Askari Polisi wanafunzi 156 wafukuzwa mafunzoni

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,807
11,969
Capture.JPG

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amesema takribani askari Polisi wanafunzi 156 wamefukuzwa mafunzo ya kijeshi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo za utovu wa nidhamu na kufanya mambo ambayo hayakubaliki ndani ya shule ya Polisi

IGP Sirro amesema hayo wakati alipofanya ziara kwenye uwanja wa medani za kivita wilaya ya Siha, West Kilimanjaro katika Shule ya Polisi Tanzania, ambapo pia amewaelekeza wanafunzi hao wa kozi ya awali ya askari Polisi kufuata sheria, kanuni na taratibu za shule hiyo ikiwa pamoja na kudumisha nidhamu ndani ya Jeshi la Polisi.
FWahqITWQAAcOPI.jpg

FWahs2ZWAAEhkM7.jpg
 
Hao watakuwa sio watoto wa maafande maana walifanya makosa gani ambayo wenzao hawafanyi
 
Wawekeeni mazingira mazuri ya kazi na mboreshe mapato yao ili waachane na rushwa kwani polisi wanatia aibu...
 
Back
Top Bottom