Asitisha huduma ya usafiri baada ya kushindwa ubunge

Baada ya viongozi wa UKAWA kutambua shida za mtwara mjini wameandaa mpango kabambe sana wa kukwamua huduma za jamii , si huu udhalilishaji ambao ni kinyume hata na maagizo ya Mungu .

Be specific unasema ulikuwa mtwara sasa unasema wameandaa mkakati ambao kimsingi si kweli
Be brilliant
 
wapi niliposema nilikuwa mtwara ? Labda kwa faida yako tu ni kwamba mgombea urais wa UKAWA alimkabidhi kila mgombea wa ubunge mkakati maalum wa kuendeleza jimbo lake .
 
Ndio maana tunakataa ahadi ya mbunge wako sauli pattaya ya kusomesha wanafunzi watatu , maana ataaminisha watu lakini baada ya kupigwa chini na mahakama ( kama tunavyotarajia ) atawaruka aliowaahidi .
Mkuu unategemea nini kutoka kwa Std VII leaver?
 
Nasikia wenje alilambwa kibao mbele ya sumaye ndo akakubali matokeo.

99.9% nakubaliana na ww mkuu hiyo moja naiweka pending ili nijilizishe maana sheria ya makosa ya mitandao imechachamaa balaa sku hizi, inawezekana kabs jamaa alilamba nakoz za kutosha na makofi yasiyo na idadi maana aligoma kabisa kusaini, mabomu yakatandikwa bila idadi naona baada ya kuja sumaye na kumzaba makofi akanywea.
 
Kaka sioni kosa hapo. Aliitoa ahadi hio 2010 na alipoupata ubunge Murji aliwapatia usafiri wa bure vijana kuanzia 2011 mpaka October 25, 2015 alipoangushwa. Sasa yeye sio mbunge tena ahadi gani atimize? Wakitaka usafiri kuanzia sasa sio wamuombe huyo mbunge wao mpya?
Hio ndio faida ya kupiga kura kwa ushabiki.
Baniani mbaya kiatu chake dawa? Sasa waitafute dawa kutoka kwa huyo mbunge mpya!
Bro usijitoe akili....eti kupiga kura kiushabiki...we vp bhana, maamuzi ya wananchi waachie wao huwezi kuwasemea....Murji kafanya nini Mtwara mpaka arejeshwe? Vitu vidogvidogo hivyo ndo uanze kumpa promo hapa? Maamuzi ya WanaMtwara na hatma yao ipo mikononi mwa WanaMtwara na Sio Murji....Sasahivi kuna magari mengi yanaenda kule Naliendele, hiyo sio shida ya kudumu.
 
Siku zote inasisitizwa tuwe makini sana na ahadi za wagombea ubunge wanazozitoa majukwaani, hasa zile za kibinadamu ambazo hatuwezi kuwabana kisheria hata kama wasipotimiza,hii imetokea jimbo la Mikindani ambapo Hasnein Murji pamoja na kuahidi mwenyewe lakini amesitisha huduma ya kuwasafirisha bure wanafunzi wa shule ya sekondari ya Naliendele baada ya kubwagwa.

Kama hao watu wa Mtwara hawamtaki kwa nini aendelee kujipendekeza!? aliyepata naye si katoa ahadi zake, azitekeleze sasa.
 
ubarikiwe sana .
 
Ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Firauni,Bukoba Mbunge aliyebwagwa na nguvu ya Umma Hamis Kagasheki amenyang'anya ambulance aliyokuwa amekabidhi katika Hospitali ya Mkoa na kisha akang'oa dish na TV kubwa aliyokuwa ameweka katika Uwanja wa Mayunga kwa ajili ya wananchi kutazama taarifa za Habari na Vipindi Muhimu.Aidha ameng'oa mitego ya radi (Vifaa vinavyozuia madhara ya radi) iliyokuwa imefungwa maeneo ya Miinuko.Pia kwa hasira kuu amewanyang'anya vijana woote aliokuwa amewapa mikopo ya bodaboda baada ya kushindwa kwa kishindo kikuu na mpinzani wake wa muda mrefu Ndugu Lwakatare...

ingekuwa mimi ningefanya hivyo pia
 
Kama hao watu wa Mtwara hawamtaki kwa nini aendelee kujipendekeza!? aliyepata naye si katoa ahadi zake, azitekeleze sasa.
ni hivi hili ni fundisho kwamba ahadi za kimasikini kama hii hazifai .
 
Siku zote inasisitizwa tuwe makini sana na ahadi za wagombea ubunge wanazozitoa majukwaani, hasa zile za kibinadamu ambazo hatuwezi kuwabana kisheria hata kama wasipotimiza,hii imetokea jimbo la Mikindani ambapo Hasnein Murji pamoja na kuahidi mwenyewe lakini amesitisha huduma ya kuwasafirisha bure wanafunzi wa shule ya sekondari ya Naliendele baada ya kubwagwa.

huyu nadhani yuko sahihi, kama alitoa ahadi ya kuwasafirisha wanafunzi kama njia yake ya kupata ubunge sasa kama wamemnyima hana sababu ya kutoa usafiri huo tena.

tatizo watanzania hawaelewi maana ya mbunge na wanachagua wabunge kwa kuangalia misaada wanayotoa watu binafsi.

mbunge kazi yake si kutoa misaada kwa wananchi bali ni mtu wa kusimamia serikali ili iwatumikie. bunge likifanya kazi yake ipasavyo wanajamii wenyewe au serikali yao watakuwa na uwezo wa kujikimu vishida hivi vidogo. lakini wanachagua wachumia tumbo na wanakwenda kujikomba kwa serikali ili ama wapate nyadhifa serikalini au wapate kandarasi za serikalini na matokeo ni serikali kutokuwa na msimamizi.
 
Kula tano mjomba , maana vile vitufe vya LIKE kwenye kitochi changu sivioni .
 
Kagasheki yeye aliamua kulichukua gali alilotoa kwa ajili ya wagonjwa (mburance) 2010. mara baada ya kuangushwa na rwakatale (cdm) haraka akaluchukua na kufuta ile arama ya red cross.
 
Kagasheki (Bukoba mjini) yeye aliamua kulichukua gali alilotoa kwa ajili ya wagonjwa (mburance) 2010. mara baada ya kuangushwa 2015 na rwakatale (cdm) haraka akalichukua na kufuta ile arama ya red cross na kuligeuza kuwa bodaboda:

Ni ombi tu: ukiamua kutoa, toa kwa moyo wote na kwa upendo kisha sahau; maisha yanaendelea; chaguzi ndo tu kwanza zimeanza, je ukigombea tena na kuwaomba kura haohao ulowanyang'anya watakupa kura tena? ni bora ukiwaachia kwa ajili faida yako in future hata ikitokea ukagombea tena utakuwa na kitu cha kuwakumbusha na wakakumbuka kisha kukurejesha tena bungeni
 
Back
Top Bottom