Askari afariki kwa ajali Siha

Askari afariki kwa ajali Siha

RIP Afande

Kesho wenzako waende kwa lengo la kusaidia Raia na sio kupiga, kushika, kufunga etc raia.

Fundisho tu
 
Dah!Inasikitisha sana kwa kweli,R.I.P mdogo wetu poleni mlioumia,lakini ndiyo hivyo Mungu huwa ana makusudi yake. Comments za wanajukwaa ni kutokana na matendo wanayotufanyia maaskari,siku hizi ni heri ukutane na majambazi kuliko askari,maaana kazi zao sasa zinafanana tena maaskari wamekuwa zaidi.Kwa kweli nimeandika haya maneno kwa unyonge sana,tukimbilie wapi??Maisha gani mazuri waliyonayo maaskari mpaka watuue??
 
mwenzio alienda ffu na wewe uko wapi??
Rest to Hell (RTH) Maliyatau umekufa kwa kujitakia.

MI NIPO HAPA JF KWANI HUNIONI?.bro u can't have that much hatred kwa mtu aliyekuwa anatimiza wajibu wake kwa ajili ya familia yake.kuwa na mtazamo tofauti kuhusu kazi ya mtu na jinsi mfumo wa kazi yake unavyofanya kazi.ile ni ajira kama zilivyo ajira zingine lakini kwa uelewa wako finyu unadhani police huwa wanajiamulia mambo wanayo yafanya.ni kama wewe ukatae kufuata maagizo ya bosi wako,unategemea hapo kutakuwa na ajira tena?anapoambiwa piga anapiga kwa kuwa anafuata maelezo ya mabosi wao na sio utashi wao.hata wao wanajua kuwa wanaowapiga ni mama zao,baba zao,kaka zao,wadogo zao,mashangazi zao,wake zao,jirani zao lakini kwa kuwa ndivyo wanavyoamriwa inakuwa haina jinsi.binafsi nachukia sana matendo yanayofanywa na jeshi la police na majeshi mengine pia lakini simchukii mtu mmoja mmoja kwa kuwa asipofanya kama anavyoelekezwa hataweza kuishi kwani atapoteza kazi yake na ukizingatia uhaba wa ajira tanzania hii jinsi ulivyo.kuna watu wengi sana wameingia kwenye hizi kazi za majeshi sio kwamba kwa sababu wanazipenda,hapana ni kwasababu hawana option.asipofanya hiyo ataenda wapi?plz nisaidie kumuombea OB wangu MALIYATABU APUMZIKE PEMA PEPONI.nilikuwa nae almost 7yrs ago lakini kwa kijana kupoteza maisha kwa wakati huu ni pigo kubwa sana,naumia sana kusikia hataweza kufumbua macho tena.
 
Nakumbuka ile kauli ya PM ''Nasema wapigwe tu maana tumechoka"

1.jpg


ASKARI mmoja wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) Mkoani Kilimanjaro, Fidelis Mwaliyatabu, amefariki dunia papo hapo na wengine tisa akiwamo Mkuu wa Kikosi hicho kujeruhiwa vibaya baada ya gari lao kupinduka katika kijiji cha Kilingi, wilaya ya Siha, wakati wakienda kuzima vurugu za wananchi.

Ajali hiyo ilitokea wakati kikosi hicho kikielekea katika kijiji cha Karansi kwa ajili ya kukabiliana na wananchi waliokuwa wakiandamana kupinga wenzao waliokamatwa usiku wa manane baada ya kuvamia mashamba mali ya Shirika la Roho Mtakatifu-Kilasara.

Taarifa kutoka kijijini humo zilieleza kwamba wanakijiji waliamua kuandamana baada ya wenzao watano kukamatwa na Jeshi la Polisi nyakati za usiku kwa mahojiano kutokana na kukabiliwa na tuhuma za kushawishi wanakijiji wenzao kuvamia maeneo ya Shule ya Kilasara na kusababisha hasara kubwa kwa shule hiyo.

Kufuatia kukamatwa kwa watuhumiwa hao, wanakijiji waliamua kuaandamana hadi katika kituo cha polisi ili kuwatoa wenzao hali ilisababisha jeshi hilo kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya, jambo ambalo lilishindikana kutokana na wingi wa watu walikuwa wanaandamana.

Inadaiwa kuwa wananchi hao walijikusanya na walianza kuandamana kuanzia majira ya saa 7 usiku kuelekea kituo cha polisi ili kuwatoa wenzao walikuwa wanashikiliwa.

Wananchi wanaoshikiliwa na jeshi hilo ni John Sokoine, Abeli Solomoni, Christopher Solomon na aliyetambuliwa kwa jina moja tu la Julius. Wote walikamatwa usiku wa kuamkia jana.

