Askofu Josephat Gwajima amjibu Dr. Slaa

Askofu Josephat Gwajima amjibu Dr. Slaa

Uchaguzi huu umeingiliwa, eti Maaskofu ndio wanaendesha midahalo kwenye Maluninga.

Kuoa au kutooa si mjadala watanzania utaotunufaisha.

Kweli uchaguzi huu ni midahalo ya kifamilia. Du huu ni uchaguzi kweliiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii.
 
Siasa ni Sawa na askari vitani kwenye uwanja wa mapambano kwahiyo chochote chaweza kuwa silaha kwakuwa kinachotafutwa ni ushindi
 
gwajima safii.umesaidia mno.
dawa imewaingia sana
ona tunavyosapoti ujinga... amekuja hadi na ushahidi feki!! katengeneza sms akasahau kuedit tarehe... tunawapa airtime watu wasio na maana badala ya kusikiliza sera za mgombea
 
Gwajima alivyopenya kwa mke wa Dk. Slaa

Mwandishi Wetu Toleo la 422 9 Sep 2015

GWAJIMA%20JOSEPHAT_0.jpg

ASKOFU wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, ambaye ndiye kiungo (mshenga) wa kufanikisha ujio wa Edward Lowassa, na kisha kuwania urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), alijipenyeza kwa mke wa Dk. Wilbrod Slaa, Josephine Mushumbushi, kuhakikisha Slaa haondoki kwenye chama hicho, Raia Mwema, limeelezwa.

Gwajima alifanya hivyo ikiwa ni juhudi zake za kuhakikisha Dk. Slaa haondoki Chadema ili kumwongezea nguvu za kisiasa Lowassa na hatimaye kufanikisha ushindi wake wa urais, Oktoba 25, mwaka huu.
Ilikuwa asubuhi ya Julai 28, mwaka huu, Gwajima alifanya kazi ya ziada kumshawishi Josephine, akifanya hivyo baada ya kushindwa kuelewana na Dk. Slaa mwenyewe ambaye alikataa ushauri wake.

Dk. Slaa ndiye anayefichua hali hiyo inayoeleza namna juhudi mbalimbali zilizofanyika na viongozi kadhaa wa Chadema kupitia kwa Gwajima bila mafanikio. Mahojiano kwa kirefu na Dk. Slaa yamechapishwa katika gazeti hili.

“Kama hana hofu ya Mungu atapinga, na mimi ndiyo maana nikahoji hata uaskofu wa Gwajima kutokana na hilo. Kama Askofu anapokanusha vitu alivyosema sasa unategemea waumini watafanya nini? Gwajima amembembeleza mke wangu asubuhi ya tarehe 28, Julai, alipotoka nyumbani kwangu tumegombana, alikwenda kumtafuta mke wangu amemkuta Kibo Complex (Tegeta) wamekaa kwenye gari, mke wangu akaweka msimamo wa kutaka kutubembeleza anatushawishi tumkubali Lowassa, na ndiyo maana nikasema alipozungumza hoja ya maaskofu kuhongwa alikuwa anajenga hoja ya kwamba nimuunge mkono kwa sababu huyu mtu anaungwa mkono na watu wengine wengi.

“Bahati mbaya anatumia hoja kwamba amewanunua, mimi hasira yangu siyo kwa hela kutolewa kwa maaskofu, lakini askofu inafikaje mahali hatambui madhara ya rushwa, askofu ni mtu anayepaswa kupiga kelele dhidi ya rushwa, lakini yeye anaona huyu tumuunge tu mkono, sikushangaa baadaye kwa sababu kuna kauli imesemwa hata kama ni kufunga mkataba na shetani, ilitolewa na Tundu Lissu, tufanye tu mkataba huo ili kuiondoa CCM, mimi nimesema siwezi kukubali kufanya mkataba na shetani kwa ajili ya lengo lolote lile.

“Kuna mahali katika theolojia, kuna kitu kinaitwa ‘the end justifies the means, naomba hawa wote wanaoutumia huu msemo waende shule wasome Theoloji ya Thomas wa Aquino, waelewe huo mfano unatumika katika mazingira gani, sababu ni hasara ya watu au kuwa wasomi nusu wanachukua misemo hawajui hata misingi yake, nimesoma theoloji najua maana ya Mtakatifu Thamos wa Aquino anaposema the end justices the means, siyo katika mazigira haya na kama watu ahwajui basi waache kutoa nukuu amabzo hawajazifanyia utafiti,” alisema

Slaa na urais wa Lowassa
Katibu Mkuu huyo wa zamani wa Chadema, Dk. Slaa, katika hatua nyingine amezidi kuhatarisha mbio za mgombea urais wa chama hicho, Edward Lowassa.
Katika kuhatarisha huko, safari hii, katika mahojiano maalumu na Gazeti hili la Raia Mwema, Dk. Slaa amefichua utajiri wenye shaka wa Lowassa.

