Askofu Josephat Gwajima amjibu Dr. Slaa

hammer-ya-gwajima.jpg
 
HAMY-D mara ujipendekeze kwa Lowasa, mara umtukane. Hakika nakushangaa sana kwa jinsi unavyopoteza mwelekeo
 
Dah!
huyu mchungaji naona kajikanyaga kweli, alikurupuka bila kuhusisha washauri, sasa hadi waumini wake amewaachia viulizo!
 
Sijasoma upuuzi wako ulioandika hapo, ila napenda kukuuliza swali moja, uliona sawa kwa Dr Slaa kutangazia dunia kuwa maaskofu wa Tanzania, kati ya 34, 30 wamepokea rushwa kutoka kwa Lowassa?

Lowassa ana madhambi yake ikiwemo ufisadi, lakini kuhusisha maaskofu na rushwa ni jambo hatari sana. Hivyo binafsi siwezi kujifanya mwendawazimu eti nimtete Dr Slaa kwa majibu anayopewa.

Hili ndio tatizo la watanzania wengi, tunapenda kukurupuka bila kufanya utafiti. Kama ulisikiliza hotuba ya Dr. Slaa alimnukuu huyo Gwajima kuwaa ndiye aliyesema na kuwa Maaskofu 30 wakatoliki wamehongwa maana wale wa Kilutheri walishakubali kumuunga Lowasa mkono. Dr. Slaa alisema kama ni kweli maaskofu wamehongwa?!!!!

Hata mimi namshangaa Gwajima kama kiongozi wa dini kutoa siri za waumini wake na kuendelea kusema kuwa Dr. Slaa amewatukana maaskofu akisahau jinsi alivyomtukana Kadinali Pengo. Kweli manabii wa uwongo hawataisha!
 
Dah!
huyu mchungaji naona kajikanyaga kweli, alikurupuka bila kuhusisha washauri, sasa hadi waumini wake amewaachia viulizo!
Tena kajikanyaga kweli. Kawaita mpaka walinzi wake ambao walikuwa wanafanya kazi ya kufuatilia maisha binafsi ya Dr Slaa
 
Nimemsikiliza kwa makini jana Askofu wa Kanisa la Ufufuko na Uzima, Josephat Gwajima akitoa utetezi wake juu ya kile kilichoelezwa na Dr Slaa kuwa ni Ushenga baina ya ndoa ya Lowasa na CHADEMA. Kimsingi amekubaliana na yale yaliyoelezwa na Dr Slaa na kujitetea eti alikuwa anafanya hivyo kama wajibu wake wa msingi kwa wanasiasa. Eti kwamba wanasiasa wengi wanapotaka kugombea wanaenda kwa waganga wa kienyeji hivyo yeye alitaka kumuandaa Lowasa kiroho.


Jambo lililonishtua zaidi ni pale aliposema kuwa kama Dr Slaa ataendelea kuwatukana Maaskofu wa Kanisa Katoliki, Anglikana, Lutherani, TAG, Masheikh na Maimamu nk, hatakaa kimya bali atajitokeza kuwatetea. Kwamba Masheikh na Maaskofu wasijisumbue kumjibu Dr Slaa bali yeye ataifanya kazi hiyo.


Binafsi nimetafakari sana juu ya msimamo huu wa Gwajima. Nimejiuliza, ni wapi Dr Slaa kawatukana Masheikh na Maaskofu? Au kuwaambia kuwa baadhi yao wamepokea hongo toka kwa Lowasa jambo ambalo ni kweli ni matusi? Ni lini Gwajima amekuwa na urafiki na Maaskofu wa Kanisa Katoliki? Ni lini Gwajima amekuwa na Urafiki na Masheikh na Maimamu?


1. Gwajima aliwahi kumtukana Askofu Pengo wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam


2. Gwajima huyo huyo aliwahi kumtukana Askofu Balina wa Kanisa Katoliki jimbo la Shinyanga ambaye kwa sasa ni marehemu.


3. Gwajima pia aliwahi kumtukana Askofu Norbert Mtega wa Kanisa Katoliki, Jimbo kuu la Songea.


4. Gwajima pia aliwahi kuwatukana Masheikh na Maimamu wakati wanadai haki ya Waislam ya kuwa na Mahakama ya Kadhi ndani ya Katiba Mpya.


Kimsingi Mchungaji Gwajima katika hili hana moral authority ya kumnyooshea kidole Dr Slaa ambaye hajatukana. Yeye ndiye alipaswa kujikanya mwenyewe kwa matusi ambayo amekuwa akiporomosha kila siku kwa mahasimu wake kiroho na kisiasa.

No lini wewe unae hoji umekuwa askofu au shekhe au umetumwa? Nani kakwambia gwajima kuwatetea maaskofu wenzake na mashehe ni kosa?. Mbona slaa alidhihalki mpango was lowasa wa kuwatoa mashehe akipata urais? Hivi unajuwa kama Dr.slaa amewahi kumwomba advocate kibatara peter awatetee hao mashehe mnao waita magaidi? Au mnaropoka tu kwasababu mnalipwa?. Angekuwa baba yako shehe yuko mahabusu anabakwa ungeaandika huo upuuzi wako?.
 
