Shoctopus
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 3,434
- 1,985
Assalamualaikum WanaJf!
Lengo la mada yangu ni kujadili swali kwamba: Inawezekana vipi kupata maridhiano kati ya CCM, chama tawala na CHADEMA, chama kikuu cha upinzani ilhali upande mmoja, CCM unahodhi mfumo wa mazungumzo, kwa maana ya ratiba ya vikao, mahali pa mkutano na gharama za uendeshaji na uwezeshaji wa mazungumzo hayo?
Napenda kujikita kwenye mada moja kwa moja:
Kwanza napenda kukiri kwamba kwangu mimi binafsi na naamini pia kwa yeyote anaeipenda nakuitakia mema nchi hii na taifa letu lazima atakuwa ameshachoshwa na kukatishwa tamaa kutokana na sintofahamu ya kisiasa ya Tanzania mpaka hapa tulipo. Kwasababu hakuna dalili kwamba mgogoro kati ya CCM na CHADEMA utamalizika lini, ili kila upande uridhike na kuendesha majukumu yake kwa taratibu zinazokubalika na kwa haki na ustaarabu; kwa maana ya kuaminiana na kuheshimiana.
Lakini pia inasikitisha sana kuona jinsi hali ya kisiasa inavyoendelea kukosa mwelekeo kwenye MUAFAKA kutokana na pande husika kushindwa kuondoa tofauti zao na vikwazo vinavyokwamisha utekelezaji wa masuala muhimu yenye maslahi kwa NCHI. ( Kwamfano Katiba mpya na Tume Huru ya Uchaguzi nk.)
Kimsingi haiwezekani pawepo na MUAFAKA kati ya pande hizi mbili CHADEMA na CCM bila pande hizi mbili kukubaliana katika masuala hayo ya msingi, ambayo (ukiacha Katiba mpya na Tume Huru ya Uchaguzi) baadhi yake ningependa kuyataja kama ifuatavyo:
1. DEMOKRASIA.
Binafsi na nina hakika wananchi wengi wanaojua maana na misingi ya demokrasia wanajua kwamba pande hizi mbili zinatofautiana sana katika tafsiri, na kwa vitendo kuhusu neno DEMOKRASIA. Kwasababu wakati upande mmoja unatafsiri ya kawaida kwamba DEMOKRASIA ni utawala wa watu kwa ridhaa na niaba yao na kwa ajili yao; upande wa pili (CCM) unaonekana kuwa na tafsiri yao, tofauti kinadharia na kivitendo!
Baadhi ya mambo muhimu kuhusu DEMOKRASIA ni pamoja na:
Kwatokana na misimamo hiyo miwili tofauti upande mmoja unaamini kwamba mfumo tulionao unakidhi vigezo vya DEMOKRASIA na utawala bora. Na kwamba maridhiano yatapatikana kupitia mfumo wanaouhodhi.
Lakini upande mwingine nao unaamini kwamba mfumo tulionao haukidhi wala kuruhusu utawala wa DEMOKRASIA. Na kwamba chini ya mfumo huu hakuna uchaguzi wa viongozi ulio huru na wa haki. MUAFAKA utapatikanaje hapo?
2. Pili kuhusu UTAWALA WA KIKATIBA NA SHERIA.
CCM na CHADEMA hawawezi kuondoa tofauti zao na kuafikiana kuhusu mwelekeo wa nchi kisiasa bila pande hizi mbili kukubaliana na kuheshimu misingi ya KATIBA na SHERIA; kifalsafa na kwa vitendo. Uzoefu unadhihirisha hivyo.
3. Jambo la tatu ni tafsiri tofauti kati ya pande hizi mbili kuhusu neno HAKI na neno AMANI.
Upande mmoja unaamini kwamba amani ni utiifu wa amri 'sheria'. Kuwepo hali isiyo na vurugu miongoni mwa wananchi. Na tafsiri yao ya hilo neno vurugu ni UKIMYA. Na kwamba ilmradi kuna UKIMYA lazima na AMANI ipo! Ni nadra sana kusikia upande huu kusisitiza watendaji wa ngazi zote kutenda kwa HAKI; iwe katika vyombo vya dola yaani polisi, magereza, usalama pamoja na mahakama za nchi! Mkazo uko katika vyombo vya dola kusimamia maamuzi ya watawala.
Upande wa pili unaamini kwamba BILA HAKI hakuna AMANI. Na kwamba utulivu pekee bila haki za binadamu na utawala bora ni utumwa!
Mambo hayo yanafanya mazungumzo kati ya pande hizi mbili yawe kama mchezo wa ngumi au soka usio na kanuni wala refa wa kusimamia hizo kanuni! Ni wazi hapo mshindi ni yule anaeandika kanuni na kumteua na kumlipa refa!
Jambo lingine linalofanya mazungumzo ya kutafuta maridhiano kati ya CCM na CHADEMA kuwa katika sintofahamu ni upande mmoja kuwa na mamlaka kuhusu lini mazungumzo hayo yafanyike, mahali pa mkutano, na yupi au mtu/watu wa aina gani wa kuongea nao kutoka upande wa pili!
