupiga marufuku maandamano ya amani na mkutano wa hadhara kabla ya Jeshi la Polisi kufanya vurugu zilizosababisha mauaji ya wananchi wasiokuwa na hatia.
Dai lingine ni kutaka Waziri wa Mambo ya Nchi Shamsa Vuai Nahodha na Inspekta Jenerali wa Polisi Saidi Mwema wawajibike wajiuzulu. nia.
"Kujiuzulu kwao kutapisha uchunguzi huru na wa kina wa matukio yote yaliyosababisha wananchi wetu kuuawa, mamia kujeruhiwa na mamia mengine kukamatwa bila sababu yoyote na kuwekwa rumande na baadaye kufunguliwa mashtaka ya uongo ya jinai," alifafanua na kuongeza:
"IGP Mwema, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha Andengenye na wale wote walioamuru au kutekeleza amri ya kuvunja maandamano na mkutano halali wafunguliwe mashtaka ya jinai kwa matumizi mabaya ya madaraka na kwa kusababisha mauaji ya wananchi wasiokuwa na hatia."

Mbowe, ambaye pia ni kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni, aliitaka serikali kuwalipa fidia stahili kwa mujibu wa sheria husika za nchi ndugu na jamaa wa wale wote waliouawa kutokana na vitendo vya polisi na wale wote walioumizwa kwa namna yoyote ile na au kuharibiwa mali zao kutokana na vitendo hivyo.
Pia alisema chama hicho kinataka matokeo ya uchaguzi wa viongozi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha yafutiliwe mbali, na uchaguzi mpya uitishwe haraka iwezekanavyo, kwani uchaguzi huo ndio chanzo cha mauaji ya wananchi.
"Sheria ziweke wazi wajibu wa Jeshi la Polisi la Tanzania kulinda maandamano ya amani na mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa na/au ya wananchi," alisema.
Katika kuhakikisha kwamba madai ya chama hicho yanatekelezwa, alisema chama kimeelekeza viongozi, wanachama na wafuasi wake mikoani na wilayani kuandaa maandamano ya amani nchi nzima ili kulaani mauaji ya wananchi wa Arusha na kudai utekelezaji wa madai hayo.
"CHADEMA Makao Makuu itatuma maafisa wa ngazi za juu wa chama, wakiwemo wabunge na wajumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA kushiriki katika maandamano hayo kwa ngazi za mikoa na wilaya ili kuyaongezea nguvu na hamasa," alisisitiza Mbowe.
Alimhusisha pia Rais Kikwete, serikali yake na chama chake, akisema waliandaa mazingira ya damu iliyomwagwa Arusha, kwani kwa mujibu wa Katiba, yeye ndiye Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi yote ya ulinzi na usalama, na pia ndiye aliyewateua IGP Mwema na waziri Nahodha waliosababisha mauaji hayo. Alisema Rais Kikwete pia alitoa kauli tete katika hotuba yake ya kufunga mwaka 2010, ambayo ilihamasisha polisi kujipendekeza kwa CCM kwa kuzuia kazi za kisiasa za CHADEMA.
Katika ibada hiyo, maaskofu wa madhehebu ya Kikristu mkoani Arusha walimkemea Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Yusuph Makamba, kwa kuitumia Biblia takatifu kuhalalisha uovu; wakamtaka aache tabia hiyo mara moja.
Huku wakimlinganisha na viongozi mbalimbali wanaotajwa kwenye Biblia waliokuwa wakifanya hivyo kulinda uovu wao, maaskofu hao wakiongozwa na Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati, Thomas Laizer, aliyezungumza kwa niaba wenzake, walisisitiza kwamba wataendelea "kuikosoa serikali na chama chochote kile pindi kinapokosea."
Kauli ya Makamba iliyowakera maaskofu hao, na ambayo amekuwa akiirudia mara kwa mara, ni ile aliyotumia kuwakejeli kwa kunukuu maandiko matakatifu ya Kurani na Biblia akisema "tiini mamlaka iliyo kuu." Walisema ufahamu wa Makamba ni finyu katika kutafsiri maana halisi ya neno hilo.
Askofu huyo alisema kazi ya viongozi wa dini ni kukosoa maovu kwenye jamii. Alisema wataendelea kufanya hivyo kila inapowabidi bila kujali ni nani au chama gani kimekosea, kwani kazi ya manabii tangu enzi za Biblia ilikuwa pia kuiongoza jamii katika njia nyoofu.
"Kama serikali wameamua kutuvunjia heshima, basi wasimame kwenye majukwaaa kutetea uovu wao, na sisi tutasimama kwa ajili ya kupinga uovu wao, tuone Mungu atamsikia nani. Sisi tunataka uchaguzi wa meya na naibu wake urudiwe, apatikane kiongozi halali bila kuangalia atachaguliwa kutoka chama gani, " alisema Askofu Laizer.
Kiongozi huyo wa kiroho alielezea kukubaliana na kauli za viongozi mbalimbali zilizotolewa kwa ajili ya kulipatia ufumbuzi suala hilo, huku akipingana na ile ya Makamba na Katibu wa CCM mkoa wa Arusha, Mary Chatanda wanaosisitiza kuwa meya wa jiji hilo alipatikana kihalali na kwa kufuata sheria, na kwamba suala hilo likapingwe mahakamani.
Alisema tabia ya Makamba kurudia lugha hizo mara kwa mara imemuambukiza kwa Chatanda ambaye aliwakejeli maaskofu akitaja wavue majoho na wamfuate kupambana katika uwanja wa siasa, hali ambayo amesema ni kuwakosea nidhamu.
''Maaskofu wamesikitishwa na kauli yake na pia kauli ya Katibu wa CCM mkoa wa Arusha, Mary Chatanda kuwataka kuvua majoho na kuingia katika siasa kwani ni kuwavunjia heshima,'' alisema askofu Laizer.
Katika ibada hiyo, Sheikh Alawi, akisoma dua, alitangaza rasmi kuwa marehemu hao Omar Ismail na Denis Shirima wamefariki kishujaa.
Mbali na Mbowe, mazishi hayo yalihudhuriwa pia na Katibu Mkuu, Dk. Willibrod Slaa, muasisi wa chama hicho, Edwin Mtei, na wabunge zaidi ya 18, wakiwamo, Godbless Lema John Mnyika (Ubungo), Halima Mdee (Kawe), Joyce Mukya (Viti Maalumu), Mustafa Akoonay (Mbulu), Philemon Ndesamburo (Moshi Mjini), Lucy Owenya (Viti Maalumu), Susan Kiwanga (Viti Maalumu), Anna Komu (Viti Maalumu), Tundu Lissu (Singida Kaskazini), Susan Lyimo (Viti Maalumu), Pauline Gekul (Viti Maalumu).
Nayo mashirika 50 yanayotetea Usawa wa Kijinsia, Haki za Binadamu, Maendeleo na Ukombozi wa Wanawake Kimapinduzi (FemAct), yamelaani ukiukwaji wa haki za binadamu, demokrasia na uvunjivu wa amani uliosababisha kuumizwa na mauaji ya raia wasiokuwa na hatia mjini Arusha.
Katika taarifa iliyotolewa jana kusainiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Usu Mallya, wanaharakati kutoka mashirika hayo walisema:
"Vurugu hizo ziliendana na unyanyasaji na udhalilishaji wa kijinsia kwa baadhi ya waandamanaji, huu ni ukiukwaji wa haki za msingi za kibinadamu na za wanawake…

