Elections 2010 Asiyefunzwa na mamaye atafunzwa na ulimwengu ni tusi?

Sijaona tatizo katika matumizi ya maneno hayo labda inaonekana ni matusi kwa kuwa tu yametamkwa na mgombea wa upinzani.
Mbona jana JK kasema watu MAJUHA sijaona mtu wa kumkamata?
 
Usemi hauna shida kwani ni kawaida ya binadamu unapokuwa kwenye sehemu kama zile kusema manane kama yale kwani inauma sana kwa jinsi mambo yanavyokwenda. Na hasa unapojiweka wewe kuwa ningefanya maamuzi ambayo huyu anashindwa?

Hivyo huyu mbunge kutegeme unaangalia upande gani unaweza kumlaumu na unaweza pia kumsifu kuwa amesema kweli yake hajatukana. Maneno alityotumia niya kawaida sana kwenye jamii. Hila kwa upande mwingine ni wasted maana sasa wamepata cha kusemea kwani walikuwa wameshabanwa mbavu ingeendelea hivyo hivyo ingekuwa poa. Hakuna kuomba msamaha let him go to court and the judge will decide and i hope on his favour.
Msisahau kwenda kupiga kura jumapili. Hii yote ni janja ya wanasiasa kuwachota mawazo yenu na kuyahamishia upande mwingine. Jamaa anataka kura za huruma kutoka kwa watanzania.
 
Mi naona CCM wanaanza kuandaa Zengwe ili mambo yakienda tofauti waanze kutoa Visingizio na kuhadaa umma wa Watanzania
 
Kwani nini hakieleweki hapa ndg zangu? Hawa jamaa wanajua kuwa hakuna kesi hapa, ila wanachofanya ni kulialia kwa wananchi kupitia vyombo nya habari, ili kuichafua CHADEMA. Mnaona kuwa hata kupitia gazeti lao la Habari leo wameamua kudanganya kuwa TBC ilibidi wakate matangazo eti 'kustahi ustaarabu wa mtanzania'. Inafahamika kuwa TBC hawakukata matangazo, hayo wanayoyaita matuis ya nguoni yasiweza kuandikika katika vyombo vya habari nayo ni uongo. Wanachofanya ni kuwaaminisha wananchi ambao hawakusikia hotuba ile kuwa CHADEMA walitukana kweli. Na huko mitaani wanawatumia mapropagandist wao wapakaze kuwa CHADEMA walitukana matusi ya nguoni.

Lakini tuwaulize, tusi la nguoni pale ni lipi? Kusema kuwa mtu hana adabu, au kusema kuwa hakufunzwa na mamaye.... Hebu watu wajichungulie ndani ya nguo zao waone kuna nini, ndio wajue tusi la nguni linafananaje...
 
Jana Kikwete yeye alifanya nini pale Membeyanga hapa nimequote gazeti tiifu la serikali Habari Leo, la Leo kama linavyosomeka kwenye mtandao.

Wamechanganyikiwa, ndio maana wanachoma watu visu, wanaua. Haki ya Mungu tuna kazi kweli, hawa bado darasa halijawaingia, endeleeni kuwasomesha.

“Wamekuwa kama wamesomewa albadir bayana. Hujafa hujaumbika, na bado tutaona mengi. Mkataeni ili achanganyikiwe, akivua nguo atapelekwa Mirembe,” alisema Rais Kikwete na kushangiliwa kwa vifijo na wananchi.

Sasa haya si matuzi kwa watu waungwana? Kwanza alibadir bayana ni maana gani? sisi hatukufundishwa hili neno

 
Katika suala la matusi mimi si shabiki hata siku moja, kwa yeyote alimsikia yule mgombea wa chadema live pale mwembeyanga yale ni matusi na anaweza kukiharibia chama chake kukosa kura za watanzania wapiga kura za mlengo wa upande wa ustaarabu. John Mnyika na Anna Maulida Komu wanasitahili pongezi kwa kumiliki jukwaa vizuri na kuushawishi uuma kwamba hawako kwenye siasa kwa ajili ya matusi bali kujenga hoja zenye mantiki ya kuvuta hisia ya mpiga kura.Tutakuwa tunafanya makosa makubwa kwa mustakabari wa taifa letu tukifikiri kwamba siasa ni matusi, na hii si kwa sababu alimtukana Kikwete mgombea wa CCM bali hata angaekuwa ni mgombea wa chama chochote...TLP, NCCR, CUF n.k

Kusema kikwete hakufunzwa na mama yake mzazi wakati mama wa mgombea huyo alishakufa ni suala lisilokubarika na linaweza kukumbusha kifo cha mama ya mtu si uungwana

Mimi binafsi sitashangaa sana kama huyu bwana atafunguliwa mashitaka.
 