Labda wengine tulitarajia kwamba kama mazungumzo hayo ni kati ya viongozi wa chama tawala na wa chama cha upinzani ushiriki wa Serikali ungekuwa kama msimamizi (refa) au mwezeshaji wa mazungumzo, jambo ambalo haliwezekani kwasababu upande mmoja unaamini CCM na Serikali ni kitu kimoja, nami nashindwa kutokubaliana na hoja hiyo. Na hicho ni kikwazo mojawapo cha maridhiano. Kwamba CCM iendelee kuwa, mfadhili na mwezeshaji, akiwa pia mchezaji na refa!
Kwahiyo katika mazingira kama yalivyo hapa juu ambapo upande mmoja kati ya hawa wawili unahodhi muda na 'uwanja' wa majadiliano kwakuwa ndio unaamua umshirikishe nani wa upande mwingine na kuamua lini na wapi majadiliano yafanyike; lazima upande huo wa pili utajiona unaingia ukiwa kwenye mazungumzo katika hali ya unyonge yaani bila CCM kuamua lini, wapi, na nani awepo/asiwepo upande wa wapinzani hakuna mkutano!
Kwa hali hiyo upande wa CHADEMA kabla ya kujikita kwenye mambo ya misingi ya mazungumzo watakuwa wakijiandaa kwa 'mapambano' dhidi ya CCM na mfumo wa mazungumzo badala ya hoja za msingi.
Na ndiyo maana ya kuamua kutumia "nguvu ya umma" (people's power) kushinikiza mabadiliko ya mfumo. Vita hii kati ya CCM na mfumo wa dola na CHADEMA na people's power kamwe haiwezi kuzaa matunda tunayotaka.
Hali hii ya CHADEMA kutaka wananchi wawe upande wao, na wanapoonekana kufanikiwa; hali hiyo (people's power) inafanya upande wa pili kujiona wana haki ya kujihami dhidi ya wasiotii sheria. Wanaoleta 'vurugu' kwa upande wa CCM, kwahiyo nao huanza kutumia (ama kwa waziwazi au kwa kisirisiri); vyombo vya dola na baadae taasisi za ushawishi kama press, TV, NGOs na inapobidi polisi. Na hatimaye wanatumia nguvu yao ndani ya bunge kutunga 'sheria' kwa lengo la kuhalalisha matumizi ya dola na mfumo uliopo.
Katika hali halisi tuliyonayo kisiasa hapa nchini na mbele ya ulimwengu ni dhahiri kwamba baada ya 2020 na kifo cha Hayati JPM ilibidi CCM iendelee kuishi kama mtawala (the defacto power).
Lakini Watanzania wenyenchi, pamoja na CHADEMA na CCM yenyewe tunapaswa kujiuliza kama sasa sio muda muafaka kutumia chombo huru cha upatanishi ili kuwezesha maridhiano kufikiwa kati ya pande hizi mbili?
Kipindi fulani kilichopita Tanzania ilishiriki kupatanisha migogoro ya kisiasa nchini Burundi na Kenya kupitia Hayati B. W. Mkapa na J. M. Kikwete. Wawili hao kila mtu akuwa Mwenyekiti wa CCM na Rais wa JMT. Litakuwa jambo la ajabu ikiwa CCM yenyewe itakataa wazo la kutumia chombo cha upatanishi kutoka kwa nchi majirani zetu au taasisi za kimataifa kama EU, UN, na kadhalika! Na kwa maana hii haitakuwa vibaya kwa kila upande kupendekeza taasisi, mtu mashuhuri kama akina Obasanjo, Tabo Mbeki, na wengine watakaokubalika na pande mbili ili mazungumzo kati ya CCM na CHADEMA yaendelee na kukamilika katika mazingira ya ukweli na uwazi, na kwa kuaminiana na uheshimiano.
Mpaka hapa inanibidi nihitimishe mada yangu kwa kuzingatia kwamba ni mada pana, nzito na yenye historia ndefu; na naamini pia wapo WanaJf humu wenye uwezo kuliko mimi, wa kudadavua hoja za pande mbili CHADEMA na CCM kuonyesha kwanini wasitafute mtu, taasisi au chombo cha upatanishi ili kuepusha hali inayoweza kupeleka nchi kwenye matatizo kama yaliyowakumba baadhi ya nchi jirani.
Nawasilisha!
Narudia tena kwamba kwa mwelekeo wa kitu kiitwacho mazungumzo ya muafaka kati ya CCM na CHADEMA; bila MPATANISHI ni vugumu sana kuuupata huo MUAFAKA.

- Uchaguzi wa viongozi katika ngazi zote kuwa huru na wa haki.
- Uhuru wa vyombo vya habari na wa raia kujieleza.
- Haki za binadamu na utawala bora. Na kadhalika.