Askofu Josephat Gwajima amjibu Dr. Slaa

Askofu Josephat Gwajima amjibu Dr. Slaa

HUYU NDIO KIONGOZI SAFI. VIONGOZI WENGI WA KIKRISTO WAOGA. BISHOP GWAJIMA YUKO vizuri.
 
Hizi ni dalili za taifa kuparaganyika! Kama wapo watu wanaoweza kushabikia analofanya Gwajima, yaani kujihusisha moja kwa moja na siasa kwa kuchukua upande, basi anguko la taifa liko njiani!!
 
Gwajima kiboko yao! Tunawahitaji wachungaji kama yeye wenye kusema bila woga sio wachungaji uchwara waliotufikisha hapa tulipo kwa dhambi ya ufisadi na huku wao wapo kimyaaa! Viva Gwajima songa mbele mpaka kieleweke.
 
Sana hawa viongozi wa dini njaa ndio waliotufikisha hapa. Gwajima ana ujasiri na sasa wanamhofia imekula kwao.
 
Kila jambo alilofanya Kristo ilikuwa kwa ajili ya Kanisa.Sasa kwa Bishop wakoo, kuvunja ndoa za watu ni kwa ajili ya Kanisa?Kutoa siri za waumini ni kwa ajili ya Kanisa?Kujihusisha na siasa ni kwa ajili ya kanisa.Kumbuka pia kwamba ana tuhuma za kujihusisha na madawa ya kulevya na mambo mengine machafu ambayo hayana haja ya kuyaongea hapa.No bwana,huyu sio mtumishi wa Mungu.
Kwa kweli watanzania wenzangu kabisa kabisa na kwa moyo thabiti, nimekua nikimuangalia askofu Gwajima kwa jicho la tofauti hasa jinsi anavyofanya mambo yake nikagundua kwamba, kiukweli kabisa tukiacha ushabika na misimamo ya kidini tunahitaji viongozi wa dini wa aina yake.. kwanini?

Kwasababu kwanza anaujasiri wa kusema jambo katika uhalisia wake bila unafiki na bila kumumunya maneno pia bila uoga.

Kwa wale wakirsto yaani wafuasi wakirsto yesu tunaaminu kwamba yesu aliwahi kuingia hekaluni akakuta kuna fanyika biashara, akakasirika sana na kuanza kupiga mateke meza zilizotumika kwa biashara huku akizipindua na kumwaga vitu, alifungua mabanda ya ndege na kuwaachia waondoke bila idhini ya wenyewe, alifungulia mbuzi na kondoo wote wokaondoka kiholela wasijulikane walikokwenda, ili mradi hakutaka unafiki alifanya jambo ambalo ukiliangalia ni kama fujo..

Yote haya alifanya yesu kwakua alikua hataki unafiki na alipokasirika alitaka watu wajue kabisa kwamba hili limemuuma, aliweka wazi alikemea...wakati mwingine alipopishana mtazamo na Petro alimwambia kwa hasira rudi nyuma yangu shetani! Si kwasababu petro alikua shetani bali kwasababu alibisha asichokijua.

Sasa najiuliza kwa wanaomsimanga Gwajima kweli wanajua walifanyalo? Na je angefanya kama alivyofanya yesu tungemuita majina gani? Tafakari...
 
Gwajima alipoita waandishi wa habari katika kujibu tuhuma alizotoa Dr Slaa, mategemeo ya watanzani yalikuwa makubwa sana kusikia majadiliano yao yalivyokwenda mpaka Lowasa kuingia CHADEMA. Badala yake Gwajima kapoteza dakika 53 kueleza mambo ya jikoni kati ya Dr Slaa na Mke wake. Kweli kampeni za mwaka huu zimeingiliwa!

Napenda ikumbukwe Dr Slaa alieleza kuwepo kwake katika mchakato wa kumleta Lowasa ndani ya CHADEMA, na akaenda mbali zaidi kueleza wapi alitofautiana na viongozi wengine hatua kwa hatua. Matarajio yangu ni kuwa Gwajima angejibu hatua kwa hatua wapi walitofautiana na wapi walikuwa pamoja. Kumbuka kuwa Gwajima alikiri kuwa aliitwa kama mpatanishi, hii inamaanisha dhahiri kuwa kulikuwa na kuhitilafiana kwa viongozi hao. Kwa bahati mbaya Gwajima hajatamka hata sababu moja ya kuhitilafiana kwao. Badala yake anatupa udaku wa jikoni kwa Dr slaa na mkeo, hii ni hatari sana kwa siasa za Tanzania.

