Askofu Josephat Gwajima amjibu Dr. Slaa

mkuu unapata shidah!!! huku mitandaon tunakutana sisi wenyewe, unayoyasema hayamfikii bibi yangu kule kijijin, hivyo ni bora ukaenda kijijin ukasema hayo na sii huku ambapo huwezi badilisha msimamo wa mtu
 
Gwajima amenishangaza aliposema yeye ni mpatanishi,hivyo alitaka kuwapatanisha Lowasa na Chadema.Sasa najiuliza kwanini asingefikiria kwanza kuwapatanisha Lowasa na CCM?Mchungaji acha siasa utaumbuka bure
 
Mie Gwajima simpendi kwa sababu alimtukana kiongozi wangu mkuu wa dini ninayemuheshimu sana kuliko watu wote hapa duniani.
 
gwajima alizungumza kuhusu upotoshaji wa slaa kwa umma wa watanzania, na hakukisemea chama, kasema yote ambayo slaa alimuhusisha yeye kuwa ni mshenga
 
Mchungaji Josephat Gwajima nakusalimu bwana Yesu asifiwe.....

Hii ni saa ya ufufuo na uzimaaaaaaaaa..........halafu mbioo
Mchungaji jana wakati unazungumza na waandishi wa habari pale Land Mark nilidhani utajibu hoja za Daktari wa theolojia, falsafa na sheria za kanisa Padre Wilbroad Peter Slaa lakini ukaenda kuzungumza maisha yake binafsi,
Ulisahau kwenye eneo hilo bora Dkt. Slaa kuliko wewe unayevunja ndoa za waumini wako hata kufikia hatua ya kutaka kuvunja ndoa ya muimbaji wa nyimbo za injili FLORA MBASHA. Tuhuma hizi ni doa kubwa kwako kama mchungaji.


Unadai Dkt. Slaa aliwatukana viongozi wa dini wakiwemo maaskofu na masheikh wa kiislamu mbona katika mazungumzo ya Slaa na wanahabari hayo hayakuwepo! Lakini Mch. GWAJIMA inaonekana unasahau sana kama viongozi wanaokutumia ambao ni LOWASSA na MBOWE. Umeshasahau kuwa ni wewe uliyemtukana Kadinali Polycarp Pengo hata kufikia hatua ya kumuambia Kadinali Pengo ni kama mtoto mdogo anavishwa pampers, umesahau? Kati ya wewe na SLAA nani mwenye kuwatukana maaskofu?


Maneno yako kwa Askofu PENGO yalileta taharuki kubwa miongoni mwa waumini wa Kikatoliki na watanzania waliowengi ambao utamaduni wa kutukana viongozi wa dini hawajauzoea lakini nampongeza sana Kadinali PENGO kwani alionyesha ni kiasi gani kiongozi wa kiroho anavyopaswa kuishi kwani Mungu alimpa hekima ya kukujibu kwa kusema anakusamehe kwa moyo mweupe na Mungu akupe rehema ubadilike na akawaomba wote waliokwazika kwa kauli yako ya kumtukana na kumdhalilisha waungane naye kukusamehe na kukuombea ubadilike. Nilitegemea wewe au waliokutuma mngeomba msamaha kwa kupotoka ila mlikaa kimya sababu ni hulka yako kutukana wengine!


NIRUDI KWENYE MADA KUU


Mchungaji GWAJIMA ulitakiwa kujibu hoja hizi za DKT. SLAA

1. Kuwa wewe ndiye uliyempigia simu ya kumpa taarifa ya kukatwa kwa LOWASSA na hivyo CHADEMA wakaribishe, jambo ambalo ulilikubali.

2. Ushiriki wako kwenye mazungumzo ya kamati kuu ya CHADEMA ulienda kama nani?

3. Wewe ulimueleza SLAA kuwa wamkubali LOWASSA sababu viongozi wote wa dini wanamuunga mkono wakiwemo kanisa analosali LOWASSA yaani KKKT, masheikh na maaskofu wa 30 kati ya 34 wa kikatoliki ambao kila mmoja LOWASSA alimpa katili ya Milioni 60-300. Tulitaka ukubali au ukatae au ufafanue. Hukufanya hivyo! Maadam hukujibu tujue wewe ni kiongozi wa kanisa unayeunga mkono matumizi makubwa ya fedha kuwanunua watu hasa viongozi wa kiimani ili kupata madaraka jambo ambalo anapaswa ukafanye TOBA Mchungaji!

4. Dkt. SLAA alimtuhumu LOWASSA kwa kuidanganya CHADEMA kuwa angehamia na wenyeviti wa CCM wa Mikoa 22, wa Wilaya 88, na wabunge wanaomaliza muda wao 50. Kitu ambacho hakikufanyika hivyo LOWASSA akawa LIABILITY badala ya ASSET! Wewe uliyekubali kuwa ulikuwa mshenga hukueleza hili?

5. Dkt. SLAA anasema alieleza kabla ya LOWASSA kupokelewa aitishe waandishi wa Habari ajisafishe na makandokando ya ufisadi halafu ndio ahamie CHADEMA, Kitu ambacho hakikufanyika na hivyo kuendelea kuwa mchafu yaani FISADI. Tulitaka mshenga ufafanue hili kama kweli au si kweli?


DKT. SLAA BADO NI SHUJAA NA MSHUMAA WA SIASA ZA UPINZANI HAPA TANZANIA MAANA ALIZUNGUMZIA MISINGI YA KIONGOZI WA UMMA NA USALITI UNAOFANYWA DHIDI YA WANAMAGEUZI WALIOJENGA UPINZANI KWA JASHO NA DAMU HALAFU HARAKATI HIZO ZINASALITIWA KWA TAMAA YA FEDHA AU MADARAKA HUKU MISINGI ILIYOWEKWA IKIKIUKWA HASA YA UADILIFU.
Pole sanaaa
 
Mie Gwajima simpendi kwa sababu alimtukana kiongozi wangu mkuu wa dini ninayemuheshimu sana kuliko watu wote hapa duniani.

kiongoz yupi mkuu!!! kiongoz abayepishana kaul na maaskof wenzie?? ndio maana hata maaskof wenzie walimpuuza huyo unayempenda
 
Ipo siku mtagundua kwamba Dr.Slaa yuko sahihi kukataa kula na mafisadi

Ata kama lakini alitakiwa kuchuja kipi cha kuzungumza public na kipi kishughurikiwe kimaadili zaidi sasa yeye kama kuchafua viongozi wa dini kwa habari za kuambiwa na ata mlipoambiana uko hatupajui ilikua wapi na mlikutana kwa malengo yapi
 
Kazi mliyompa DR. ni ngumu mno!! na yeye alikurupuka kuikubali - huko aliko atakuwa anajuta!!
 
Na ndio maana nikasema Gwajima ni mtoto wa mjini Halafu mjanja na trust me jamaa anajua mengi tena ya pande zote. Amekuwa mwerevu kuliko TISS yetu

Sasa naelewa kwa nini Slaa baada ya kujua kuwa Gwajima atamjibu kupitia vyombo vya habari ikabidi asepe,he knew what was coming na alijua asingeweza kujibu mapigo.Kama msemaji mmoja hapo juu alivyosema,kama ataendelea kufungua mdomo wake tena (ambalo silioni kutokea) Gwajima atashusha "Little Boy"
 
Back
Top Bottom