Askofu Mwamakula: Nani atamtangazia Ghofira/Msamaha wa Dhambi (absolution) Spika Ndugai?

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,634
697,845
"Nimekosa Mimi! Nimekosa Sana! Nimekosa Mimi! Mungu Anisamehe"! Ni toba ya mwisho kabisa katika 'Kanisa Katholico na la Kimitume' (Orthodox Catholic, Roman Catholic, Moravian, Anglican na Lutheran) inayoweza kufanywa na kuhani hadharani. Ni toba inayoelekezwa kwa Mungu peke yake ingawa husemwa hadharani. Msemaji anakuwa anasema huku akiwa anajipiga kifua kila akisema na hutamkwa mara tatu na hivyo anayetubu hujipiga kifua mara tatu! Toba ya aina hiyo haihojiwi na mtu ye yote na mamlaka za juu za dini ndizo hutangaza msamaha au ghofira (absolution)!

Kwa ujumla, Msemaji wa toba ya aina hiyo hujutia yote aliyowahi kuyasema na kuyatenda ikiwemo uasi dhidi ya Mungu na uasi dhidi ya Kanisa. Uzito wa toba hiyo hufananishwa na maungamo ya waumini katika madhehebu ya Roman Catholic, Anglican, Moravian, Orthodox Catholic na Lutheran. Maungamo hayo mara zote hutolewa mara tu baada ya ibada kuanza na hufuatiwa na ghofira au tangazo la msamaha wa dhambi linalotolewa na Padre au Mchungaji au Kasisi au Padre au Aakofu.

Mara nyingi ghofira au msamaha huo hutangazwa kwa waumini na Mchungaji au Kasisi au Padre au Askofu mwenye daraja la juu zaidi kati ya watumishi waliohudhuria ibada! Swali Hapa ni kuwa: "Je, katika haya majuto ya Spika Ndugai, ni nani anatakiwa kutoa ghofira au kumtangazia msamaha wa dhambi hadharani?"! Je, ni Kasisi wake, au Askofu wake? Je, Rais Samia anayo mamlaka ya kutoa ghofira au kutangaza msamaha wa dhambi kwa muumini mwingine? Bila ghofira kutolewa, majuto ya Ndugai yanabaki kuwa kalata ya kisiasa ili aendelee kuishi katika Bahari ya siasa za CCM!

Mutatis mutandis! Nampongeza Ndugai kuona mapungufu yake na kuomba radhi badala ya kuendeleza malumbano. Amefuata maneno ya Yesu aliyesema, ukiona Jeshi lako ni dogo kuliko Jeshi la adui yako basi nenda katafute amani kwake kwa kupatana naye kabla yeye hajakushukia na kukuangamiza!

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
 
naona unaenyoy demokrasia mkuu...

Ndugai ni spika wa Bunge, Baba wa watoto na familia, ana ndugu zake na jamaa wengine wako humuhumu..
I'm not condoning the disrespectful act lakini in the first place nadhani pia spika angejiheshimu huwa anaropoka mno mpaka alijiita yeye ni kichaa na ana file mirembe.

Jiheshimu uheshimiwe waswahili wanasemaga.
 
Duh yale yale ya mwendazake kupewa utukufu....hali bado mbaya kwetu kama mtu atakubali kulinganishwa na Mungu kiasi cha mwanadamu kuungama ili asamehewe na huyo mwanadamu.
Ndugai anazidi kuchanganya mambo bora angekaa kimya.
 
Tuna spika dhaifu sana tangu Bunge lianzishwe..ukweli hakua mweledi 2015-20 lakini haikumzuia yeye kubadilika 2021-25 kutumia kiti chake kuichallenge serikali na kua mtenda haki ila alichofanya ni udhaifu mkubwa sana na kama yeye kama kiongozi wa bunge ameufyata vipi hao wabubge wengine?.


Ndugai ameharibu zaidi kuliko kutengeneza ,hii imeonesha jinsi gani hawa watu wako kwa maslahi ya matumbo yao.

#katiba mpya spika asitokane na chama chochote.
 
Back
Top Bottom