"FemAct inalaani kitendo cha halmashauri ya Jiji la Arusha kusimamia na kuendesha uchaguzi batili usiozingatia sheria kanuni na taratibu za uchaguzi ambao ulimpata Meya na Naibu wake 18/12/,2010 na kumpelekea kutokea kwa vurugu hizo.
"FemAct tunalaani kwa nguvu zetu zote ubabe na matumizi mabaya ya vyombo vya dola, hasa Jeshi la Polisi ambacho ni chombo cha ulinzi na usalama wa wananchi kugeuka na kuvunja sheria ya kuwazuia wananchi kutoa sauti zao na kupigania haki zao za msingi…
"Sisi wanaharakati tunalitaka jeshi la Polisi na serikali kuweka wazi muktadha na hali halisi ya tukio la Arusha, kuwataja na kuwachukulia hatua za kisheria walioshiriki kuvunja sheria na kutoa idadi kamili ya wananchi waliojeruhiwa na kupoteza maisha katika tukio hilo."
Waliitaka serikali kuunda tume huru itakayowashirikisha wananchi, plisi, vyama vya siasa, wanaharakati na watetezi wa haki za binadamu kushughulikia suala hili na kuwahakikishia wananchi wa Arusha kuwa tukio kama hili halitatokea tena.
"Tunaitaka serikali,vyama vya siasa na vyombo vya dola kutokuwanyamazisha wananchi, viongozi wa kijamii na dini wanaolizungumzia suala la Arusha kwani hivyo ni kinyume na demokrasia iliyoendelea na kukomaa nchini."
 
wenye busara huona na kusema yao then hukaa kimya ila wapumbavu huropoka na kutaka kuuona mwisho wa ubishi wao ambapo maranyingi huwa ni fedhea


maneno makali haya lakini sijakusoma bado
 
Mi mkuu sitaki kukuelewesha maana kwanza umetoka nje ya mada halafu umebadilisha topic imekua ya kidini.....kwa hiyo unataka kutuchafua waislamu kwamba tunaunga mkono mauaji ya arusha?? Kama wewe unaunga mkono usiseme waislamu wala dini fulani kaa na umbumbu wako.