Mnamo Juni 11, mwaka huu majira ya mchana wananchi wa kijiji hicho walivamia eneo lenye ukubwa wa hekta mbili na kufyeka mazao mbalimbali yaliyokuwa shambani hapo kwa madai kuwa wamiliki wa shule hiyo wamechukua eneo hilo kinyume cha taratibu.

Kwa upande wake, Mkuu wa Shirika la Roho Mtakatifu, Kanda ya Afrika, Padri Jerome Okama, aliushutumu uongozi wa kijiji hicho kwa kuvifumbia macho vitendo vya wananchi kujichukulia sheria mkononi wakati wakitambua kuwa eneo hilo lenye ukubwa wa hekta 8.9 linamilikiwa na shirika hilo kihalali.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Robert Boaz, akizungumza na NIPASHE kwa njia ya simu kutoka wilayani humo jana jioni, alisema askari hao walipata ajali hiyo majira ya saa 6.45 mchana katika kijiji cha Kilingi nje kidogo ya mji wa Sanya Juu.

Alisema askari hao wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC na wengine wamelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Ugonjwa wa Kifua Kikuu ya Kibong'oto ilioyopo wilayani Siha na kwamba watano kati yao hali zao ni mbaya.

Alitaja gari la Polisi lililopinduka na kuua kuwa ni Toyota Land Cruiser lenye namba PT 2070 lililokuwa likiendeshwa na Sajenti Herman Dancan. Chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi na kuacha njia na kupinduka.

Aliwataja waliojeruhiwa katika ajali hiyo kuwa ni Mkuu wa FFU mkoani hapa, ASP Nonino, Renatus Misigalo, Alfonce Joseph, Koplo Elifuraha Lenare, Peter Albert, Bashiri Yusuph, George Mwakyusa na Gaspar Mwapunda.

Alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Kibong'oto.

 
Safi sana yaendelee kufa tu, tumeyachoka na yatakufatu..., yakishindwa tutayauwa tu...
 
R.I.P. Green Guard Mwaliyatabu

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Sasa kulikuwa na sababu yakwenda mwendo kasi kuwahi watu waliokuwa wanandamana! si wangeenda polepole wangewakuta, au ndo ajali haina kinga! poleni wafiwa.
 
Mungu kawaua watesi wa wananchi!!!!Naunga mkono kifo hicho ni sawa kifo cha mnyama mbaya aitwaye fungo ambaye hunya sehemu mmoja maishani mwake...Mungu mkubwa katulipia kisasi
 
R.I.P. Green Guard Mwaliyatabu

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums

Natamani wangekufa wote, hawanamaana wanapokea hata amri ambazo sio sahihi, kwanini wasitafute suluhisho la amani, wao ni mababu tu, Hibi huwa hawakumbuki kama na wao wanaishi uraiani
 
Natamani wangekufa wote, hawanamaana wanapokea hata amri ambazo sio sahihi, kwanini wasitafute suluhisho la amani, wao ni mababu tu, Hibi huwa hawakumbuki kama na wao wanaishi uraiani

Mkuu taratibu, sipendi jamaa wanavyo operate lakini hii ya kuwaombea wafe wote nadhani haijakaa vizuri sana. Be blessed
 
Mkuu taratibu, sipendi jamaa wanavyo operate lakini hii ya kuwaombea wafe wote nadhani haijakaa vizuri sana. Be blessed

Yaani ni huzuni kwa wafiwa na majeruhi pamoja na ndugu.

lakini kwa kuwa Majeshi yetu wanakubali kutumiwa kisiasa, "NASEMA TUMECHOKA, NA WAFE / WAUMIE TU. MWENYEZI MUNGU AWAPUMZISHE KWA AMANI MAREHEMU NA MAJERUHI SISI WANANCHI TUMECHOKA"

Kwa kuwa walikuwa wanatimiza amri ya jamaa "MIMI NASEMA WAFE WOTE TU............." KWANI NI WANGAPI WANANCHI WAMEKUFA KUTOKANA NA HAWA JAMAA KUPOKEA AMRI TOKA JUU????

hapo wakifika wao hawaulizi chochote ni kupiga virungu na mabomu tu.



MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!!
 
Mkuu Samaritan waangalie hawa, jinsi wenyewe walivyokosa ubinadamu:-


View attachment 103936


View attachment 103937

Je, hata wewe umkute ndugu yako anaadhibiwa kinyama hivi, utaendelea kuwapenda hawa watu??

Kazi yao ni kulinda amani lakini wao wanaharibu amani.



MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Last edited by a moderator:
Mungu kawaua watesi wa wananchi!!!!Naunga mkono kifo hicho ni sawa kifo cha mnyama mbaya aitwaye fungo ambaye hunya sehemu mmoja maishani mwake...
Hahaha, JF kiboko, kuna mnyama mwenye sifa hizo kweli?
 
Back
Top Bottom