Kwa mujibu wa mahojiano hayo hayo yaliyochapishwa kwa kirefu katika kurasa za 14 na 19 za gazeti hili, anasema; “Lowassa, watu wengi hawajui anahusika na utajiri wa aina gani, ndiyo maana swali analotakiwa kujibu ni uhalali wa utajiri wake, asiendelee kuwapumbaza Watanzania kwamba anachukia umasikini, tunajua utajiri siyo kosa, si dhambi, si ufisadi, ufisadi ni namna ulivyopata utajiri wako.”

Akisimulia zaidi, anasema; “Tarehe 07, April, 1997 (Lowassa) alianzisha yeye na mke wake Regina kampuni inayoitwa Barare Ltd, katika kampuni hiyo Lowassa ana hisa 500 na Regina ana hisa 500, na hii ni 1997, akiwa mbunge tu, hisa 500 zilikuwa na thamani ya shilingi milioni 50, niambie hizo milioni 50 kila mmoja walizipata wapi? Kumbuka Frederick Sumaye akiwa Waziri Mkuu, alituhumiwa kwa kukopa NSSF milioni 50, huyu hakukopa alizipata wapi?”

Alisema Lowassa ana mali nyingi ambazo hajaziorodhesha kwenye Sekretariati ya Maadili ya Viongozi wa Umma, jambo ambalo ni kosa, akiongeza kwamba baada ya Lowassa kujiuzulu uwaziri mkuu, Juni 30,2010, kampuni hiyo ikanunua hisa 7,500 kwa shilingi 60,000.

“Hiyo ni jumla ya shilingi milioni 450, jiulize wakati huo Lowassa amemaliza miaka miwili ya uwaziri mkuu, akabaki mbunge wa kawaida, hivi milioni 450 huyu Lowassa alizitoa wapi? Lakini Lowassa ni mbunge wa kawaida posho za mbunge wa kawaida zinajulikana, na mshahara unajulikana milioni 450 zilitoka wapi, ingekopwa tungeona kwenye fomu yake ya maadili kule kwenye Sekretariati ya Maadili na kosa kubwa zaidi hata kule hakueleza kwamba ana hisa zimenunnuliwa kutoka kwenye kampuni inaitwa Integrated property Limited, kutokutaja hisa zako kwenye Sekretariati ya Maadili ni kosa linalofanya mbunge afutwe ubunge bila hata kwenda mahakamani,” alisema.

Katika hatua nyingine Dk. Slaa alionya kuhusu pupa ya mabadiliko wanayoyataka Watanzania, akisema yanaweza kuleta majuto badala ya neema wanayoitarajia.
“Watanzania wajiulize mabadiliko daima yana sura mbili kuna mabadiliko mema na kuna mabadiliko mabaya, hata Hitler kwa wakati wake alileta mabadiliko yakaishia kuua mamilioni ya watu, kwa hiyo sisi tunaojua kwenye dhamiri zetu hatuwezi kukaa kimya,” alisema.

- See more at: Raia Mwema - Gwajima alivyopenya kwa mke wa Dk. Slaa

Chanzo: Gazeti la Raiamwema
 
"Dk Slaa, alimshambulia Lowassa kwa mwenendo wake juu ya maadili ya uongozi, juu ya ufisadi na tabia yake ya uongo juu ya mambo ya kuliongoza taifa letu. Hakusema chochote kuhusu maisha ya ndoa ya Lowassa na wala juu ya maisha binafsi ya Lowassa. Tunaamini Dk, Slaa kwa kiasi fulani anayafahamu maisha binafsi ya Lowassa, lakini kwa vile hoja ya msingi si maisha binafsi, yeye hakugusia jambo hili." na Bado hapa hasemi kuhusiana na Binti mwimbaji wa nyimbo za kiinjili wa Arusha alivyotafunwa na mamvi kiasi cha kuhatarisha ndoa yake, Dr anajua hilo japo hasemi kwa kuwa sio muhimu!
 
Who is Gwajima in this country hadi tupoteze muda kumjadili?
 
