Askofu Bagonza: Ukuu wa Katiba VS Ukuu wa Rais

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,015
TULIENI MIOYONI: Ukuu wa Katiba Vs Ukuu wa Rais.

Hoja ya Katiba Mpya pamoja na sababu nyingine nyingi, inalenga kupunguza au kuondoa mgongano wa hatari kati ya Ukuu wa Katiba na Ukuu wa Rais. Kwa hali ilivyo, Rais na Katiba wako vitani.

Nawasihi wanaojadili, watulize mioyo yao. Wasikilize kabla ya kusema na kama wakiweza, wasahau tofauti zao kwa muda wanapojadili suala hili. Nimesikiliza pande mbili na nina haya ya kushauri:

1. Tunaposema "Rais", msimwangalie SSH. Itazame taasisi ya urais. Hata SSH siku moja anaweza kujikuta ni mhanga (victim) wa maguvu yaliyo katika taasisi hii ya urais. Tumkumbuke Chiluba na Kaunda!

2. Tukisema Katiba Mpya, msitazame uzuri na ubaya wa Katiba iliyopo. Tazameni uzuri au ubaya wa Katiba inayodaiwa.

3. Katiba hii haikutuvusha salama wakati wa msiba. Tulivushwa na HEKIMA za watu na UVUMILIVU wa watanzania.

4. Hekima, uzuri, uvumilivu na utu wa watu ni vitu vinavyopita. Tusiwekeze sana katika hivyo. Tuviweke katika katiba mpya.

5. Rais (taasisi) tuliye naye ni Mkuu kuliko katiba hata kama ni katiba hii hii inayomleta madarakani. Ukuu wa Katiba hukoma pale inapomwingiza madarakani. Kinachobakia ni Ukuu wa Rais asiye mwanadamu wala Mungu. Ni hatari.

6. Anayevunja katiba hii anaweza pia kuvunja katiba mpya inayodaiwa. Tofauti ipo kwenye madhara ya uvunjaji wa Katiba. Mpya ije na madhara yasiyomtegemea Rais mvunjaji kujiwajibisha.

7. Wanaodai katiba mpya wako katika makundi matatu makuu:

a. Wanaosema ipitishwe katiba pendekezwa.

b. Wanaosema tuanzie Warioba alipoishia pale alipokabidhi kwa bunge.

c. Wanaosema tuanzie kwenye sheria inayoruhusu kuandika katiba mpya.

Yote yanatatulika kwa njia ya kuruhusu mjadala wa kitaifa. Hekima ziko nyingi zikiruhusiwa kufanya kazi.

8. Wanaopinga Wana makundi mawili makuu:

a. Katiba Mpya si sehemu ya ilani ya CCM.

b. Kuna mambo mengine muhimu zaidi ya kufanya kuliko hili.

9. Tukumbushane haya ili tuhairishe ubishi wetu kwa muda:

a. CCM si zaidi ya Katiba na si zaidi ya Rais hata kama anatoka CCM (alichaguliwa na watanzania).

b. Ilani ni nyenzo ya kutafutia kura, si Katiba ya nchi (iliandaliwa na CCM). Hapa tunazungumzia jambo kubwa, la watu wote waliopo na wajao, na jambo hili haliwezi kutatuliwa na chama chochote peke yake wala mtu mmoja peke yake. Tunazungumzia mustakabali wa nchi na Taifa letu.

10. Uchache au wingi wa wanaodai au kupinga, si hoja. Hata wengi hupotea. Hata wachache hukosea.

TULIENI MIOYONI na muiinue mioyo yenu tujadiliane.
 
Huyu, Sheikh Ponda, Askofu Mwamakula na yule Sheikh waliyekuwa wanasafiri naye pamoja na Lissu kwenye Kampeni za 2020 na Askofu Niwemuigizi nawapenda sana hawa Viongozi wa dini. Hawana UNAFIKI hata chembe bali wanajali maslahi ya Tanzania na Watanzania.

Tungepata maaskofu 8 kama huyu nchi ingepiga hatua sn
 
Wanaoenda kuswalishwa na huyo askofu punda wa ngada hawana akili wote.

Askofu haelewi hata kwamba Tanzania iliingia uchumi wa kati mapema zaidi kwa miaka 5.

Askofu haelewi hata kwamba kuna Corona na nchi nyingi zimekumbana na negative economic growth isipokuwa Tanzania.
 
Asiye mwelewa huyu Askofu simply ni Hayawani...akili yake kama ya Wanyama. Anasubiri kuswagwa uelekeo wowote ule ..
 
huyu askofu naye limbukeni tu, hana lolote..!!! sijui kwanini mpaka sasa hivi hajavuliwa hicho cheo cha uaskofu... badala ya kuwa kuhani wa kanisa kawa kuhani wa siasa... big shame
 
huyu askofu naye limbukeni tu, hana lolote..!!! cjui kwanini mpaka sahv hajavuliwa hicho cheo cha uaskofu... badala ya kuwa kuhani wa kanisa kawa kuhani wa siasa... big shame
Ukweli huwa unaumiza sana.
 
huyu askofu naye limbukeni tu, hana lolote..!!! cjui kwanini mpaka sahv hajavuliwa hicho cheo cha uaskofu... badala ya kuwa kuhani wa kanisa kawa kuhani wa siasa... big shame
Wanaodhani Watanzania tuna elimu waanze kujifunza kutokana na comments kama hizi! Ukiwa na watu wengi kama hawa hata mjadala wa Katiba inabidi tuache kwanza twende shule sambamba na kuanzisha chekechea ya watu wazima?
 
huyu askofu naye limbukeni tu, hana lolote..!!! cjui kwanini mpaka sahv hajavuliwa hicho cheo cha uaskofu... badala ya kuwa kuhani wa kanisa kawa kuhani wa siasa... big shame
Alisoma elimu dunia na theology,wewe ndio limbukeni hutakaa umwelewe Bagonza kama unaamini katiba za vyama kuliko KATIBA YA NCHI
 
Wanaoenda kuswalishwa na huyo askofu punda wa ngada hawana akili wote.

Askofu haelewi hata kwamba Tanzania iliingia uchumi wa kati mapema zaidi kwa miaka 5.

Askofu haelewi hata kwamba kuna Corona na nchi nyingi zimekumbana na negative economic growth isipokuwa Tanzania.
Uchumi wa kati!?😝😝😝😝
 
Back
Top Bottom