Askofu Josephat Gwajima amjibu Dr. Slaa

Askofu Josephat Gwajima amjibu Dr. Slaa

Gwajima amedharaulika

Hahahaha haaaaa! Huo ni mtazamo wako kwa kijiakili chako... nikutaarifu tu... tupo weeeengi ambao kwa tukio hili tumemweshimu Gwajima ! Yaan ni shujaa wetu! Km anakuboa sn.. Kalambe magadi! Maana malimao yameadimika.
 
Anatutaka tuwe watiifu na haturuhusiwi kuwa na mtazamo hasi na utawala, hii ina kwamba tuwe kama kondoo tu kwa lolote tuambiwalo na watawala tusihoji kwa kuwa kitendo cha kuhoji jambo ni lazima uwe na mtazamo tofauti hapo tayari ni mtazamo hasi.
Sasa mimi namuuliza Askofu wangu vipi tunaweza kubadirisha uongozi/utawala kwa kipiga kura kama watu hawawezi kuwa na mtazamo hasi kwa yale wanayofanyiwa, maana yake ni kwamba kwenye kampeni watawala wanapotudangaya dhahiri tusipinge tuwaitikie tuwape kura, ukiukataa uongo wao una mtazamo hasi.
Kwa kweli mi sijakubaliana naye nilikuwa namsikiliza kupitia redio yake ya wapo.
Angalizo kama tunajadili tuangalie zaidi labda nini maana ya mtazamo hasi pengine mi ndo sijaelewa
 
Huyo mtu maisha yake yamefungama na CCM unategemea nini Namna hii ndio maana hata waumini wao wakati mwingine huwa wanawadharau Utaniambiaje nitii Utawala unaonikandamiza.....Anatumia vibaya tafsiri ya Biblia Utii mwingine niwakijinga Ingekuwa hivyo YESU asingewatimua waliokuwa wanauza bidhaa mle HEKALUNI
 
Naunga mkono hoja kwa sababu kuna siku nilikutana na Dr. Slaa mahali akiwa na wife to be wake, tukazungumza kidogo niliuliza kuhusu yeye kugombea urais 2015, wife to be ndie alitoa msimamo fulani!. Kwa vile mazungumzo yale yalikuwa sio formal, nayaregard as off the record.
P.
 
Kwanini Dr.Slaa anatafuta aibu, kwanini asitulie huko Canada kama alivyokuwa kafanya mwanzo?! Umri wenyewe umeshaenda sana tu, anadhani ata accomplish nini kwenye siasa za Tanzania kwa muda aliobaki nao?! Angetulia na mkewe walee mtoto badala ya kukimbizana, ccm wameshampa shavu la retirement ni balozi kwasasa na atapokea retirement benefits mpaka afe na atazikwa kama balozi mstaafu. Sasa tabu yanini mzee huyu?! Binadamu wengine watambishia hadi mungu huko tuendako.
 
Naunga mkono hoja kwa sababu kwa sababu kuna siku nilikutana na Dr. Slaa akiwa na wife tukazungumza kidogo niliuliza kuhusu Eyre kugombea urais 2015, wife ndio alitoa msimamo fulani!. Kwa vile mazungumzo yale yalikuwa sio formal, nayaregard as off the record.
P
Pasco acha udaku,tutakuogopa hata tukikutana tutashindwa kuongea mambo ya kawaida tu,kwa kuogopa usije kuyatumia huku kama reference
 
Naunga mkono hoja kwa sababu kwa sababu kuna siku nilikutana na Dr. Slaa akiwa na wife tukazungumza kidogo niliuliza kuhusu Eyre kugombea urais 2015, wife ndio alitoa msimamo fulani!. Kwa vile mazungumzo yale yalikuwa sio formal, nayaregard as off the record.
P
Ni off record isiyo off record, nadhani kuna watu watahisi na kupatia nini kilizungumzwa kwenye hiyo "off record"!
 