Heshima pekee ninayompa Dr.W.Slaa kwa sasa ni kutokana na umri. Out of that nimempuuza kwa viwango vya kimataifa
 
Last edited by a moderator:
Gwajima alivyopenya kwa mke wa Dk. Slaa

Mwandishi Wetu Toleo la 422 9 Sep 2015

GWAJIMA%20JOSEPHAT_0.jpg

ASKOFU wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, ambaye ndiye kiungo (mshenga) wa kufanikisha ujio wa Edward Lowassa, na kisha kuwania urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), alijipenyeza kwa mke wa Dk. Wilbrod Slaa, Josephine Mushumbushi, kuhakikisha Slaa haondoki kwenye chama hicho, Raia Mwema, limeelezwa.

Gwajima alifanya hivyo ikiwa ni juhudi zake za kuhakikisha Dk. Slaa haondoki Chadema ili kumwongezea nguvu za kisiasa Lowassa na hatimaye kufanikisha ushindi wake wa urais, Oktoba 25, mwaka huu.
Ilikuwa asubuhi ya Julai 28, mwaka huu, Gwajima alifanya kazi ya ziada kumshawishi Josephine, akifanya hivyo baada ya kushindwa kuelewana na Dk. Slaa mwenyewe ambaye alikataa ushauri wake.

Dk. Slaa ndiye anayefichua hali hiyo inayoeleza namna juhudi mbalimbali zilizofanyika na viongozi kadhaa wa Chadema kupitia kwa Gwajima bila mafanikio. Mahojiano kwa kirefu na Dk. Slaa yamechapishwa katika gazeti hili.

“Kama hana hofu ya Mungu atapinga, na mimi ndiyo maana nikahoji hata uaskofu wa Gwajima kutokana na hilo. Kama Askofu anapokanusha vitu alivyosema sasa unategemea waumini watafanya nini? Gwajima amembembeleza mke wangu asubuhi ya tarehe 28, Julai, alipotoka nyumbani kwangu tumegombana, alikwenda kumtafuta mke wangu amemkuta Kibo Complex (Tegeta) wamekaa kwenye gari, mke wangu akaweka msimamo wa kutaka kutubembeleza anatushawishi tumkubali Lowassa, na ndiyo maana nikasema alipozungumza hoja ya maaskofu kuhongwa alikuwa anajenga hoja ya kwamba nimuunge mkono kwa sababu huyu mtu anaungwa mkono na watu wengine wengi.

“Bahati mbaya anatumia hoja kwamba amewanunua, mimi hasira yangu siyo kwa hela kutolewa kwa maaskofu, lakini askofu inafikaje mahali hatambui madhara ya rushwa, askofu ni mtu anayepaswa kupiga kelele dhidi ya rushwa, lakini yeye anaona huyu tumuunge tu mkono, sikushangaa baadaye kwa sababu kuna kauli imesemwa hata kama ni kufunga mkataba na shetani, ilitolewa na Tundu Lissu, tufanye tu mkataba huo ili kuiondoa CCM, mimi nimesema siwezi kukubali kufanya mkataba na shetani kwa ajili ya lengo lolote lile.

“Kuna mahali katika theolojia, kuna kitu kinaitwa ‘the end justifies the means, naomba hawa wote wanaoutumia huu msemo waende shule wasome Theoloji ya Thomas wa Aquino, waelewe huo mfano unatumika katika mazingira gani, sababu ni hasara ya watu au kuwa wasomi nusu wanachukua misemo hawajui hata misingi yake, nimesoma theoloji najua maana ya Mtakatifu Thamos wa Aquino anaposema the end justices the means, siyo katika mazigira haya na kama watu ahwajui basi waache kutoa nukuu amabzo hawajazifanyia utafiti,” alisema

Slaa na urais wa Lowassa
Katibu Mkuu huyo wa zamani wa Chadema, Dk. Slaa, katika hatua nyingine amezidi kuhatarisha mbio za mgombea urais wa chama hicho, Edward Lowassa.
Katika kuhatarisha huko, safari hii, katika mahojiano maalumu na Gazeti hili la Raia Mwema, Dk. Slaa amefichua utajiri wenye shaka wa Lowassa.

