BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,376
- 8,118
Paul Makonda ni zaidi Katibu Mwenezi wa chama Tawala. Tumewahi kuwa nao wengi na wapo wengi wa vyama vingine. Hakuna kama Makonda uzuri na kwa ubaya. Kwa nini?
1. Kama Makonda ni tatizo basi halina suluhisho. Kwa sababu ndani ya chama tawala huyu ndiye ameonekana. Na kama huyu ndiye bora zaidi, waliobaki wana hali gani?
2. Kama Makonda ni dalili ya tatizo basi dalili huwa hazina tiba. Tusubiri ugonjwa wenyewe ndipo tujue tiba. Mgonjwa anayetetemeka kwa homa, kumfunika blanketi zito si kutibu ugonjwa. Ni kusaidia mayai ya vimelea yaanguliwe na mgonjwa atakuwa na hali mbaya zaidi.
3. Kama Makonda ni Suluhisho basi ni lile la “Bomoa yote tutajenga kesho”. Mchelea mwana kulia hulia yeye mwenyewe. Yeye amekuwa suluhisho zaidi ya dawa ya rangi mbili inayoua vimelea vyote mwilini.
AMESAIDIA SANA:
- Sasa tunajua hali yetu si njema. Hakuna utawala wa sheria wala wa mfumo.
- Sasa tunajua hasara za kukaa gizani. Ukikosa upinzani bungeni na mabarazani, ukakosa uhuru wa habari, ukakosa wana harakati huru, unastawisha CHAWA kila mahali.
- Sasa tunajua wananchi wanaona bora dikteta kuliko demokrasia, yaani bora shibe ya gerezani kuliko njaa ya uraiani.
- Sasa tunajua wenye shida wanataka mtu si taasisi wala mfumo.
- Sasa tunajua kila suluhisho linazaa tatizo. Ukifuga mbwa mkali wa kulinda wezi, kuna siku atakuzuia wewe usiingie nyumbani kwako.
- Sasa tunajua hakuna bunge huru, hakuna mahakama huru, hakuna DPP huru, hakuna AG huru - ila kuna Chama huru.
HEKIMA: Kuna mbwa akiwinda na kukamata mawindo, huwezi kumfukuza eti anaharibu ngozi. Atakula kitoweo chote na mwenye mbwa atakula mchicha siku hiyo.