Ni nani kati yenu mlioowa ambao hamna matatizo ya unyumba huko majumbani kwenu? Ni mwl nyerere hakuwa na matatizo na mkeo, au Alhaj Mwinyi, au Mkapa na Kikwete? Sijawauliza ya Mbowe, Bob Makani, Lowasa, Ndesamburo au Lipumba? Jamani tuachane na siasa za udaku.


Kazungumza mengi, toka mashetani mpaka Jikono Lakini si siasa, ni ulaghai mtupu. Eti anasema Enyi, maaskofu Katoliki, protestant, Pentakost na Mashekhe huyu Dr Slaa akiwagusa msimjibu niachieni mimi, wewe ni nani? Acha kila mmoja ajibu kwa nafsi yake usiwajibie watu. Jamani msikubali Gwajima awatawale ni shetani mkubwa huyu.

Azungumzia juu ya usalama kumlinda Dr Slaa. Hii ni haki yake na ni haki ya kila mtanzania anapohisi usalama wake uko hatarini. Mimi namkosoa Gwajima na najua hawezi kunidhuru kwanini nikawaite usalama waje kunilinda? Hata yeye akijisikia kuwa usalama wake uko hatarini aende kwa usalama watamlinda. Hatuna usalama watakao walinda watanzania 40 milioni wasiotishiwa usalama wao.

Nahitimisha kwa kusema huyu Gwajima ni mnafiki, mzandiki, mdini, mpotoshaji, mzabizabina, muongo na anaingia katika maeneo ya siasa ambaye hana uwezo nae. Namashaka hata kama anauwezo wa kuendesha mambo ya kidini. Bali ninauhakika kuwa huyu Gwajima ni baba wa MASHETANI.

Nawe ni wale wale. Wa wimbo ni "ile ilee"
 
Hata kama kampeni ya Lowasa nilipenda ajibu tofauti iliyokuwepo ambayo yeye alikwenda kusuluhisha. Maelezo kinaganaga ndio yangemsafisha sio habari za jikoni kwa Dr Slaa.

Unachopenda wewe usilazimishe wengine wapende
 
Gwajima ni Askofu mwenye mahaba mazito na lowasa tell him nothing about lowasa!
 
Nalia na Mod, maana kanishughulikia. Najiandaa kuanzisha Thread nyingine juu ya maelezo choo ya Gwajinga.
 
Unachopenda wewe usilazimishe wengine wapende

Kwa hiyo unachopenda wewe ni siasa za udaku. Utamchagua mtu kwa kueneza mambo ya jikoni kwako na kwangu. Kweli hayo ni mabadiliko kweli kweli. Kumbe akina Gwajima ni wengi. Ila sijui ni wengi kiasi gani.
 
Nawe ni wale wale. Wa wimbo ni "ile ilee"

Well, inawezekana. Lakini usisahau kutenganisha kati ya Gazeti la Ijumaa na Tanzania Daima. Kifupi kati ya Udaku na Siasa.

Mwenzako nilishajikomboa kwenye hilo, kwani hata ninapoenda kununua gazeti ni lazima nijue hili gazeti ni la udaku au mambo makini. Big up!
 
Hana ishu huyo. Keshalambushwa rupia na ccm saaizi amebaki kuitwa controversial padre/politician
 
Kwa hiyo unachopenda wewe ni siasa za udaku. Utamchagua mtu kwa kueneza mambo ya jikoni kwako na kwangu. Kweli hayo ni mabadiliko kweli kweli. Kumbe akina Gwajima ni wengi. Ila sijui ni wengi kiasi gani.

Yani mkuu ulichosikia wewe kwa muda wote wa 53mns ni habari za jikoni tu!!! hujasikia hata mahusiano kati ya ujio wa Lowassa UKAWA, Dr Slaa kuwania uraisi na matakwa ya mchumba wake? be fair mkuu
 
Jamani timu ya dr slaa mko wapi mjibuni Gwajima ili tufahamu mzigo na watu wanne south africa, ni muhimu sana kuufahamu huu mzigo jamani, njooni, jitokezeni mumjibu, kwa nn mpo kimya hivyoooooooo. Mnaogopaaaaaaaaaaaa:bange:
 
Back
Top Bottom