Dr Feki Kamala amesema ''Dr Slaa ni mbumbumbu wa uchumi''...hajakamatwa tu?

Chadema nao wana haki ya kushitaki kama wanaona wametukanwa kwani hiyo haiondoi kosa la mgombea wa chadema kumtukana wa CCM. Two wrongs don't make one right, kwa kiswahili kibovu....Makosa mawili hayafanyi kuwa kosa moja lililo sahihi. Tuhukumu kila kosa kwa hoja zake. Usije kwenda mahakamani/kizimbani ukamwambia hakimu kwamba, mheshimiwa hakimu niliamua kumwibia ng'ombe bwana X aliyenishitaki baada ya hapo awali yeye kuniibia mbuzi wawili.
 
Vry funny indeed, shamte na akina kikula wametuma meseji za uchochezi kwa taif zima, wana-roll na utility vehicles... aleyerejea msemo wa kiswahili temeke, anatiwa ndani

African democracy at its best!!!
 
huyo jamaa natakiwa kuomba radhi hadhrani ili kukisafisha chama, mbona jaji tendwa alikosea na kuomba radhi hadharani na mambo yakaisha. We have to be grown ups. we want serious politics and not wasting time and resources.

Utaomba samahani bila kufanya kosa?
WEWE NI PANDIKIZI LA CCM NA UKOO WENU NI MAFISADI... NAKUJUA GABACHORI MKUU WE!!
 
Kama unakumbuka jk alivyo kuwa lindi na Mtwala aliwatukana wapinzan eti ''watu wazima hovyo''pia aliwatukana waathirika wa ukimwi kwamba nikihelehele chao, sasa kwanini mtukama huyo asiambiwe hakufunzwa na mamaye tabia njema?
 
Nadhani ndugu zangu wapenzi wa ccm na hasa polisi wetu kwa kutojua sheria na kuzingatia kanuni na maadili ya kazi zao mara nyingi wamekuwa wakilitukanisha jeshi la polisi kwa umma. Wameshindwa kujua nafasi yao katika mchakato wa siasa. Ndio maana kule maswa polisi ocd anapigwa na kudhalilishwa tena akiwa ofisini kwake na wanashindwa kuchukua hatua stahili kisa mhalifu ni kada wa chama tawala. Hii ni hatari sana kwa ustawi wa nchi kama yetu. Kama chama tawala wanawapiga polisi na hakuna hatua zinazochukuliwa,je nani atawaheshimu polisi wasiojua wajibu wao? Polisi kazeni buti blia kujali mhalifu ni mwanachama wa chama gani vinginevyo wahuni wote wataingia ccm ili wakiwapiga mshindwe kuchukua hatua.

Mie nawashangaa sana hawa CCM, jana Mrisho J.K kawadharau wanamageuzi hajafanywa chochote, Hadija Kopa nae kamkashifu Dr. Slaa lakini Selemani Kova hajasema chochote.

Kila siku Yusuph Makamba anatoa kauli za hovyo kabisa na manager wa kampeni Abdulhaman Kinana hakemei kabisa yeye analalamika tu CCM wanaposemwa.

Mie nafikiri mkuu wa jeshi la polisi ndugu Said Mwema anatakiwa awe makini sana na mambo haya.
 
"wanaopata Ukimwi ni kiherehere chao' J.Kiwete mwisho wa kumnukuu, ananyanyapaa waathirika je anatufaaa huyu
 
Kumbe kikwete hakubali kwamba kiswahili ni lugha ya taifa.
Lakini hata akiwa ndani huyo komredi wetu tutampa kura zoote za ndiyo
Hayuko ndani, alihojiwa na kutoka jana hiyo hiyo,, amedhaminiwa na mkurugenzi wa kampein.
 
Hivi Kipenzi Chetu JK kwanini meweka picha ya Mama yake kwenye kampeni zake? halafu watu wakiongea kwa kumtaja mama anaona ametukanwa? hajui shillingi ina pande mbili , kumtumia mama kuna faida yake na pia kuna hasara zake, kama vile kumtumia mkewe au watoto, au pesa
 
MIMI NAKUMBUKA NIKIWA SHULE YA MSINGI NILIFUNDISHWA NA WALIMU WANGU KUWA "ASIYEFUNTHWA NA MAMAYE HUFUNTHWA NA ULIMWENGU" AU HIYO METHALI IMEBADILIKA WAJAMENI??????????????????????????????? NGOJA NIPERUZI KUJUA KAMA KUNA MABADILIKO KTK METHALI HII. :A S-coffee:
 
Mbona ni kweli kikwete kawakosea adabu watanzania kwa kuanza na kauli mbiu ya maisha bora kwa kila mtanzania na kuamua kuikimbia?
 
Back
Top Bottom