Askofu Mwamakula: Polepole ametahadharisha tusipokuwa makini, Serikali inaweza 'kutekwa nyara' na kubaki kama 'mwanasesere'

Humphrey Polepole ameanza kujenga taasisi huru ya fikra! Hahitaji kiwanja cha kujengea taasisi hiyo wala hahitaji Wajumbe wa Bodi wa kuendesha kwani kichwa chake ndio Bodi yenyewe...
Huyu anayejiita askofu anapitisha hoja yake kwa mgongo wa Polepole, Anajua yeye watanzania wameshaamua kumpuuza. Hatari sana
 
Polpole si ndiyo huyu anatembea na makahaba,hivyo hawezi kuwa timamu.mwacheni abwatuke akitaka msaada atatuamsha hata saa tisa usiku tumsaidie.
 
Upuuzeni huyo "Polepole"! Muda wake umekwisha. Awaache waliopo madarakani wafanye kazi.
 
Mzee wa v eighty kabanwa mithili ya mjusi kwenye mlango. Apandae ngazi hushuka. Uliipigania katiba mpya baadae ukapiga abouturn. ..ulijua Meko ataishi milele? Ulituaminisha huwezi kaa chama kimoja na Mzee Lowassa, leo uko nae! Poleeee
 
Humphrey Polepole ameanza kujenga taasisi huru ya fikra! Hahitaji kiwanja cha kujengea taasisi hiyo wala hahitaji Wajumbe wa Bodi wa kuendesha kwani kichwa chake ndio Bodi yenyewe. Ameanza kutoa mihadhara kuhusu mustakabali wa nchi. Anatahadharisha kuwa tusipokuwa makini, Serikali inaweza 'kutekwa nyara' na kubaki kama 'mwanasesere'! Kwamba 'kikundi cha wahuni' wanaweza kuiteka nyara ikawa inaendeshwa na hicho kikundi!
1631598289874.png
 
Humphrey Polepole ameanza kujenga taasisi huru ya fikra! Hahitaji kiwanja cha kujengea taasisi hiyo wala hahitaji Wajumbe wa Bodi wa kuendesha kwani kichwa chake ndio Bodi yenyewe. Ameanza kutoa mihadhara kuhusu mustakabali wa nchi. Anatahadharisha kuwa tusipokuwa makini, Serikali inaweza 'kutekwa nyara' na kubaki kama 'mwanasesere'! Kwamba 'kikundi cha wahuni' wanaweza kuiteka nyara ikawa inaendeshwa na hicho kikundi!

Hizo ndizo fikra huru zenyewe! Lakini Polepole anasahau kuwa hata yeye alipokuwa Mwenezi na Msemaji wa Chama kinachoongoza Serikali, kuna watu walikuwa wanasema kama yeye anavyosema sasa! Watu wale waliokuwa na fikra huru wakati akina Polepole wameshika hatamu walipigwa; waliteswa; walitekwa; walibambikiwa Kesi za uchochezi, uhujumu uchumi na utakatishaji Fedha. Sisi Askofu tuliokuwa tukiwapazia sauti na kuwatetea watu hao tuliandamwa na hata kukiona cha moto.

Mwelezeni Mheshimiwa Humphrey Polepole kuwa sisi Askofu tunamkaribisha katika ulimwengu ulio huru ambao hauna dola ya kukutetea badala yake dola ndio iliyo na uhuru wa kukufanya cho chote kile! Kwa ujumla, katika ulimwengu huu hatuna kinga ye yote dhidi ya dola haijalishi tuna hadhi gani katika jamii! Huku ukitoa tu mawazo yaliyo tofauti na ya watawala au hata watu walio karibu na watawala, basi wewe unalo.

Jamii yetu huku ni kama ya wale wezee walioambiwa wakati Polepole yupo katika hatamu kuwa 'watatwangwatwangwa' na yule aliyekuwa Mkuu wa Mkoa ule aliozaliwa Mukwavinyika! Huku katika ulimwengu huu ulio huru, unaweza kulazwa mahabusu hata kwa kutetea watu haijalishi kama wewe ni Askofu au Profesa! Huku, Jeshi la Polisi halifuatu hata kanuni na Sheria za kukamata watuhimiwa! Huku, Askofu anaweza kufuatwa hata alfajiri katika faragha akiwa chumbani. Mwambieni Polepole kuwa asiwe na wasiwasi kwani akianza kufinywa kwa kusema ukweli na kutetea haki za wengine, sisi Askofu tutakuwa tayari kumpazia sauti. Mwambieni aungane na Askofu kuhamasisha upatikanaji wa Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula

POLE POLE kahusika kutufikisha hapa , ni SUKUMA GANG , na kwakuwa hsmkubali SSH ajiuzulu tu , atokee.
 
Mzee wa ile moja iliobaki weka kichwani ,nasikitika kukuambia unaakili Kama za nzi.Masaa 24 unawaza mavi yako wapi.
 
Back
Top Bottom