Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 17,551
- 28,511
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Alex Gehaz Malasusa, amesema Kanisa limeshitushwa, kusikitishwa na kuumizwa kwa tukio la kushambuliwa na kujeruhiwa kwa Katibu Mkuu wa Baeaza la Maaskofu Katoliki Tanzania ( TEC), Pdri Dr Charles Kitima.
Askofu Malasusa alendelea kusema, jambo la Kusikitisha ni kuona Taifa linaendelea kushuhudia matukio ya kinyama yasiyostahili wanadamu wenye utu, kuyafanya dhidi ya mwanadamu mwingine.
" Kumvizia mtumishi wa Mungu kumetuumiza sana, si tu kwa vile ni mtumishi wa Mungu, lakini tunaona matukio haya yamevuka mipaka, ule woga na heshima imepungua sana" alisema Askofu Malasusa akizungumza na Upendo Media.