Kwa mujibu wa mahojiano hayo hayo yaliyochapishwa kwa kirefu katika kurasa za 14 na 19 za gazeti hili, anasema; “Lowassa, watu wengi hawajui anahusika na utajiri wa aina gani, ndiyo maana swali analotakiwa kujibu ni uhalali wa utajiri wake, asiendelee kuwapumbaza Watanzania kwamba anachukia umasikini, tunajua utajiri siyo kosa, si dhambi, si ufisadi, ufisadi ni namna ulivyopata utajiri wako.”
1441952255056.jpg
Akisimulia zaidi, anasema; “Tarehe 07, April, 1997 (Lowassa) alianzisha yeye na mke wake Regina kampuni inayoitwa Barare Ltd, katika kampuni hiyo Lowassa ana hisa 500 na Regina ana hisa 500, na hii ni 1997, akiwa mbunge tu, hisa 500 zilikuwa na thamani ya shilingi milioni 50, niambie hizo milioni 50 kila mmoja walizipata wapi? Kumbuka Frederick Sumaye akiwa Waziri Mkuu, alituhumiwa kwa kukopa NSSF milioni 50, huyu hakukopa alizipata wapi?”

Alisema Lowassa ana mali nyingi ambazo hajaziorodhesha kwenye Sekretariati ya Maadili ya Viongozi wa Umma, jambo ambalo ni kosa, akiongeza kwamba baada ya Lowassa kujiuzulu uwaziri mkuu, Juni 30,2010, kampuni hiyo ikanunua hisa 7,500 kwa shilingi 60,000.

“Hiyo ni jumla ya shilingi milioni 450, jiulize wakati huo Lowassa amemaliza miaka miwili ya uwaziri mkuu, akabaki mbunge wa kawaida, hivi milioni 450 huyu Lowassa alizitoa wapi? Lakini Lowassa ni mbunge wa kawaida posho za mbunge wa kawaida zinajulikana, na mshahara unajulikana milioni 450 zilitoka wapi, ingekopwa tungeona kwenye fomu yake ya maadili kule kwenye Sekretariati ya Maadili na kosa kubwa zaidi hata kule hakueleza kwamba ana hisa zimenunnuliwa kutoka kwenye kampuni inaitwa Integrated property Limited, kutokutaja hisa zako kwenye Sekretariati ya Maadili ni kosa linalofanya mbunge afutwe ubunge bila hata kwenda mahakamani,” alisema. 1441952255056.jpg

Katika hatua nyingine Dk. Slaa alionya kuhusu pupa ya mabadiliko wanayoyataka Watanzania, akisema yanaweza kuleta majuto badala ya neema wanayoitarajia.
“Watanzania wajiulize mabadiliko daima yana sura mbili kuna mabadiliko mema na kuna mabadiliko mabaya, hata Hitler kwa wakati wake alileta mabadiliko yakaishia kuua mamilioni ya watu, kwa hiyo sisi tunaojua kwenye dhamiri zetu hatuwezi kukaa kimya,” alisema.

- See more at: Raia Mwema - Gwajima alivyopenya kwa mke wa Dk. Slaa

Chanzo: Gazeti la Raiamwema

Too late raia mbaya 1441952255056.jpg
 
Gwajima alipoita waandishi wa habari katika kujibu tuhuma alizotoa Dr Slaa, mategemeo ya watanzani yalikuwa makubwa sana kusikia majadiliano yao yalivyokwenda mpaka Lowasa kuingia CHADEMA. Badala yake Gwajima kapoteza dakika 53 kueleza mambo ya jikoni kati ya Dr Slaa na Mke wake. Kweli kampeni za mwaka huu zimeingiliwa!

Napenda ikumbukwe Dr Slaa alieleza kuwepo kwake katika mchakato wa kumleta Lowasa ndani ya CHADEMA, na akaenda mbali zaidi kueleza wapi alitofautiana na viongozi wengine hatua kwa hatua. Matarajio yangu ni kuwa Gwajima angejibu hatua kwa hatua wapi walitofautiana na wapi walikuwa pamoja. Kumbuka kuwa Gwajima alikiri kuwa aliitwa kama mpatanishi, hii inamaanisha dhahiri kuwa kulikuwa na kuhitilafiana kwa viongozi hao. Kwa bahati mbaya Gwajima hajatamka hata sababu moja ya kuhitilafiana kwao. Badala yake anatupa udaku wa jikoni kwa Dr slaa na mkeo, hii ni hatari sana kwa siasa za Tanzania.

Ni nani kati yenu mlioowa ambao hamna matatizo ya unyumba huko majumbani kwenu? Ni mwl nyerere hakuwa na matatizo na mkeo, au Alhaj Mwinyi, au Mkapa na Kikwete? Sijawauliza ya Mbowe, Bob Makani, Lowasa, Ndesamburo au Lipumba? Jamani tuachane na siasa za udaku.

Kazungumza mengi, toka mashetani mpaka Jikono Lakini si siasa, ni ulaghai mtupu. Eti anasema Enyi, maaskofu Katoliki, protestant, Pentakost na Mashekhe huyu Dr Slaa akiwagusa msimjibu niachieni mimi, wewe ni nani? Acha kila mmoja ajibu kwa nafsi yake usiwajibie watu. Jamani msikubali Gwajima awatawale ni shetani mkubwa huyu.