Mie siuingi mkono mauaji ya arusha na vilevile siungi mkono biashara ya maaskofu kuicommand serikali ni jambo lapaswa kukemewa kwa nguvu zote
 
Wewe unafanya mtandao wa kijasusi wa marekani kuwa reference..umepitwa ...kwenye CIA pages huweka taarifa kutokana na malengo yao ya wakati husika ....shangaa taarifa ambazo zipo hadi kwenye congress na white house ni hizi:- achaana na wamarekani...wewe amini tu kuwa hakuna taarifa rasmi...

The study of the United States Bureau of Democracy, Human Rights, and Labor for 2009 suggests that 62% of the population of Tanzania is Christian, 35% is Muslim, and 3% are members of other religious groups.[2]

So bwana Philemon nikuulize swali moja CIA fact book US Human rights watch nani wanaagenda ya siri? CIA ni goverment institution na ukienda katika US department of state wanasema hivi:-

The country has an area of 364,900 square miles and a population of 37 million, of which 36 million live on the mainland and 1 million on the Zanzibar archipelago. Current statistics on religious demography are unavailable because religious surveys were eliminated from government census reports after 1967. Religious leaders and sociologists estimate that the Christian and Muslim communities are equal, each accounting for 30 to 40 percent of the population, with the remainder consisting of practitioners of other faiths and indigenous religions, and atheists .

Reference zaidi hiyo:-

Tanzania

Nilipofatilia waliofanya study nikakuta ni Christian institution mmoja ambayo iko marekani sasa unajiuliza kwanini wamepata 60% jibu nadhani umelipata. na kama umesoma US department yenyewe wameshindwa kusema hii ni conclusive wameestimate rather than an actual figure. Kama maneno yako uliyoyanukuu haya:-

The country has an area of 364,900 square miles and a population of 40 million, of which 38.8 million live on the mainland and 1.2 million on the Zanzibar archipelago, which has a president and semiautonomous political structure separate from the mainland political system. The Government does not gather religious identification data in its census as a matter of policy. However, recent information suggests that 62 percent of the population is Christian, 35 percent is Muslim, and 3 percent are members of other religious groups.

NIKUULIZE SASA KWANINI SERIKALI INAOGOPA KUFANYA STUDY YA DINI!!!! NAOMBA JIBU
 
sipendi tabia hii mtu akikosea kwenye kazi ...anatetewa kwa misingi ya udini .....

kwani tunapoongelea inflation tumeongelea dini ya mtu ...kwani ni uwongo kuwa gharama za maisha zinapaa...kwani wewe unalipa umeme tofauti na mimi>?

kwani wewe unapenda serikali iwalipe DOWANS bilioni 96...tunapinga mambo ya msingi na hakuna aliyeongeelea diini ya mtu!!!....sasa kaama tutawatetea viongozi kwakuwa ni dini au kabila zetu waatakuwa na kiburi !!

Inflation na kucommand serikali wapi na wapi ndugu? Mie sikubaliani na ufisadi kamwe ndio maana nabakia sina chama na siwaungi mkono Chadema kwasababu nawajua wabaguzi hivyo basi tafadhali sana usinitengenezee picha isiyo yangu.
 
Duh we jamaa sikujua ni kilaza kiasi hiki.Unajenga hoja kwa imagination za ajabu kweli.Its shame kuropoka kwamba kikwete kapigiwa kura na waislamu tu, thats quite empty argument.Second ni asilimia ngapi ya watanzania walipiga kura? Do your homework before spiting crap here.. unajishushia heshima.

Mgalanjuka,

Mie spit tu bali najenga arguments na ndio maana natoa argument zengine hapa watu wengine wanakimbia. Mie nimeuliza a solid question kwanini mnamuandama JK ukiondoa ufisadi Jakaya Kikwete amejitahidi na mie hapo nampongeza. Ila kwakuwa nyie na chuki zenu dhidi ya Kikwete mnaropoka ropoka vitu visivyo na maana. Mnasupport a religous institution kuwalazimisha serikali iwafuate mnadhani mnatengeneza taswira gani Tanzania. Who the hell are maaskofu in Tanzania governance?!!! Think big ndugu.
 
Back
Top Bottom