Askari JWTZ auawa akijiokoa asibakwe

Askari JWTZ auawa akijiokoa asibakwe

Sio kwamba jamaa alikuwa anadai haki yake, kesi ikageuzwa juu kwa juu?
 
Wamejuaje kuwa alimkaba kwa ajili ya kumbaka, au walikuta ameishambaka tayari ila wameamua kupunguza ukali wa maneno kwa kamanda wetu??
Yaani ambaye anaamua kumkaba mwanajeshi hadi anamzidi nguvu unadhani hakumbaka, nawaza tu!!!

R.I.P Mwanajeshi wetu.Tumepoteza mtu muhimu sana
Kaligeuza lile neno kila upande kaanza ku-KABA na baadae aka-BAKA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tabora. Esther Gway, askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) ameuawa wakati akijinasua asibakwe na anayedaiwa kufanya kitendo hicho ni fundi ujenzi.

Fundi huyo inadaiwa alikuwa akijenga nyumba ya marehemu eneo la Kariakoo katika manispaa ya Tabora.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumatatu Januari 28, 2019 kamanda wa polisi mkoa wa Tabora, Emmanuel Nley amesema tukio hilo limetokea jana Jumapili Januari 27, 2019 saa moja usiku.

Kamanda Nley amesema kwamba mtuhumiwa alimvizia mwanajeshi huyo akiwa nyumbani kwake muda huo na kumkaba shingo kisha kumuangusha chini na katika purukushani za kutaka kumbaka huku akimkaba shingoni alisababisha kifo chake.

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi

Chanzo: Mwananchi
Mbona ameuawa kizembe sana?
Yaani mwanajeshi mzima alishindwa kupangua hiyo roba? Ni aibu sana kusema mwanajeshi tena wa JWTZ kapigwa roba na raia tu hadi kuuawa,wanajeshi wanafundishwa Combat Karate,jinsi ya kupigana na adui bila silaha,how comes azidiwe ?
Tena hiyo roba hata mimi nisiyejua Combat Karate ninajua tu Karate kawaida huwezi kunipiga roba hadi nikafa,ni lazima niipangue huku nikikuachia ulemavu wa kudumu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila kubakwa ni kitu kibaya sana!
Tena sana!
Yani mwanaume anakuwa ni mtu tena Bali mnyama!
Mwanamke usipojifunza kuliitia jina la Bwana ndo yaweza tokea hayo!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Halafu Jamani tuwe tunaambizana kwenye familia tusiwe na mazoea ya mtu kuishi peke yake kwa muda mrefu hadi mtu au watu wakakusoma na kukuchorea ramani ya uhalifu!
Angalia Yule bimkubwa juzi alouawa na houseboy wake!
Imeandikwa ni kheri kuwa wawili kuliko mmoja


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom