Asitisha huduma ya usafiri baada ya kushindwa ubunge

Basi mbunge mpya ana haki ya kukataa kutoa huo msaada.

Watajua mbunge, serikali na wananchi jinsi ya kushughulikia matatizo. Murji wala hausiki kabisa labda aamua kusaidia tu kama mimi na wewe tunavyoweza kufanya hivyo kwa jamii zetu
 
ile ambulance ilikuwa mbovu, sasa unatoa msaada wa pajero kuku, ipo imepaki juu ya mawe mwambieni aje na breakdown ya khimji aikokote.

Mlipewa mkaharibu so mlitaka awe anawatengenezea?! Watu wa kayenze bana!
 
Ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Firauni,Bukoba Mbunge aliyebwagwa na nguvu ya Umma Hamis Kagasheki amenyang'anya ambulance aliyokuwa amekabidhi katika Hospitali ya Mkoa na kisha akang'oa dish na TV kubwa aliyokuwa ameweka katika Uwanja wa Mayunga kwa ajili ya wananchi kutazama taarifa za Habari na Vipindi Muhimu.Aidha ameng'oa mitego ya radi (Vifaa vinavyozuia madhara ya radi) iliyokuwa imefungwa maeneo ya Miinuko.Pia kwa hasira kuu amewanyang'anya vijana woote aliokuwa amewapa mikopo ya bodaboda baada ya kushindwa kwa kishindo kikuu na mpinzani wake wa muda mrefu Ndugu Lwakatare...

kanda ya ziwa sijui wabunge wetu wana vielement vya ukichaa yaani akishindwa tu ni vituko hebu kumbukeni masha aliposhindwa na wenje 2010 alikatalia funguo za ofisi haya huyu kagasheki nae katoa kali mwaka huu, kiwia yy ndo nasikia alizimia kbs(bora hata hyu ni mshituko tu) yote tisa wenje ilikuwa shughuli kukubali matokeo mpaka mabomu yalitandikwa na kura kurudiwa zaidi ya mara 3 komesha ya yote wasira alitembeza kichapo na hela kapigwa naiomba serikali kwa taadhima na heshima na unyenyekevu uliotukuka ianzishe malamoja hospital maalumu ya vichaa kanda ya ziwa kama ilivyo milembe dom watu wapimwe akili kwanza kabla ya kuomba kuchaguliwa kuwa viongozi
 
Siku zote inasisitizwa tuwe makini sana na ahadi za wagombea ubunge wanazozitoa majukwaani, hasa zile za kibinadamu ambazo hatuwezi kuwabana kisheria hata kama wasipotimiza,hii imetokea jimbo la mikindani ambapo Hasnein Murji pamoja na kuahidi mwenyewe lakini amesitisha huduma ya kuwasafirisha bure wanafunzi wa shule ya sekondari ya Naliendele baada ya kubwagwa.

Magazeti ya leo yameripoti.
Sasa kama ahadi inaendana na kuchaguliwa ubunge , wewe ulitegemea nini?
Ule cha mtu halafu wewe usitimize ahadi yako!
Huyo mgombea angeendelea kutoa huduma ya bure huku hakuchaguliwa hata mi ningemwona mjinga kabisa!
 
Gazeti la nipashe la leo jumamosi ukurasa wa 8.
Nimechunguza ni kweli wameandika lakini kwa faida yako na wengine, hakuna jimbo la Mikindani... labda wangeandika "aliyekuwa Mbunge wa Mtwara Mjini-Mikindani." Administrative title ya Mtwara Mjini ni kama ile ya Kigoma Mjini, that's Kigoma- Ujiji. Mikindani ni mji Mkongwe wa Mtwara Mjini kama ilivyo kwa Ujiji upande wa Kigoma. Kama sikosei, ofisi nyingi za serikali ndo zipo hapo Mikindani kama ambavyo, bila shaka ilivyo kwa Ujiji upande wa Kigoma! Watu wa Mtwara na Kigoma wanaweza ku-clarify vizuri hili c.c Chinga One
 
Last edited by a moderator:
Mkuu tatizo sio huyo mbunge Murji, tatizo ni chama alichokuwepo CCM . Sisi wana mtwara tulimwambia kama unautaka ubunge tena basi hama chama cha CCM aje upinzani akakataa, SABABU KUBWA YA JIMBO LA MTWARA MJINI KWENDA UPINZANI NI LILE SAKATA LA GESI

Huo ndio ukweli. Nilikuwa huko kabla ya uchaguzi na nilipata kuongea na watu wengi sana wengi wao walimchoka Murji kipitia CCM yake. Wanakwambia tulipigwa sana sababu ni gesi tu. Hata hivyo wengi walisema huduma za kijamii Mtwara ni shida sana labda usafiri eti mtu ukiwa na msiba ndio unapatiwa usafiri na mmbunge. Wanakwambia alikuwa hafanyi maendeleo yoyote zaidi ya kutoa usafiri.
Ila suala la kufuta usafiri hata mimi namuunga mkono maana gharama za uendeshaji ni ngumu wakati hauko bungeni na ndicho alikuwa anategemea.
 