Kitendo cha UKAWA kumwachia Gwajima awe msemaji kwa ajili ya kufanikisha ushindi ni vema kikaangaliawa kwa tahadhari. Hii ni kutokana na kujenga taswira isiyo sahihi kwa wapiga kura. Kama inawezekana viongozi wa UKAWA walifanyie kazi jambo hili. Huu ni ushauri wangu tu, kwa sababu sijui majukumu yake Gwajima ndani ya CHADEMA(UKAWA).

Dr Slaa inawezekana alichokonoa ili waumbuke maana anajua huyu mchungaji mkurupukaji ....sasa kazi imekuwa nyepesi kabisa ....subirini uchaguzi upite ....
 
Nashangaa eti kiongozi wa kiroho wa aina hii nae ana waumini tena wanatoa sadaka kubwa hadi ananunua Hammer na helikopta, kweli wajinga ndio waliwao!
 
Mimi kama mwana jamvi wa muda mrefu ninasikitika sana kuona maana halisi ya jamiiforum ikibadilika toka jamvi la watu wenye fikra pevu, watu wanaojadili mambo kwa upana wakiangalia maslahi mapana ya nchi yetu, watu wanaojua kujenga hoja, kuzifafanua na kuzitetea kwa hoja na lugha yenye hekima, busara na upeo wa kiwango cha juu, leo imebadilika kuwa uwanja wa wahuni, walevi na watu wasiokuwa na hekima.
Lugha za matusi, uchochezi na ushabiki wa kijinga zimetawala jamvi mpaka kufikia wakati watu wanashindwa kuweka mambo sensitive ili yajadiliwe kwani watu smart na wanaojua kuchambua na kujadili mambo kwa upana na uelewa wa kiwango kilichokuwepo awali hawapo tena.
Inakera na kuuma sana kuona sehemu pekee ambayo watu wenye akiri timamu na wazalendo wa kweli walikua wakikutana kujadili na kubadilishana mawazo imekuwa namna hii.

"TUJISAHIHISHE"
Kama akili yako haijakomaa kwa kiwango cha kutosha kujadili mambo nyeti na yanayoamua mwelekeo wa Nchi yetu, bora mara trillion Ukae kimya na kusoma tu wanachochangia wenye akili timamu.

Huu ujinga mnaofanya humu kama wahuni wa vijiweni wanaochangia wakiwa wamebwia drugs na pombe nawaombeni sana muuweke pembeni.

INASHANGAZA SANA KUONA WATU WAKICHANGIA THREADS ZA AINA HII KWA USHABIKI WA AJABU AJABU KANA KWAMBA KILICHOFANYIKA NI KIZURI SANA.
UJINGA MKUBWA.
JAMBO ALILOFANYA GWAJIMA NI JAMBO LA KUKEMEWA KWA NGUVU ZOTE.
SASA WATU HUMU ETI SABABU TU GWAJIMA YUPO UPANDE WA UKAWA WANATAKA KUHALALISHA UPUUZI ALIOONGEA.
KUWENI NA AKIRI ENYI KIZAZI KILICHOPOTEA
 
Kuna wakati nahisi kuwa Wana CCM ni wajinga au CCM inawafanya wanachama wake kuwa wajinga au labda wajinga huvutiwa na CCM. Mtoa post si mzima kichwani mwake.
 
Dr kavuna alichopanda,cha msingi aje akanushe ili Gwajima aendelee kutueleza kilicho mpeleka Dr kwa Madiba nawatu aliokwenda nao.hayo mengine tunamwachia Bi jose na familia yake.
 
Sijasoma upuuzi wako ulioandika hapo, ila napenda kukuuliza swali moja, uliona sawa kwa Dr Slaa kutangazia dunia kuwa maaskofu wa Tanzania, kati ya 34, 30 wamepokea rushwa kutoka kwa Lowassa?

Lowassa ana madhambi yake ikiwemo ufisadi, lakini kuhusisha maaskofu na rushwa ni jambo hatari sana. Hivyo binafsi siwezi kujifanya mwendawazimu eti nimtete Dr Slaa kwa majibu anayopewa.


We are talking about the Moral responsibilities of Religious leaders, and especially those who listens to the confessions of their flocks. Also do not forget that it is the role of religious leaders to intervene and try and resolve any problems between couples and families, thus is it morally correct to talk of these confessions and problems in public and at press conference paid for with his followers contributions. Viongozi wa dini wanapaswa kuwa na uvumilivu wa ziada.

Jee unaunga mkono Gwajima kurekodi mazungumzo ya watu anaotatua matatizo yao, Jee anawafahamisha kama anawarekodi??
 
Nashangaa eti kiongozi wa kiroho wa aina hii nae ana waumini tena wanatoa sadaka kubwa hadi ananunua Hammer na helikopta, kweli wajinga ndio waliwao!
Viongozi wako wa dini ni malaika!? Mimi sio muumini wa Gwajima ila nilifurahi kitendo chake cha kumkemea Pengo
 
Sijasoma upuuzi wako ulioandika hapo, ila napenda kukuuliza swali moja, uliona sawa kwa Dr Slaa kutangazia dunia kuwa maaskofu wa Tanzania, kati ya 34, 30 wamepokea rushwa kutoka kwa Lowassa?

Lowassa ana madhambi yake ikiwemo ufisadi, lakini kuhusisha maaskofu na rushwa ni jambo hatari sana. Hivyo binafsi siwezi kujifanya mwendawazimu eti nimtete Dr Slaa kwa majibu anayopewa.

Alistahili Hayo Yote
 
Back
Top Bottom