samaki2011
JF-Expert Member
- Dec 17, 2013
- 1,775
- 468
Ngara. Askofu wa Jimbo Katoliki la Rulenge Ngara, Severin NiweMugizi ameungana na Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, Zachary Kakobe kupigia debe Serikali ya Tanganyika.
Akizungumza katika mahojiano ofisini kwake mwishoni mwa wiki iliyopita, NiweMugizi alitaka Serikali kutobeza maoni ya wananchi wanaotaka Serikali ya Tanganyika kwa kuwa muungano uliopo unaunganisha nchi mbili.
Kauli hiyo inarandana na ile iliyotolewa na Askofu Kakobe juzi wakati akitoa mahubiri ya Pasaka, aliposema anaungana na Watanzania wanaodai Serikali ya Tanganyika na kuahidi kuwapa ari na shauku ya kuhakikisha inapatikana.
NiweMugizi ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), alisema ukosefu wa elimu ya uraia kwa Watanzania wasomi na wananchi, ndiyo kikwazo cha kutetea uzalendo kwenye muundo wa Muungano.
Alisema katika miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, kumeibuka mambo mengi ya mpasuko wa umoja uliokusudiwa na waasisi wa kufanya mataifa mawili kuwa moja.
Alisema ili kuhakikisha Tanganyika inapatikana, lazima Serikali ya Jamhuri ya Muungano ikubali kuwa shirikisho, kwa kila nchi kupoteza baadhi ya mamlaka na masilahi ya taifa.
Huyu atakuwa ni askofu wa 37 kuumbua misimamo ya chama cha mafisadi
source - Mwananchi