Nimechunguza ni kweli wameandika lakini kwa faida yako na wengine, hakuna jimbo la Mikindani... labda wangeandika "aliyekuwa Mbunge wa Mtwara Mjini-Mikindani." Administrative title ya Mtwara Mjini ni kama ile ya Kigoma Mjini, that's Kigoma- Ujiji. Mikindani ni mji Mkongwe wa Mtwara Mjini kama ilivyo kwa Ujiji upande wa Kigoma. Kama sikosei, ofisi nyingi za serikali ndo zipo hapo Mikindani kama ambavyo, bila shaka ilivyo kwa Ujiji upande wa Kigoma! Watu wa Mtwara na Kigoma wanaweza ku-clarify vizuri hili c.c Chinga One

Uko sawa mikindani ni title tu ya kiutawala yani halmashauri ya wilaya ya mtwara-mikindani(badala ya wilaya ya mtwara mjini) na mtwara mjini linasimama kama jimbo(hakuna jimbo la mikindani).

ila niku sahihishe kidogo chige ni kweli mikindani ni mji mkongwe na wa kihistoria mtwara kama ilivyo kilwa na bagamoyo,but mikindani hakuna ofisi yoyote ya serikali kama ulivyosema.

Asante.
 
Last edited by a moderator:
Kaka sioni kosa hapo. Aliitoa ahadi hio 2010 na alipoupata ubunge Murji aliwapatia usafiri wa bure vijana kuanzia 2011 mpaka October 25, 2015 alipoangushwa. Sasa yeye sio mbunge tena ahadi gani atimize? Wakitaka usafiri kuanzia sasa sio wamuombe huyo mbunge wao mpya?
Hio ndio faida ya kupiga kura kwa ushabiki.
Baniani mbaya kiatu chake dawa? Sasa waitafute dawa kutoka kwa huyo mbunge mpya!

Unashabikia upumbavu......huyo si ndio Murji aliyeshiriki kuhamasisha na kufadhili vurugu Zao Gesi Haitoki Watu wakafa ,wakapata ulemavu ,wakaumia......etc kwa taarifa Mbaya juu yake hata tukashangaa imekuwaje CCM ikampitisha
Zile vurugu Zao gas alifanya akisukumwa na tamaa ya kibiashara kuliko upendo kwa wananachi ......
Aliamini angeweza kupata fursa kueleta malori na mambo mengine
 
Huo ndio ukweli. Nilikuwa huko kabla ya uchaguzi na nilipata kuongea na watu wengi sana wengi wao walimchoka Murji kipitia CCM yake. Wanakwambia tulipigwa sana sababu ni gesi tu. Hata hivyo wengi walisema huduma za kijamii Mtwara ni shida sana labda usafiri eti mtu ukiwa na msiba ndio unapatiwa usafiri na mmbunge. Wanakwambia alikuwa hafanyi maendeleo yoyote zaidi ya kutoa usafiri.
Ila suala la kufuta usafiri hata mimi namuunga mkono maana gharama za uendeshaji ni ngumu wakati hauko bungeni na ndicho alikuwa anategemea.

Kama Ana upendo angeendelea na usafiri kwa kuchaji gharama ...Sio kukomoa
 
Acheni wapate fundisho ambalo litawasaidia wengine kwenye majimbo yao kabla ya kufanya maamuzi.

Lakini hili pia funzo kwa watanzania hasa wale wanaobeza amani iliyopo tanzania na kushabikia vurugu - a bird in hand is better than 1000 on air
 
kanda ya ziwa sijui wabunge wetu wana vielement vya ukichaa yaani akishindwa tu ni vituko hebu kumbukeni masha aliposhindwa na wenje 2010 alikatalia funguo za ofisi haya huyu kagasheki nae katoa kali mwaka huu, kiwia yy ndo nasikia alizimia kbs(bora hata hyu ni mshituko tu) yote tisa wenje ilikuwa shughuli kukubali matokeo mpaka mabomu yalitandikwa na kura kurudiwa zaidi ya mara 3 komesha ya yote wasira alitembeza kichapo na hela kapigwa naiomba serikali kwa taadhima na heshima na unyenyekevu uliotukuka ianzishe malamoja hospital maalumu ya vichaa kanda ya ziwa kama ilivyo milembe dom watu wapimwe akili kwanza kabla ya kuomba kuchaguliwa kuwa viongozi

Nasikia wenje alilambwa kibao mbele ya sumaye ndo akakubali matokeo.
 