Azungumzia juu ya usalama kumlinda Dr Slaa. Hii ni haki yake na ni haki ya kila mtanzania anapohisi usalama wake uko hatarini. Mimi namkosoa Gwajima na najua hawezi kunidhuru kwanini nikawaite usalama waje kunilinda? Hata yeye akijisikia kuwa usalama wake uko hatarini aende kwa usalama watamlinda. Hatuna usalama watakao walinda watanzania 40 milioni wasiotishiwa usalama wao.

Nahitimisha kwa kusema huyu Gwajima ni mnafiki, mzandiki, mdini, mpotoshaji, mzabizabina, muongo na anaingia katika maeneo ya siasa ambaye hana uwezo nae. Namashaka hata kama anauwezo wa kuendesha mambo ya kidini. Bali ninauhakika kuwa huyu Gwajima ni baba wa MASHETANI.
 
Gwajima yuko kwenye timu ya kampeni ya Lowassa. Alichokifanya pale ni mkakati wa kampeni wa Lowassa.
 
Gwajima amesema hivi "Roketi ranger(Dr.Slaa) iliyotumiwa na CCM ili kusambaratisha ukawa, risasi zake zimemkosa adui, na moto umewaunguza wenyewe"
 
Gwajima alipoita waandishi wa habari katika kujibu tuhuma alizotoa Dr Slaa, mategemeo ya watanzani yalikuwa makubwa sana kusikia majadiliano yao yalivyokwenda mpaka Lowasa kuingia CHADEMA. Badala yake Gwajima kapoteza dakika 53 kueleza mambo ya jikoni kati ya Dr Slaa na Mke wake. Kweli kampeni za mwaka huu zimeingiliwa!

Napenda ikumbukwe Dr Slaa alieleza kuwepo kwake katika mchakato wa kumleta Lowasa ndani ya CHADEMA, na akaenda mbali zaidi kueleza wapi alitofautiana na viongozi wengine hatua kwa hatua. Matarajio yangu ni kuwa Gwajima angejibu hatua kwa hatua wapi walitofautiana na wapi walikuwa pamoja. Kumbuka kuwa Gwajima alikiri kuwa aliitwa kama mpatanishi, hii inamaanisha dhahiri kuwa kulikuwa na kuhitilafiana kwa viongozi hao. Kwa bahati mbaya Gwajima hajatamka hata sababu moja ya kuhitilafiana kwao. Badala yake anatupa udaku wa jikoni kwa Dr slaa na mkeo, hii ni hatari sana kwa siasa za Tanzania.

Ni nani kati yenu mlioowa ambao hamna matatizo ya unyumba huko majumbani kwenu? Ni mwl nyerere hakuwa na matatizo na mkeo, au Alhaj Mwinyi, au Mkapa na Kikwete? Sijawauliza ya Mbowe, Bob Makani, Lowasa, Ndesamburo au Lipumba? Jamani tuachane na siasa za udaku.

Kazungumza mengi, toka mashetani mpaka Jikono Lakini si siasa, ni ulaghai mtupu. Eti anasema Enyi, maaskofu Katoliki, protestant, Pentakost na Mashekhe huyu Dr Slaa akiwagusa msimjibu niachieni mimi, wewe ni nani? Acha kila mmoja ajibu kwa nafsi yake usiwajibie watu. Jamani msikubali Gwajima awatawale ni shetani mkubwa huyu.

Azungumzia juu ya usalama kumlinda Dr Slaa. Hii ni haki yake na ni haki ya kila mtanzania anapohisi usalama wake uko hatarini. Mimi namkosoa Gwajima na najua hawezi kunidhuru kwanini nikawaite usalama waje kunilinda? Hata yeye akijisikia kuwa usalama wake uko hatarini aende kwa usalama watamlinda. Hatuna usalama watakao walinda watanzania 40 milioni wasiotishiwa usalama wao.

Nahitimisha kwa kusema huyu Gwajima ni mnafiki, mzandiki, mdini, mpotoshaji, mzabizabina, muongo na anaingia katika maeneo ya siasa ambaye hana uwezo nae. Namashaka hata kama anauwezo wa kuendesha mambo ya kidini. Bali ninauhakika kuwa huyu Gwajima ni baba wa MASHETANI.

Kama huna la kuandika ni bora ukadowea dona na kushushia maji ya kandoro ukahesabu siku
 
Back
Top Bottom