Huyu Bishop ambae huwa anajinasibu kuwa ni mwanachadema kindakindaki hana ushawishi wowote kisiasa. Ni mlopokaji na mpiga kelele na kelele zake ni kama kelele za chura.
Nilishangaa sana kumsikia Mambo Sasa amemkamata eti anataka kuitisha maandamano. Huyu jinsi anavyopuuzwa na watu ndio wa kushawishi umma uandamane?
Kama anaushawishi mbona alizunguka na Lissu wakati wa Kampeni za uchaguzi mkuu na hakuleta ushasishi wa kuvutia watu na kujazia kura za Lissu.
Chadema tafuteni mikakati mingine,sio kutumia watu kama Mlwamakula ambao hawana ushawishi kabisa. Unadhani askofu mwenye ushawishi akisema neno nchi inatulia?