Uko sawa mikindani ni title tu ya kiutawala yani halmashauri ya wilaya ya mtwara-mikindani(badala ya wilaya ya mtwara mjini) na mtwara mjini linasimama kama jimbo(hakuna jimbo la mikindani).

ila niku sahihishe kidogo chige ni kweli mikindani ni mji mkongwe na wa kihistoria mtwara kama ilivyo kilwa na bagamoyo,but mikindani hakuna ofisi yoyote ya serikali kama ulivyosema.

Asante.
Oh! Thanks pal... nilishakariri CCM na serikali yake inavyopenda kutumia majengo yaliyoachwa na wakoloni wa kizungu na kiarabu!!! OMG, yaani natoka Lindi halafu Mtwara ckujui... itabidi nichukue hatua ya makasudi!!
 
Siku zote inasisitizwa tuwe makini sana na ahadi za wagombea ubunge wanazozitoa majukwaani, hasa zile za kibinadamu ambazo hatuwezi kuwabana kisheria hata kama wasipotimiza,hii imetokea jimbo la mikindani ambapo Hasnein Murji pamoja na kuahidi mwenyewe lakini amesitisha huduma ya kuwasafirisha bure wanafunzi wa shule ya sekondari ya Naliendele baada ya kubwagwa.

Magazeti ya leo yameripoti.

Vizur sana mlitaka mpewe bure bila kura
 
Kaka sioni kosa hapo. Aliitoa ahadi hio 2010 na alipoupata ubunge Murji aliwapatia usafiri wa bure vijana kuanzia 2011 mpaka October 25, 2015 alipoangushwa. Sasa yeye sio mbunge tena ahadi gani atimize? Wakitaka usafiri kuanzia sasa sio wamuombe huyo mbunge wao mpya?
Hio ndio faida ya kupiga kura kwa ushabiki.
Baniani mbaya kiatu chake dawa? Sasa waitafute dawa kutoka kwa huyo mbunge mpya!

Well said kudadadeq wakome wao c wanapiga kula kishabiki watakula jeuri yao na huyo ustadhi wao waliomchagua dasadeq zao
Yan wana mtwara ni watu wa ajabu sana na itageuka kama lindi muda c mrefu fursa zote zitaondolewa
 
Nimechunguza ni kweli wameandika lakini kwa faida yako na wengine, hakuna jimbo la Mikindani... labda wangeandika "aliyekuwa Mbunge wa Mtwara Mjini-Mikindani." Administrative title ya Mtwara Mjini ni kama ile ya Kigoma Mjini, that's Kigoma- Ujiji. Mikindani ni mji Mkongwe wa Mtwara Mjini kama ilivyo kwa Ujiji upande wa Kigoma. Kama sikosei, ofisi nyingi za serikali ndo zipo hapo Mikindani kama ambavyo, bila shaka ilivyo kwa Ujiji upande wa Kigoma! Watu wa Mtwara na Kigoma wanaweza ku-clarify vizuri hili c.c Chinga One
Asante kwa masahihisho .
 
Last edited by a moderator:
Sasa kama ahadi inaendana na kuchaguliwa ubunge , wewe ulitegemea nini?
Ule cha mtu halafu wewe usitimize ahadi yako!
Huyo mgombea angeendelea kutoa huduma ya bure huku hakuchaguliwa hata mi ningemwona mjinga kabisa!
Ndio maana tunakataa ahadi ya mbunge wako sauli pattaya ya kusomesha wanafunzi watatu , maana ataaminisha watu lakini baada ya kupigwa chini na mahakama ( kama tunavyotarajia ) atawaruka aliowaahidi .
 
Huyu mhindi kiboko ya wapiga kura wa ukawa...sasa wacha wasote na mbunge wao wao wa ukawa ndiyo watajua
Baada ya viongozi wa UKAWA kutambua shida za mtwara mjini wameandaa mpango kabambe sana wa kukwamua huduma za jamii , si huu udhalilishaji ambao ni kinyume hata na maagizo ya Mungu .
 
Back
Top Bottom