Napingana kabisa na wanaodhani chanzo cha kuondoka Dr Slaa si ujio wa Lowassa Dr Slaa kama binadamu na kama kiongozi alikuwa na malengo, na ktk malengo yake lazima aishirikishe familia ili kuwa na mkakati wa pamoja, mikakati inayohusisha resources mbalimbali na ukizingatia maandalizi mengine yalisimamiwa na Chama chenyewe kwa mafunzo nje ya nchi. Mabadiliko ya ghafra hayamathiri Dr Slaa peke yake, yana athiri kwanza familia yake, mashabiki na marafiki waliounga mkono njozi zake na wawezeshaji waliomfadhiri kutimiza njozi zake. Kama hakuna mkakati wa kisaikolojia kuwaandaa hawa wote lazima wawe mbogo. Hivyo tukubaliane, chanzo cha yote ni mabadiliko ya ujio wa ghafra wa mtu mwingine na Slaa kuwekwa pembeni na taratibu zilizotumika.
 
Chadema mnapaswa kupambana na hali yenu sasa hivi chama hakieleweki, msimamo wenu haueleweki, ile list ya mafisadi mmeiondoa halafu mnahangaika na Dr. Slaa kwani wengi wenu mlitegemea baada ya kuondoka angedhalilika kumbe kuna watu waliona uwezo wake ndio maana sasa ana post ya ubalozi hali nyie mliotegemea Lowassa atashinda na kupata vyeo hamjaambulia chochote kwa kifupi mlicheza kamari na mkapoteza tulieni mpange mikakati mingine nani mtamshawishi kutoka CCM abebe bendera yenu maana hamna watu zaidi ya kutegemea waliotoka CCm
 
Sawa, tatizo ni kwamba Dr. Slaa mwenyewe alihusika katika kumkaribisha Lowassa na kulingana na watu wake wa karibu alishakubali maamuzi ya kikao. Kumbe huko nyuma first lady in waiting alishachora red line! Lakini tukiyaacha hayo nini hasa lengo la Dr. Slaa katika kutoa matamshi anayoyatoa hivi leo baada ya kuukwaa ubalozi? Kwa nini asichutame tu ale kivulini na kuacha kulikurupusha dude?
 
Chadema mnapaswa kupambana na hali yenu sasa hivi chama hakieleweki, msimamo wenu haueleweki, ile list ya mafisadi mmeiondoa halafu mnahangaika na Dr. Slaa kwani wengi wenu mlitegemea baada ya kuondoka angedhalilika kumbe kuna watu waliona uwezo wake ndio maana sasa ana post ya ubalozi hali nyie mliotegemea Lowassa atashinda na kupata vyeo hamjaambulia chochote kwa kifupi mlicheza kamari na mkapoteza tulieni mpange mikakati mingine nani mtamshawishi kutoka CCM abebe bendera yenu maana hamna watu zaidi ya kutegemea waliotoka CCm
Na yeye je, kama angeukwaa Urais angeweza kweli kumweka ndani huyo aliyemzawadia ubalozi kwa kufisadi nyumba za serikali kama alivyoahidi?
 
Hana ushawishi wowote kwa siasa za ndani.Bora huko nje labda kwa ugeni wao wanaweza kumuelewa, ulaji keshapata akatulie na mkewe sasa
 
Chadema mnapaswa kupambana na hali yenu sasa hivi chama hakieleweki, msimamo wenu haueleweki, ile list ya mafisadi mmeiondoa halafu mnahangaika na Dr. Slaa kwani wengi wenu mlitegemea baada ya kuondoka angedhalilika kumbe kuna watu waliona uwezo wake ndio maana sasa ana post ya ubalozi hali nyie mliotegemea Lowassa atashinda na kupata vyeo hamjaambulia chochote kwa kifupi mlicheza kamari na mkapoteza tulieni mpange mikakati mingine nani mtamshawishi kutoka CCM abebe bendera yenu maana hamna watu zaidi ya kutegemea waliotoka CCm
Hivi unadhani ni CDM tu wamuonea wivu Dr Slaa ?! Je wale CCM waliomtukana kipindi chote wanamtizamaje dr leo akiwa balozi ?!
 
Back
Top Bottom