Askofu Mwamakula: Sisi viongozi wa dini tumesitisha safari ya kwenda Mbweni na kwenda kumuona IGP Sirro!

BAADA YA WANAWAKE WA CHADEMA KUACHIWA, SISI VIONGOZI WA DINI TUMESITISHA SAFARI YA KWENDA MBWENI NA KWENDA KUMUONA IGP SIRRO!

Jumapili tulitangaza kuwa kama siku ya Jumatatu Jeshi la Polisi lisingeliwaachia viongozi wa CHADEMA 7 na Waandishi wa Habari 2 waliokuwa
Good
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Acha uwongo wako, mtu mzima ovyoo sana wenzenu kina maria sarungi wana tengeneza michuzi hawa sura zimewapa ukaa jua!
msidanganyike
Eeeen Heeee Heeeee! Wacha nicheke!

Eti umeandika nini? Mbona unamatatizo makubwa ya kueleza unachotaka kukieleza watu wakuelewe!

Kwa hiyo unapomsoma Maria Sarungi unaelewa anachoandika, au ndio hivi kama ulivyoonyesha uwezo mdogo sana wa kuelewa nilichoandika mimi!

Kiufupi ni kwamba huna uwezo wa kuelewa chochote. Hata huyo Maria hujui anaeleza kitu gani katika maandishi yake.

Akina mama hao wa CHADEMA wameweka alama, wewe utabaki unashobokea tu usiyoyaelewa.
 
BAADA YA WANAWAKE WA CHADEMA KUACHIWA, SISI VIONGOZI WA DINI TUMESITISHA SAFARI YA KWENDA MBWENI NA KWENDA KUMUONA IGP SIRRO!

Jumapili tulitangaza kuwa kama siku ya Jumatatu Jeshi la Polisi lisingeliwaachia viongozi wa CHADEMA 7 na Waandishi wa Habari 2 waliokuwa wanashikiliwa katika Kituo cha Polisi Mbweni - Dar es Salaam, sisi Askofu Mwamakula pamoja na viongozi wengine wa dini tungelifika kituoni hapo siku ya Jumanne kwa ajili ya kuwaona. Baadaye tungeliujulisha umma na dunia kwa ujumla.

Baada ya azimio letu, Viongozi wa Dini kupitia Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Maaskofu na Mashehe kuhusu Maadili, Amani na Haki, Askofu William Mwamalanga walitoa tamko kutuunga mkono na kuahidi kuungana pamoja nasi kwenda Mbweni na pia kumuona IGP Simon Sirro. Usiku wa Jumatatu tumepewa taarifa kuwa viongozi hao waliachiwa wote Jumatatu jioni.

Baada ya taarifa hiyo, sisi Askofu Mwamakula tunatangaza kusitisha safari yetu pamoja na viongozi wa dini tuliyopanga kwenda Kituo cha Polisi Mbweni siku ya Jumanne. Tunatangaza pia kuahirisha safari ya kumuona IGP Sirro. Tutashauriana kuhusu kupanga siku nyingine ya kuonana na IGP Sirro kuhusiana na mambo yanayoendelea nchini yakiwemo ya kunyanyasa wanaharakati na wanasiasa wa upinzani kunakofanywa na Jeshi la Polisi.

Tunapenda kuwashukuru wote walioshiriki kusambaza ujumbe wetu, walioshiriki kupaza sauti kwa njia mbalimbali na waliokuwa tayari kutuunga mkono kwa kutaka kutusindikiza sisi viongozi wa dini. Pamoja na kutiwa moyo na hatua ya Jeshi la Polisi kutokana na kusikia kelele za umma na kuamua kuwaachia, tunaendelea kutoa wito kwa Jeshi la Polisi kutokuwasumbua kwa lo lote viongozi hao kuhusiana na kukamatwa kwao.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula

View attachment 1963149
Ndiyo walikuwa wajogi na madela hayo🤣
 
Back
Top Bottom