Askari JWTZ auawa akijiokoa asibakwe

Askari JWTZ auawa akijiokoa asibakwe

Wamejuaje kuwa alimkaba kwa ajili ya kumbaka, au walikuta ameishambaka tayari ila wameamua kupunguza ukali wa maneno kwa kamanda wetu??
Yaani ambaye anaamua kumkaba mwanajeshi hadi anamzidi nguvu unadhani hakumbaka, nawaza tu!!!

R.I.P Mwanajeshi wetu.Tumepoteza mtu muhimu sana
 
Tabora. Esther Gway, askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) ameuawa wakati akijinasua asibakwe na anayedaiwa kufanya kitendo hicho ni fundi ujenzi.

Fundi huyo inadaiwa alikuwa akijenga nyumba ya marehemu eneo la Kariakoo katika manispaa ya Tabora.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumatatu Januari 28, 2019 kamanda wa polisi mkoa wa Tabora, Emmanuel Nley amesema tukio hilo limetokea jana Jumapili Januari 27, 2019 saa moja usiku.

Kamanda Nley amesema kwamba mtuhumiwa alimvizia mwanajeshi huyo akiwa nyumbani kwake muda huo na kumkaba shingo kisha kumuangusha chini na katika purukushani za kutaka kumbaka huku akimkaba shingoni alisababisha kifo chake.

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi

Chanzo: Mwananchi
Ni nani amesimulia kisa hiki?
Kuna aliyeshukudia mtiririko huu wa matukio?
 
Marehem apumzike kwa amani
IMG-20190127-WA0004.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom