Asiyefunzwa na mamaye atafunzwa na ulimwengu ni tusi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Asiyefunzwa na mamaye atafunzwa na ulimwengu ni tusi?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by silver25, Oct 28, 2010.

 1. silver25

  silver25 JF-Expert Member

  #1
  Oct 28, 2010
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 744
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aliyemtusi JK mbaroni

  [​IMG]
  LABDA WATU HAWAJUI METHALI...

  """POLISI Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, imemtia mbaroni mgombea ubunge jimbo la Temeke kwa tiketi ya CHADEMA, Dickson Ng’hili, kwa tuhuma za kutumia lugha ya matusi dhidi ya mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Rais Jakaya Kikwete. Ng’hili (33), mkazi wa Mbezi Jogoo, alikamatwa jana, ikiwa ni siku moja baada ya kudaiwa kutoa maneno hayo katika mkutano wa kampeni wa chama hicho, uliofanyika katika viwanja vya Mwembe Yanga, wilayani Temeke. Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo, Suleiman Kova, alisema Ng’hili alikamatwa jana saa nne asubuhi, eneo la Temeke.

  SOURCE: UHURU: Wednesday, 27 October 2010 21:27 ""

  LABDA UPEO WANGU WA KUFIKIRI MIMI NI MDOGO,, NINACHOJUA MIMI "" ASIYEFUNZA NA MAMAYE ATAFUNZA NA ULIMWENGU"" NI MANENO AMBAYO BABUZETU HUTUMIA KAMA METHALI,, AMBAZO HUSAIDIA KUWAASA WATU MBALIMBALI AMBAO WANAKWENDA KINYUME NA MAADILI YA JAMII YAO..

  SASA SIJUI NI TUSI GANI AMBALO NG'hILI ALIMTUKANA KIKWETE PALE TEMEKE???
   
 2. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #2
  Oct 28, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Kumbe kikwete hakubali kwamba kiswahili ni lugha ya taifa.
  Lakini hata akiwa ndani huyo komredi wetu tutampa kura zoote za ndiyo
   
 3. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #3
  Oct 28, 2010
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,214
  Likes Received: 316
  Trophy Points: 180
  Methali sio tusi. Penye UHURU WA KUSEMA (freedom of speech) hawawezi kumkamata mtu (tena MGOMBEA WA UBUNGE) kwa kutumia uhuru wake wa kusema.

  Suleman Kova kakubali kutumia ofisi yake KIFISADI. Itabidi awajibishwe nchi ikishakombolewa toka kwa mfisadi wenzake.

  Ila wanaopigania wananchi na kupata ushindi wakiwa jela la waonevu wanapata heshima sana katika Historia ya nchi. Ni kama Mandela. Mbunge Mtarajiwa asijali. He is on the right side of History.
   
 4. c

  chamajani JF-Expert Member

  #4
  Oct 28, 2010
  Joined: Sep 22, 2010
  Messages: 554
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Silvia acha ushabiki usio na tija kwa taifa, pamoja na kuwa kura yangu ntaipeleka kwa DR...?? lakini yule jamaa kachemka na ikibidi akanwe na Chadema hadharani kwani inaonyesha kama ni pandikizi anayekusudia kuiangamiza chadema ionekane kama Chama cha theolojia na matusi (CHATHEMA). Otherwise-Hasira za Mkizi, ni Tijara kwa Mvuvi!
   
 5. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #5
  Oct 28, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,648
  Likes Received: 4,754
  Trophy Points: 280
  Huyu JK sijui tumkumbushe yale ya ZE UTAMU !!!!!
   
 6. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #6
  Oct 28, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Ngoja tudadavue, Je hapo tusi ni lipi? ASIYEFUNZWA AU NI MAMA AU NI ATAFUNZWA AU NI ULIMWENGU????
   
 7. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #7
  Oct 28, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,860
  Trophy Points: 280
  Kwani mamaye Kikwete alimfunza Siasa? Si ulimwengu ndio umemfunza kuwa bila mafisadi mambo hayaendi....yule Mama nimemwangalia sana leo asubuhi katika ile picha yake pale Kenyatta Drive Junction haelekei kujua ufisadi kabisa....huyu bwana kweli kafunzwa na ulimwengu na sio na mamaye....alitakiwa kuishukuru hii methali ambayo inatumika kila siku mpaka makanisani
   
 8. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #8
  Oct 28, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  na yeye jana si katukana kwa kita mikutano ya chadema ni mikusanyiko ya majuha

  hili ndo tusi sasa tena kubwa sana
   
 9. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #9
  Oct 28, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Jamani hili suala la maneno ya wanasiasa lilishawekewa msimamo na marehemu Jaji Mwalusanya kwenye kesi ya Mtikila kuwa statements kenyr mikutano sio uchochezi Ona Rev Chistopher Mtikila & 3 Others Versus AG Civil Appeal No 90 of 1992 Dodoma Registry naomba ninukuu kwa faida yetu, hasa Bwana Kova

  " the trial Magistrate in his Jugdment very briefly stated that " to call a president of a country a thief and to say "chama cha majambazi" for CCM was very revolting and likely to cause a breach of peace. However I think he missed the point, as the issue here is not whether the Magistrate thinks the abuses and insults are very revolting or slightly revolting, but as to whether the insults were likely to lead ordinary and reasonable men to feel the words are revolting and thus incite them to cause a breach of peace".

  Jaji akamalizia:

  " it is difficult to accept that the politicaf harangues given by the 1st appellant amounted to abuses and insults. The audience were given an opportunity to choose the grain from the chaff"

  KOva soma sheria usikurupuke.
   
 10. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #10
  Oct 28, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,860
  Trophy Points: 280
  Na haya ni matusi yake mengine
  • Upinzani ni fotokopi
  • upinzani ni pumba na CCM ni mchele
   
 11. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #11
  Oct 28, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 419,846
  Trophy Points: 280
  Hawa watu wa CCM na serikali yao wamepagawa hawaelewi kinachoendelea...................Huo ni usemi na kamwe haliwezi kuwa ni tusi.............
   
 12. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #12
  Oct 28, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  na kuwaita watumishi "mbayuwayu" ni sifa au tusi? chichiem, waache hizo.
   
 13. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #13
  Oct 28, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,526
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Kova unaweza kudefine tusi? Huu si msemo wa kila siku kwa wanadamu au Jk sio mwanadamu bro? Kama na hilo hulijui basi soma hukumu hapo juu japo imeandikwa kwa umombo. Unaweza kumtafuta mkalimani wako akutafsirie
   
 14. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #14
  Oct 28, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  kuna jamaa anaijiita dr. kamala (sijui udokta aliupata wapi????? ukisikia anavyoongea utabaki unashangaa eti huyo ndiye waziri wa afrika mashariki) naye alitoa maneno siyo mazuri kwa Rais wetu Mtarajiwa Dr. Slaa. Chadema fuatilieni kauli mbalimbali zilizotolewa na wagombea wa chichiem ili nanyi mtoe kama ushahidi. wasije wakatutibulia dakika za mwisho za kuikomboa nchi yetu.
   
 15. tempo_user1

  tempo_user1 Senior Member

  #15
  Oct 28, 2010
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  JK ameuita mkutano wa Chadema kwamba ni mkusanyiko wa majuha, vyombo vya habari na vya usalama vimekaa kimya, mbona rais wanchi anatukana watu hadharani?
   
 16. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #16
  Oct 28, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kwa bahati mbaya sikuweza kuhudhulia mkutano huo, lakini kama huyu mgombea amesema Kikwete hakufunzwa na mamaye ni tusi basi tumekwisha. Wanaowapiga walinzi wetu tunaambiwa sawa sawa, tukiambiwa sisi ni majuha tunapokwenda kuwasikiliza mashujaa wetu, kwa matukio haya yote sishangai kusikia kuwa nchi hii itaingia kwenye migogoro.

  Migogoro yote huanza pale ambapo vyombo vya usalama na vya haki vinapokuwa na sheria zaidi ya moja kwa watu wake, Rwanda na Burundi wameuana kutokana na dhambi hii. Watusi wanaweza kufanya watakalo bila wasiwasi, lakini Mhutu akifanya lolote anakiona cha mtema makuni. Wahutu walipochoka waliamua kulipiza na kisasi cha uonevu ndicho kitaingamiza nchi hii kama hili kundi lililo nyuma ya CCM litaendelea kushika hatamu na udanganyifu katika kura
   
 17. M

  Mwavilenga Member

  #17
  Oct 28, 2010
  Joined: May 13, 2010
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani ndugu zangu wapenzi wa ccm na hasa polisi wetu kwa kutojua sheria na kuzingatia kanuni na maadili ya kazi zao mara nyingi wamekuwa wakilitukanisha jeshi la polisi kwa umma. Wameshindwa kujua nafasi yao katika mchakato wa siasa. Ndio maana kule maswa polisi ocd anapigwa na kudhalilishwa tena akiwa ofisini kwake na wanashindwa kuchukua hatua stahili kisa mhalifu ni kada wa chama tawala. Hii ni hatari sana kwa ustawi wa nchi kama yetu. Kama chama tawala wanawapiga polisi na hakuna hatua zinazochukuliwa,je nani atawaheshimu polisi wasiojua wajibu wao? Polisi kazeni buti blia kujali mhalifu ni mwanachama wa chama gani vinginevyo wahuni wote wataingia ccm ili wakiwapiga mshindwe kuchukua hatua.
   
 18. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #18
  Oct 28, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  huyo jamaa natakiwa kuomba radhi hadhrani ili kukisafisha chama, mbona jaji tendwa alikosea na kuomba radhi hadharani na mambo yakaisha. We have to be grown ups. we want serious politics and not wasting time and resources.
   
 19. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #19
  Oct 28, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  :A S angry:
   
 20. M

  Mugerezi JF-Expert Member

  #20
  Oct 28, 2010
  Joined: Mar 28, 2007
  Messages: 454
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Usemi hauna shida kwani ni kawaida ya binadamu unapokuwa kwenye sehemu kama zile kusema manane kama yale kwani inauma sana kwa jinsi mambo yanavyokwenda. Na hasa unapojiweka wewe kuwa ningefanya maamuzi ambayo huyu anashindwa?

  Hivyo huyu mbunge kutegeme unaangalia upande gani unaweza kumlaumu na unaweza pia kumsifu kuwa amesema kweli yake hajatukana. Maneno alityotumia niya kawaida sana kwenye jamii. Hila kwa upande mwingine ni wasted maana sasa wamepata cha kusemea kwani walikuwa wameshabanwa mbavu ingeendelea hivyo hivyo ingekuwa poa. Hakuna kuomba msamaha let him go to court and the judge will decide and i hope on his favour.
   
Loading...