TABORA: Askari JWTZ auawa baada ya kupigwa fimbo na wafugaji

Pistol

Senior Member
Oct 13, 2015
194
86
Watu watatu wameuawa kwa nyakati tofauti mkoani Tabora akiwemo Askari wa Jeshi la wananchi wa Tanzania, (JWTZ)aliyepigwa fimbo na wafugaji akiwa katika ujenzi wa nyumba yake, baada ya kuwalalamikia kuwa, ng’ombe wamevamia katika kiwanja chake na kuharibu vitu mbalimbali vya ujenzi.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari mkoani Tabora Kamanda wa polisi mkoani humo ACP Hamis Issa Suleiman, amemtaja marehemu kwa jina la Carritus Mkunozi (35) wa kikosi cha 212KJ, ambapo ugomvi ulitokea baada ya kupishana kauli na wafugaji,na ugomvi kuanza, ambapo alifariki akiwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tabora Kitete muda mfupi,akipata matibabu.

Aidha amesema kuwa katika tukio hilo kundi kubwa la ng’ombe zaidi ya mia mbili,waliokutwa katika kiwanja cha marehemu huyo wanashikiliwa, na muuaji mmoja, huku akiwataja marehemu wengine, waliouawa kuwa ni mama mmoja,mganga wa kienyeji aliyepigwa fimbo kichwani baada ya kuwapa kisogo wauaji waliokuwa wamemwomba maji ya kunywa.

Katika hatua nyingine Kamanda Hamisi Issa Suleiman amesema huko kata ya kijiji cha Motomoto Vumilia wilayani Urambo kijana mmoja kibarua ambaye hakufahamika alipigwa ngumi kifuani na kufariki papo hapo, wakati wakigombea mgao wa posho ya kazi yao.

Chanzo: ITV
 
Pole yao hawa wafugaji ngoja moto uje sijui kama wataweza kuuzima watafute pakwenda siyo tanznia.
 
Inafika hatua Jeshi inabidi lirudi katika misingi yake ukauzu na kutochekea raia maana hawa watu wanaanzaga hivihivi kwenye taasisi zingine sasa wakifikia kuchezea sehemu ya jeshi na kuona hakuna reaction yoyote ipo siku watajitangazia uhuru wao kwa kuamini Jeshi haliwawezi.
Ubabe wa Jeshi letu hauepukiki kwa matukio kama haya Pumzika kwa Amani Askari wetu.
 
hao wasubiri kuja kupgwa INTRO maana shughuli ya hao jamaa ni shida. R.I.P mjeda ila kiukwl kwa sasa mauaji ya kiraia yamezidi sana. wananchi tumrudie mwenyezi Mungu.
 
Masakata ya wakulima na wafugaji ni Mengi..... na Mara zote jamii moja huenda kuchokoza jamii nyingine..... Labda sasa baada ya tukio hili hatua zinaweza zikaanza kifuatwa
 
Back
Top Bottom