Asitisha huduma ya usafiri baada ya kushindwa ubunge

Asitisha huduma ya usafiri baada ya kushindwa ubunge

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
141,507
Reaction score
283,945
Siku zote inasisitizwa tuwe makini sana na ahadi za wagombea ubunge wanazozitoa majukwaani, hasa zile za kibinadamu ambazo hatuwezi kuwabana kisheria hata kama wasipotimiza,hii imetokea jimbo la Mikindani ambapo Hasnein Murji pamoja na kuahidi mwenyewe lakini amesitisha huduma ya kuwasafirisha bure wanafunzi wa shule ya sekondari ya Naliendele baada ya kubwagwa.

Aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Mikindani, mkoani hapa, Hasnein Murji, amesitisha huduma ya usafiri kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Naliendele kufuatia kushindwa ubunge katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 25.
Murji aligombea jimbo hilo kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

Alikuwa akitoa usafiri kwa wanafunzi wa shule hiyo tangu mwaka 2011 alipochaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo.

Wakizungumza na Nipashe kwa nyakati tofauti shuleni hapo, wanafunzi hao walisema kuwa kitendo cha kutochaguliwa mbunge huyo kimewaathiri kiusafiri.

?Tangu alipochaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hili, alitoa magari mawili ambayo yalikuwa yanapokezana, tulikuwa hatulipi nauli, tulikuwa tunawahi vipindi kwa sababu tulikuwa na uhakika wa usafiri,? alisema mmoja wa wanafunzi hao.

Walisema usafiri wa daladala ni mchache, lakini pia wanatozwa nauli ya Sh. 500 badala ya Sh. 200.

Walidai kuwa wakati mwingine wazazi wanashindwa kumudu gharama na kushindwa kufika shuleni kwa sababu ya kukosa nauli.

Walisema hivi sasa wanafunzi wanaofanya mitihani ya kumaliza kidato cha nne wanalazimika kupanda mabasi ya Tandahimba na Newala ili kuwahi kufanya mitihani.

Kharim Mohamed, ni mwanafunzi wa kidato cha tatu, alisema kuwa ukosefu wa usafiri wa uhakika unawafanya wachelewe vipindi na hukaa kituoni kwa saa tatu wakingoja usafiri.

Awali Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Hittu Rashid, alisema shule hiyo ilianza mwaka 1997, na tatizo la usafiri kwa shule hiyo limekuwa la muda mrefu. ?Miaka ya nyuma kabla sijahamia hapa, niliambiwa kwamba wanafunzi walikuwa wakitumia malori ya mchanga kama usafiri wa kuja shuleni, na mwanafunzi mmoja alipata ulemavu baada ya kuvunjika mguu wakati akipanda gari,? alisema.

Alisema, tangu kuwepo kwa usafiri wa uhakika wanafunzi wake wamekuwa na mahudhurio mazuri darasani na utoro ukipungua.

?Kutoka mjini kuja hapa shuleni ni kilomita 12, na kutokana na tatizo la usafiri kwa wanafunzi wangu aliyekuwa mbunge aliona tatizo hili akaamua kuwasaidia, zaidi ya wanafunzi 50 walikuwa wakipanda magari yake bure,? alisema.

Alipoulizwa na Nipashe kuhusu kusitisha usafiri huo, Murji, alikiri kuchukua hatua hiyo tangu Jumatatu iliyopita kwa madai kuwa alikuwa akitoa huduma hiyo kama mbunge wao, lakini sasa sio mbunge tena ni mfanyabishara kama walivyo wengine.

Aliwataka wamuombe mbunge wao wa sasa awasaidie.

Hata hivyo, alisema atatoa magari kwa ajili ya kwenda Mikindani kwa wananchi wote na nauli yake itakuwa Sh. 200 bila kujali umri wa mtu.

Akizungumzia mpango wa kuwasaidia wanafunzi hao hata kwa kuwatoza nauli ili kupunguza makali ya usafiri, Murji alisema: ?Kwa kuwa mimi sio mbunge wao tena nafikiria kama nitaweza huenda nitawapelekea, lakini sijajua itachukua muda gani kurejesha usafiri shuleni hapo,? alisema.


Chanzo: Nipashe
 
Jimbo la mikindani kwenye majimbo ya NEC halipo,halafu mtu anakaa mikindani then secondary anasoma day Naliendele?
 
huku kwetu kuna ametoa milango yote na madirisha ya ofisi iliyokuwa ya mbunge.
 
Hiyo ndio shida ya kushindwa kuweka mifumo. ....mfalme akifa na ufalme unafutika
 
Jimbo la mikindani kwenye majimbo ya NEC halipo,halafu mtu anakaa mikindani then secondary anasoma day naliendele?
Sina hakika kama litakuwa limegawanywa ama kubadilishwa jina , lakini kwenye magazeti limeitwa jimbo la mikindani .
 
Wananchi wamekiuka makubaliano,waliemchagua aendelee na hiyo offer
 
Hehe wakione cha mtema kuni,wabongo tunapenda vya bure tatzo
Alipoulizwa amekiri kuchukua hatua hiyo na kudai kwamba alitoa usafiri wa bure kwa vile alikuwa mbunge wao , lakini kwa sasa amebakia MFANYABIASHARA WA KAWAIDA .
 
dangote yupo atawapa usafiri wasijali,
 
Siku zote inasisitizwa tuwe makini sana na ahadi za wagombea ubunge wanazozitoa majukwaani,hasa zile za kibinadamu ambazo hatuwezi kuwabana kisheria hata kama wasipotimiza,hii imetokea jimbo la mikindani ambapo Hasnein Murji pamoja na kuahidi mwenyewe lakini amesitisha huduma ya kuwasafirisha bure wanafunzi wa shule ya sekondari ya Naliendele baada ya kubwagwa !

Magazeti ya leo yameripoti .

bado singida waanze kuchangishana pesa ya sanda na majeneza, azim dewj hayupo tena. Redio kahama nasikia imeshuzwa tayari hakuna matangazo ya vifo ya bure tena. kule kwa kagasheki matangazo ya kihaya yatapotea sio muda mrefu.
 
Kaka sioni kosa hapo. Aliitoa ahadi hio 2010 na alipoupata ubunge Murji aliwapatia usafiri wa bure vijana kuanzia 2011 mpaka October 25, 2015 alipoangushwa. Sasa yeye sio mbunge tena ahadi gani atimize? Wakitaka usafiri kuanzia sasa sio wamuombe huyo mbunge wao mpya?
Hio ndio faida ya kupiga kura kwa ushabiki.
Baniani mbaya kiatu chake dawa? Sasa waitafute dawa kutoka kwa huyo mbunge mpya!
 
Back
Top Bottom